Saturday, October 25, 2014

HII NDIO HISTORIA YA MZIKI YA MAREHEME YP KUTOKA TMK WANAUME FAMILY

Wiki hii hapa tasnia ya bongofleva ilimpoteza msanii maarufu YP pichani ambaye anaunda kundi la TMK Wanaume Family.Msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Yessaya Ambikile alifariki usiku wakuamkia Jumanne katika hospitali ya Temeke.
Said Fella ambaye ni meneja wa kundi hilo amesema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kifua kwa muda mrefu na ndo kitu ambacho kimechukua uhai wake.
Historia yake katika muziki:
Saidi Fella anasema kuwa alikutana na marehemu YP kwa mara ya kwanza mwaka 2004 katika ukumbi wa King Palace huko Temeke.Baadae kulikuwa na shoo ya TMK Wanaume Family katika ukumbi wa Luxury Pub marehemu akamfata akaomba amsaidie kimziki, ndipo Fella akamwambia amwimbie, akamwimbia wimbo wake uliokuwa unaitwa ‘Saidali’ na huo ndo ukawa mwanzo wakuitwa kwenye kundi hilo. Alivyofika kwenye kundi baada ya kumwambia Juma Nature kuhusu kipaji cha marehemu, Nature akamwambia kama yeye Fella ameona marehemu ana uwezo basi ni sawa apewe nafasi katika kundi hilo.

Mwaka 2005 marehemu pamoja na msanii mwingine wa kundi hilo Y Dash akatoa wimbo wao wa kwanza ‘Shemsa’ ambao ulifanya vizuri na kumtambulisha msanii huyo kwenye tasnia ya muziki.Kutokana na sauti ya marehemu kuendana na msanii mwenzake Y Dash wakatoa wimbo mwingine uliokuwa unaenda kwa jina la ‘Pumzika’.

Said Fella aliendelea kueleza kuwa marehemu alitoa wimbo ulioenda kwa jina la ‘Mapengo matatu’ ambao ni wimbo alioimba kutokana na kufiwa na baba yake,mama yake na mdogo wake.Mwaka 2006 marehemu pamoja na Y Dash ambaye kwasasa yuko nchini Afrika Kusini wakatoa album ya pamoja waliyoipa jina la ‘Mapengo matatu’.
Baada ya hapo marehemu akaendelea kushiriki kwenye kazi zingine za wasanii wa kundi la Tmk Wanaume Family na kazi za kundi kama ‘Twende zetu’ , ‘Dar mpaka Moro’, ‘Kichwa kinauma’ na nyingine nyingi.

Mwaka 2008 marehemu aliamua kuondoka katika kundi hilo na msanii mwenzake Y Dash pamoja na Jebby wakaenda kundi lingine ambalo walilipa jina la TMK Unity.Said Fella anasema mwaka 2010 msanii huyo alimtafuta nakumuomba kurudi katika nafasi yake tena ndipo alipomkubalia nakuwa kwenye kundi hilo mpaka kifo chake.Baada yakurudi TMK Wanaume Family nyimbo ambazo alizoshiriki marehemu nakufanya vizuri ni ‘Kichwa kinauma’, ‘Tunafurahi’ ya Mh Temba na Chegge.

Meneja huyo wa kundi hilo anasema kuwa kundi hilo limepata pengo kwasababu toka mwanzo kabla wakati TMK Wanaume Family kuvunjika msanii huyo alikuwa ni kati ya wale wasanii 11 wa mwanzo.Said Fella alifanunua kuwa alikuwa akianza Juma Nature,Chegge,Kr,Mh Temba na wengine na yeye YP anakuwa na namba.Kitu kingine alisema kuwa watamkumbuka YP kwa ucheshi na ubunifu wa staili za kucheza. “Yaani zile staili zote za TMK Wanaume Family kama mapangashaa nyingi alikuwa akizibuni marehemu pamoja na Kr, alikuwa ni mtu anayependa kucheza, mtu wakutengeza step”, Said Fella.Alieleza kuwa kazi ya mwisho ya kundi marehemu kurekodi ilikuwa ni mwezi uliopita katika studio za Sound Crafters.

Marehemu,Mh Temba na Chegge
Pia msanii wa kundi hilo Chegge alimzungumzia marehemu nakusema kuwa alipatwa na uchungu hadi anajikuta analia kwasababu watu wengi walikuwa wakizifananisha sauti zao na ndo maana alipenda kumshirikisha kwenye nyimbo zake.Msanii mwingine wa kundi hilo Mh Temba alisema kuwa atakumbuka ucheshi wa marehemu na pia ubunifu wake katika kutunga viiitikio(chorus) za nyimbo. “Kwakweli TMK Waunaume Family tumepoteza jembe.

Marehemu Yessaya Ambikile alizikwa jUZI katika makaburi ya Chang’ombe Maduka mawili alizaliwa tarehe 10 November mwaka 1986 jijini Dar es salaam akiwa ni mtoto wa kwanza, kisha akapata elimu ya msingi katika shule ya msingi Keko Magurumbasi.Baada yakumaliza elimu ya msingi marehemu hakuendelea na masomo akaanza kujishughulisha na muziki mpaka kifo chake.Marehemu ameacha mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 8 pamoja na mzazi mwenzake ambaye alikuwa ana mpango wakufunga ndoa hivikaribuni.
Mungu ampuzimshe kwa amani YP.

HAYA NDIO MAKOSA MATATU MAKUBWA DIAMOND ALIYOWAKOSEA WATANZANIA HADI WANAMZOMEA NA KUMCHUKIA….

Katika pitapita zangu Instagram nkakutana na picha na maneno yaliyoandikwa na mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Bikira Wa Kisukuma. Baada ya kusoma nkasema sio mbaya kama ntashea kilichoandikwa na Bikira kwa wasomaji wangu wa Bongoclan. Hebu soma na kisha tupe maoni yako je ni kweli kua Diamond kafanya makosa haya??????

“DIAMOND ANA MAKOSA 3 MAKUBWA ALIYOTUTENDEA WATANZANIA:

1.Kosa la kwanza ni KUWA NA BIDII KWENYE MUZIKI WAKE…Hili ni kosa kubwa sana kwa Watanzania..Hakupaswa kuwa na bidii hivi..Angekuwa tu wa KAWAIDA kama wenzake waliopita ili AFULIE awaachie na wengine waje kwenye chati arudi Tandale kuuza Wali..

2.Kosa la 2 ni KUJITAMBUA YEYE NI NANI..Kwanini ajitambue wakati wenzie wenye majina walishindwa??Kwani yeye nani awe tofauti??Hii ni DHARAU KUBWA sana kwa Watanzania na Wanamuziki wenzie na inaonyesha ana KIBURI..Diamond kujua yeye ni Mwanamuziki mahiri na kutumia VALUE yake aliyoipata kwa mbinde kuiletea sifa Tanzania nje ya Mipaka ni KOSA KUBWA!

3.Kosa lake la 3 ni KUUHESHIMU MNO MUZIKI UNAOMPA HELA…Kwanini asiwe kama wakina Mr nanihii tu,kwani wao hawakuhit kama yeye?Mbona waliishi kawaida tu na kuuchukulia muziki poa hadi walipofulia na leo hata wakiingia Masai Club nobody cares..Kwani kufulia kitu gani?Diamond hakupaswa kuuheshimu Muziki kama kazi..Angefanya bora liende tu aimbe imbe yaishe..Sasa kujifanya Anatoa Collabo mara Davido mara Mafikizolo mara Trey Songs na K’Cee na Yemi Alade AMETUMWA NA NANI??Huku ni kutafuta sifa tu alipaswa awe mdogo milele awaachie na wenzie.. Kwa makosa haya ma3 WATANZANIA wameamua kumuadhibu..Diamond Anaringa…Ana dharau sana..Anaupenda sana Muziki uliompa JINA..HESHIMA..PESA..na ametafutiwa REPLACEMENT kwa sababu tu ANAHESHIMU MUZIKI KAMA KAZI na sio JUST SINGING FOR FAME…Watanzania tumeamua kuadhibu MTU ANAYEHESHIMU KAZI YAKE iliyomtoa from Zero to Hero na tutamshusha kwa lazima taji apewe mwingine..Watanzania tunataka Diamond awe another Mr Nice ili tupate kitu cha KUCOMPARE…Shida yetu kuu wala sio dharau ila ni KWANINI DAI HASHUKI???? Hardwork Pays! Respect Pays! Knowing Your Value Pays! Kama alimpandisha MUNGU…Hakuna wa kumtoa pale… Nasibu..wakomeshe..Toa ule wimbo na MAFIKIZOLO wiki ijayo tuone kama watazomea Spika za redio zao…

CRD BONGOCLAN

DIAMOND AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA KILE KILICHOMKUTA KIWA POLISI, SOMA HAPA…..

Dar es Salaam. Mwanamuziki Nassib Abdul, ‘Diamond Platnumz’ amesalimisha nguo zake za kijeshi kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Diamond alisema kuwa juzi alipokea wito uliomtaka afike kituoni hapo (Oysterbay) akiwa na madansa wake pamoja na nguo hizo. Alisema haikuwa rahisi kwake kutii amri ya vyombo vya dola kwani alikuwa na woga kutokana na kutokuwa na rekodi ya yoyote ya matukio ya uhalifu. “Nisingeweza kukaidi amri ya dola, nilifika na yale mavazi na nikahojiwa kwa saa kadhaa. Nikaeleza kwamba yalikuwa yakifanana na ya jeshi na hayakuwa sare rasmi za jeshi hilo, kikubwa nilihitaji kumaliza tatizo,” alisema nyota huyo aliyetajwa kuwania tuzo za MTV EMA zinazotarajiwa kufanyika Novemba 9 mjini Glasgow, Scotland. Diamond alisema si kweli kwamba alichukuliwa dhamana na Chifu Kiumbe, ila ukweli ni kwamba alisindikizwa na mdau huyo wa sanaa nchini kama kaka yake kutokana na woga aliokuwa nao, lakini hakushikiliwa na kutakiwa dhamana yoyote.

ALIKIBA AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZA KUKODI WATU WA KUMZOMEA DIAMOND FIESTA

Alikiba ameiambia Bongo5 kuwa hajui uvumi huo umeanza vipi. “Hamna ukweli wowote, naanzaje?,” amehoji. “Siwezi kufanya kitu kama hicho. Kikubwa ni kuwashukuru wana Dar es Salaam walivyonipokea, nimefurahi sana. Hii imenitia moyo na kunifanya niongeze bidii kuwaandalia vitu vizuri zaidi.” Katika hatua nyingine, msanii huyo amesema mashabiki wa muziki wake

 BOFYA HAPA KUSOMA ZAID 

MOURINHO AELEZA KUHUSU DIEGO COSTA KUCHEZA AU KUTOCHEZA KWENYE MECHI DHIDI YA MAN UNITED JUMAPILI HII

KOCHA Jose Mourinho ameghairi kumuweka benchi mshambuliaji Diego Costa katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United Jumapili. Mshambuliaji huyo wa kati wa Hispania, amekosa mechi mbili zilizopita katokana na maumivu ya nyama na wiki hii alipelekwa hospitali kwa tiba ya tatizo hilo. Lakini Mourinho, ambaye amethibitisha Loic Remy atakuwa nje kwa wiki tatu zijazo kwa maumivu ya nyonga, amesema mshambuliaji wake huyo nyota ana nafasi ya kwenda Old Trafford. Diego Costa ana nafasi ya kuivaa Manchester United Uwanja wa Old Trafford, amesema kocha wa Chelsea, Jose Mourinho Alipoulizwa leo iwapo Costa atacheza, Mourinho akasema: "Kuna nafasi, ana nafasi ndogo. Diego ana nafasi kidogo, sawa na Ramires na (John Obi) Mikel. Lakini Remy yuko nje na hatacheza. Hana nafasi,". "Kila kitu kilichotokea (kwa Costa). Alikuwa majeruhi kama kawaida- hiyo ilikuwa ni nyama. Ilibidi aende hospitali kwa matibabu, tatizo ambalo tusingeweza kulitatua bila kuwa hospitali kwa usiku mmoja- hiyo ilikuwa kabla ya kucheza na Maribor,"amesema.

Thursday, October 23, 2014

DIAMOND PLATNUMZ NDO HANZO CHA MSANII HUYU WA NYIMBO ZA INJILI KUITISHA MAANDAMANO, SOMA KISA HAPA…

Bongo kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wasanii kua malipo wanayopata pale wanapopata show ni madogo zaidi ukilinganishwa na wanayopewa wasanii wa nje wanapokuja kupiga show Tanzania. Katika pitapita zangu katika website za Kenya nmekutana na picha za maandamano yaliyoandaliwa na msanii wa Kenya ajulikanaye kama Ringtone.
Lengo kubwa la yeye kuanzisha maandamano hayo ni kulalamikia pesa ndogo aliyolipwa katika tuzo za MCSK ambapo alilipwa sh 50,000 ya Kenya ambayo ni sawa na sh 950,000 za kibongo huku Diamond msanii kutoka hapa kwetu akilipwa 1,500,000 za Kenya ambazo ni zaidi ya 28,000,000 za kibongo. Msanii huyo wa nyimbo za injili alilalamikia mfumo mzima wa malipo katika tuzo hizo akisema ni wa Kinyonyaji na unawarudisha nyuma wasanii wa Kenya. Unaweza tazama picha za maandamano hayo hapa chini.

MSANII MIKE TEE AVAMIWA NA AJAMBAZI, ATANGAZA DONGE ONO KWA ATAEIONA GARI HII.

Msanii Mike Tee anaumaliza mwaka vibaya baada ya leo kuvamiwa na watu wenye silaha na kumpora mali zake zenye thamani kibao, Mike Tee ameandika kwenye account yake ya Facebook maneno yafuatayo: “Leo hii asubuhi majira ya saa 05:30 nikiwa naelekea ofisini , nimevamiwa na watu watano wenye mapanga wakiwa na gari aina RAV4 ya silver no. T280AZQ wamechukua laptop yangu MacPro, External HDD 4, Headphones za Sony na Modem . Nnachoshukuru nimepona ila nnachoomba atakayeiona gari hii popote atutaarifu kwa number +255754310202 / na ntampatia cash 300,000 then ntadeal nao mwenyewe”

KUBALI USIKUBALI, MWANA YA ALIKIBA NI DONGO KWA DIAMOND, USHAHIDI HUU HAPA

HUU HAPA UTHIBITISHO.
Mali ni nyingi nyumbani, kipi kimekukimbiza,
Hapa Alikiba, anamwambia Diamond, nyumbani ( SHAROBARO RECORDS) kuna kila kitu, beats kali, management nzuri and all that, kitu gani kilimkimbiza SHAROBARO RECORDS?

Ona babio mamio wote wanakulilia,
HAPA ALIKIBA ANAMAANISHA, SHAROBARO RECORDS, WAKIONGOZWA NA BOB JUNIOR, WOTE WANAMLALAMIKIA DIAMOND KWA KITENDO CHAKE CHA KUKIMBIA KUFANYA KAZI SHAROBARO. (BOB JUNIOR ALIPIGA KELELE SANA DIAMOND ALIPOKIMBIA SHAROBARO RECORDS )

Mtoto pekee ako nyumbani, kipi kimekukimbiza,
HAPA ALIKIBA ANASEMA, DIAMOND ALIKUWA NDO ARTIST PEKEE MKALI ALIYEKUWA CHINI YA SHAROBARO RECORDS. HAKUKUWA NA UPINZANI WOWOTE NDANI YA SHAROBARO, KITU GANI KILIMFANYA AONDOKE ?

Ona babio mamio wote wanakulilia

Ndani ya Dar es salame ulikuja bure
HAPA ALIKIBA ANAMKUMBUSHA DIAMOND, KUWA SIKU ALIPOKWENDA SHAROBARO RECORDS KWA MARA YA KWANZA, HAKUWA NA HATA SENTI TANO NA ALIREKODIWA WIMBO WAKE BURE KABISA.NENO DAR ES SALAME, LIMETUMIKA KUMAANISHA SHAROBARO RECORDS AU MUSIC INDUSTRY.
(KAMA ULIKUKUWA HUJUI, ALIKIBA NI MMOJA KATI YA WANAHISA WA SHAROBARO RECORDS, NA NDIO ALITOA IDHINI KWA BOB JUNIOR, AREKODI BURE WIMBO WA DIAMOND. ILIKUWA HIVI DIAMOND ALIENDA KWA BOB JUNIOR NA KUMWAMBIA ANA WIMBO WAKE ANAOMBA UREKODIWE LAKINI HANA UWEZO WA KIFEDHA, BOB JUNIOR AKAOMBA KUMSIKILIZA, ALIPOMSIKILIZA AKAGUNDUA KIPAJI CHA DOGO, BUT HAKUWA NA MAMLAKA YA KUREKODI WIMBO HUO BURE BILA IDHINI YA BOSS, ALIKIBA, SO IKABIDI AENDE KWANZA KUOMBA IDHINI KWA ALIKIBA, ALIKIBA AKAMWAMBIA BOB JUNIOR KAMA DOGO ANAJUA KUIMBA VIZURI, MREKODIE TU, HAKUNA SHIDA. ALIKIBA ALIYASEMA HAYA AKIWA ANAYAFANYA MAHOJIANO KWENYE KIPINDI CHA MKASI HIVI KARIBUNI.

Tena kimwana, kimwana hujui kuchuna
WAKATI DIAMOND, ANAENDA KUOMBA KUREKODI KWA BOB JUNIOR, ALIKUWA TAYARI KUFANYA SHOW ZAKE HATA BURE ILIMRADI TU AWEZE KUJITANGAZA..DIAMOND ALIWAHI KUMUOMBA ALIKIBA, APANDE NAYE KWENYE SHOW YA ALIKIBA, BILA MALIPO YOYOTE ILI WATU WAMUONE AKIWA NA ALI KIBA. SO ALIKIBA AMETUMIA NENO “KIMWANA ASIYE JUA KUCHUNA” AKIMAANISHA ‘MSANII UNDERGROUND ALIYE TAYARI KUIMBA HATA BILA MALIPO.

Na zile lawama za wale walokuzoeza,
HAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA LAWAMA ZA MADEMU WANAO TOSWA NA DIAMOND

Ulikuja jana na leo tofauti sana.
HAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA NAMNA AMBAVYO DIAMOND AMEBADILIKA KITABIA BAADA YA KUPATA MAFANIKIO KIMUZIKI.

. Tena bora Yule wa jana, wa leo tofauti sana,
HAPA ALIKIBA ANAWAZUNGUMZIA WEMA SEPETU NA PENNY, ANASEMA BORA HATA PENNY KULIKO WEMA AMBAYE NDIO YUPO NA DIAMOND KWA SASA

Dakika mbili mbele nyuma, kichwa kinauma
HAPA ALIKIBA ANAZUNGUMZIA TABIA TABIA ZA WEMA SEPETU. MKOROFI(DAKIKA MBILI MBELE NYUMA), NA MWINGI WA HABARI, AMA PASUA KICHWA ( KICHWA KINAUMA) AMA KICHECHE.

Tena bora Yule wa jana, wa jana leo wa jana,
HAPA ALIKIBA ANASISITIZA ANACHO KIMAANISHA, KWAMBA ANAMZUNGUMZIA WEMA, ” tena bora yule wa jana, wa jana leo wa jana ” YANI YULE AMBAYE UPO NAE LEO, NA AMBAYE ULIWAHI KUWA NAE ZAMANI. NI WA JANA, UPO NAE LEO, LAKINI ULIWAHI KUWA NAYE JANA. HUYO NI WEMA SEPETU, ALIWAHI KUWA NA DIAMOND, WAKAACHANA, WAMERUDIANA TENA. ( ‘WAJANA LEO WA JANA = WEMA SEPETU )

Dakika mbili mbele nyuma, kichwa kinauma
HAPA ALIKIBA ANAKUTOLEA UFAFANUZI ZAIDI KWAMBA, HUYU ” WA JANA LEO WA JANA” SI MWINGINE ILA NI WEMA SEPETU. ANAFANYA HIVYO KWA KUELEZEA TABIA YA WEMA SEPETU AMBAZO NI “UKOROFI” (DAKIKA MBILI MBELE NYUMA ), NA UKICHECHE A.K.A PASUA KICHWA (KICHWA KINAUMA)..KAMA UMESAHAU WEMA SEPETU ALIWAHI KUMTUKANA BOB JUNIOR MATUSI YA NGUONI, KESI IKAENDA MAHAKAMANI..UNAKUMBUKA HIYO?

Oyayee , mbona unawatesa sana,
HAPA ALIKIBA ANAMWAMBIA DIAMOND MBONA UNAWATESA SANA HAO WASICHANA UNAO WABADILISHA BADILISHA ?

Omamee, omame oya mame, omame oya mamee .

.. Mbona unajitesa sana

HAPA ALIKIBA ANAMWAMBIA DIAMOND “WHAT GOES AROUND COMES AROUND”. ANAVYO WATESA HAO WSICHANA, NI SAWA NA KUJITESA MWENYEWE TU. UKICHECHE WA DIAMOND UNAMTESA KIASI CHA KUMFANYA ASHINDWE KUJUA AMPENDE NANI KATIKA MAISHA YAKE, KWA SABABU WANAWAKE KARIBU WOTE ANAO TOKA WANAKUWA NA KASORO ZISIZO VUMILIKA.

Omamee, oya mame, omame oya mamee
Ukaanza kulewa, madawa kuvuta kwa sana.

HAPA ALIKIBA ANATHIBITISHA NAMNA AMBAVYO HALI YA KUWATESA WANAWAKE INAMRUDIA DIAMOND MWENYEWE. BAADA YA KUUMIZWA NA MWANAMKE/WANAWAKE, DIAMOND AKAONA HAKUNA NJIA NYINGINE YA KUPAMBANA NA MAUMIVU YA KUUMIZWA NA MWANAMKE, ZAIDI YA KULEWA. DIAMOND ALITOA WIMBO, ” NATAKA KULEWA” AMBAO ULIKUWA BASED ON TRUE STORY.

Ndani ya Dar Es salaam, mambo matamu hayakukwisha hamu

HAPA ALIKIBA ANAELEZEA NAMNA AMBAVYO DIAMOND HAJAISHIWA NA HAMU YA KUTEMBEA NA WANAWAKE AMBAO ANAWAPATA BAADA YA YEYE KUWA MAARUFU KUPITIA MUZIKI.

We bado mtoto wa mama hujayajua mengi

HAPA ALIKIBA ANAUA NDEGE WAWILI KWA JIWE MOJA., KWANZA ANATOA UFAFANUZI WA MTU ANAYE MZUNGUMZIA. ALIKIBA ANATAKA UJUE KUWA ANAMZUNGUMZIA DIAMOND NA SIO MTU MWINGINE YOYOTE YULE, SO ANAELEZEA JAMBO LINALO ASHIRIA MTU ANAYE MZUNGUMZIA HAPA ” we bado mtoto wa mama “ DIAMOND NI MTOTO WA MAMA, YUPO KARIBU ZAIDI NA MAMA YAKE NA HANA MAWASILIANO MAZURI NA BABA YAKE. ( UKISIKILIZA VIBAYA HAPO UNAWEZA KUDHANI ALIKIBA ANA MAANISHA “MTOTO KWA MAMA”, BUT KIUKWELI ANAMAANISHA “MTOTO WA MAMA” )
NA ANAPOSEMA HUJAYAJUA MENGI, ANAELEZEA MTAZAMO WAKE KUHUSU UPEO WA DIAMOND, KUHUSU MAISHA YA MWANADAMU. ALIKIBA ANA AMINI KUWA DIAMOND BADO HAJAJUA MENGI KUHUSU MAISHA, NDIO MAANA ALIWADHARAU SHAROBARO RECORDS WALIO MTOA PAMOJA NA BABA YAKE MZAZI.

.. Mwenda tezi na omo marejeo ngamani
HAPA ALIKIBA ANAMKUBUSHA DIAMOND ASISAHAU ALIPOTOKA.

Amesema sana mama, dunia tambala bovu

Kuna asali na shubiri ujana giza na nuru

HAPA ALIKIBA ANAMSHAURI DIAMOND, ASICHEZE NA UJANA WAKE NA AKUMBUKE KUWA KUNA WAKATI WA KILA JAMBO, LEO YUPO JUU KIMUZIKI NA KIMAISHA LAKINI KESHO ATAKUWA CHINI. SO AKUMBUKE ALIPOTOKA, ASIJISAHAU.

We mwana wewe mwana, mbona jeuri sana

HAPA ALIKIBA ANA ELEZEA NAMNA AMBAVYO DIAMOND AMEKUWA JEURI BAADA YA KUPATA MAFANIKIO YA KIFEDHA NA KIMUZIKI.

Ulichokifata hukupata , umekosa ulivyo achaa

Kwa baba yako mwana, na mama yako mwana

Kwa vicheche ulivyo vitaka , ni vingi ulivyo achaa,

HAPA ALIKIBA ANAMWAMBIA DIAMOND ” UMEKIMBIA SHAROBARO RECORDS NA KWENDA KWINGINEKO ILI UPATE UPATE MAFANIKIO ZAIDI YA KIMUZIKI NA HATIMAYE UPATE FURSA YA KUN’GOA MADEMU, LAKINI UMEISHIA KUPATA VICHECHE TU KAMA AKINA WEMA SEPETU NA JOKATE. WAKATI VICHECHE KAMA HAO ULIKUWA NA NAFASI YA KUWAPATA HATA KAMA UNGEBAKI SHAROBARO RECORDS. MATOKEO YAKE SASA, WALE MADEMU AMBAO ULIKUWA UNAWATAKA WAKATI UPO SHAROBARO RECORDS ( AMBAO WALIKUWA NA AFFILIATION NA SHAROBARO RECORDS) UMEWAKOSA NA MADEMU AMBAO ULITARAJIA UNGEWAPATA UKIWA NJE YA SHAROBARO RECORDS HUJAWEZA KUWAPATA.

Oyayee, mbona unajitesa sana

Mbona unawatesa sana

( IMESHAELEZEWA JUU )

UNALETA LAWAMA, UNALETA LAWAMA X 2
Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.
Uchungu wa mwana aujuaye mzazi, siku zote leilee
Analiaa oooh oooh oooh oooh
Kutwa nzima analalamika
Obaba baba na mama yako yako, oooh mwana rudi eeeh
Watafurahi wakikuona umerejea salama.

HAPA ALIKIBA AMEFANYA KAMA KUPOTEZA MABOYA VILE ILI ASIONEKANE KAMA ANAMPIGA MADONGO DIAMOND MOJA KWA MOJA.

SOURCE :LIKUD / JAMII FORUM

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BOFYA HAPA ILI HUPATE HABARI KIRAHISI PUNDE ZITUFIKIAPO 

KWELI NIMEAMINI HUYU MISS TANZANIA SIO HALALI.. NI MWONGO WA KUFA MTU...TAZAMA VIDEO ALIVYODANGANYA NA KUBWABWAJA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI

Kwa sasa tuna miss Tanzania mpya aitwaye Sitti Mtemvu ambaye kwa maelezo yake anasema ana miaka 23 huku ushahidi mwingine ukionyesha kua ana zaidi ya miaka 23. Baada ya kuchaguliwa tu watu wengi walianza kulalamika kua Sitti alipewa ushindi huo kwa kupendelewa jambo ambalo hata mimi naona ni la kweli. Jana mwandaaji wa mashindano hayo Lundenga aliitsha mkutano na waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi ya kua mshindi huyo hana miaka 18 kama watu wanavyosema na kuweka vithibitisho ya kua Sitti ana miaka 23 kama cheti chake kinavyosema. Uongo ambao nauona hapa tumedanganywa ni kuhusu hicho cheti ambacho mimi nakiona ni feki ni kua kilitengenezwa mda mfupi kabla ya kuanza mashindano huku cheti cha kwanza ambacho ndicho kilichotumika kutengeneza hadi Passport yake inayoonyesha kua kazaliwa mwaka 1989 kikiwa kimepotea. Na alipoulizwa kilivyopotea ulienda kutoa taarifa kituo gani cha polisi aligoma kutaja. Kwa nini agome na wakati ilikua rahisi tu kutaja jina la kituo cha polisi kama kweli alienda kutoa taarifa?? ni maswali mengi aliulizwa lakini akagoma hii ni dalili kua miss Tanzania wetu ni magumashi matupu. Haiwezekani mtu tunayemwamini akaiwakilishe Tanzania katika mashindano ya dunia ashindwe kujibu maswali muhimu kabisa kuhusu umri wake. Hii ni aibu kubwa kwa Lundenga na nahisi atakua amejifunza kitu na hatarudia kupitisha mamiss kimagumashi hivi, na naamini hata yeye roho inamuuma kwa alichokifanya. Unaweza tazama video ya mahojiano hayo hapa chini :

SHINJI KAGAWA ALIYEONEKANA'WA KAZI GANI' MAN UNITED AENDELEA KUNG'ARA NA UZI WA NJANO AKIINGOZA DORTMUND KUUA 4-0 ULAYA

Kiungo wa zamani wa Manchester United, Shinji Kagawa (kulia) akigombea mpira na mchezaji wa Galatasaray, Felipe Melo katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu nchini Uturuki. Borussia Dortmund imeshinda 4-0, mabao ya Aubameyang dakika ya sita na 18, Reus dakika ya 41 na Ramos dakika ya 83.

LIGI YA MABIGWA: ANGALIA LIVERPOOL ILIVOFANYWA KITU MBAYA NA REALMADRID KATIKA UWANJA WA NYUMBANI

Mambo yameendelea kuwa magumu baada ya Liverpool kuchapwa nyumbani kwa mabao 3-0 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Real Madrid ndiyo walioingusha Liverpool ikiwa nyumbani na Cristiano Ronaldo akapiga bao la kwanza kabla Mfaransa, Karim Benzema kutupia mbili. Juhudi za Liverpool kutaka kusawazisha katika kipindi cha pili hazikuzaa matunda. Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli alionekana kufanya juhudi, lakini hakufurukuta.

LIGI YA MABIGWA ULAYA: MATOKEO YA MECHI KATI YA ANDERLTECH YA UBELGIJI vs ARSENAL HAYA HAPA

Arsenal imejitutumua na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ikiwa ugenini katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Arsenal imeichapa Anderletch ya Ubelgiji katika mechi hiyo iliyoonekana itaisha kwa wenyeji kushinda lakini Arsenal ikafunga mabao mawili katika dakika mbili. Keran Gibbs alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 89, kabla ya Lukas Podolski kufunga la pili katika dakika ya 90.

Wednesday, October 22, 2014

SIMBA SC YAINGIA KATIKA WAKATI MWINGINE MGUMU ZAIDI LIGI KUU

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM BAADA ya mechi nne mfululizo za nyumbani katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC itacheza mechi yake ya kwanza ugenini mwishoni mwa wiki. Simba SC itacheza na Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi, Ikitoka kutoa sare nne katika mechi zote za mwanzo, 2-2 na Coastal Union, 1-1 na Polisi Moro, 1-1 na Stand Unted na 0-0 na Yanga SC. Katika Ligi yetu, nyumbani ni sehemu nzuri ya kuvuna pointi kuliko ugenini, hususan timu za Dar es Salaam zinaposafiri mikoani na kwenda kukutana na viwanja vyenye hali isiyo nzuri sana katika eneo la kuchezea. Sasa Simba SC ndiyo wanaingia katika wakati huo, kwani baada ya mechi na Prisons Jumamosi, wiki inayofuata watakuwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kumenyana na Mtibwa Sugar Novemba 1, kabla ya kurejea tena Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting Novemba 9. Huo utakuwa mchezo wa mwisho kabla ya mapumziko marefu ya karibu mwezi mzima kupisha Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge na michuano ya vijana ya Kombe la Uhai, inayohusisha klabu za Ligi Kuu hadi Desemba 26 ligi hiyo itakaporejea tena. Simba SC haijashinda mechi kati ya nne ilizocheza nyumbani na katika mechi zake tatu zijazo, mbili itacheza ugenini tena dhidi ya timu ambazo zinapokuwa nyumbani kwao, hushinda mara nyingi. Tayari kuna shinikizo la mashabiki kutaka timu ishinde baada ya sare hizo nne za nyumbani- na bahati mbaya Simba SC inakwenda kwenye mchezo mgumu zaidi. Kipa Ivo Mapunda bado hajapona na anahitaji wiki mbili zaidi kabla ya kuanza mazoezi taratibu, Hussein Sharrif ‘Casillas’ naye si wa kumtarajia mwaka huu kucheza- maana yake klabu itacheza mechi hizo ikiwa na kipa mmoja tu, Peter Manyika. Huyo ni wa kumuombea naye asiumie na wala asipate adhabu ya kumzuia kucheza- wakati huo huo wachezaji wengine majeruhi akina Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Miraj Adam, Nassor Masoud ‘Chollo’, Paul Kiongera, Jonas Mkude na Amisi Tambwe mustakabali wao bado haueleweki. Wazi mashabiki wa Simba SC wanatakiwa kushikamana sana na timu yao kwa wakati huu mgumu, wakijua hali halisi kwamba wapo katika kipindi kigumu cha mpito.
Wachezaji wa Simba SC watakuwa na mechi mfululizo za ugenini kuanzia wikiendi hii

PICHA KUTOKA KWENYE MSIBA WA MSANII YP

Aliyekuwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, YP ambaye amefariki usiku wa jana katika hospitali ya Temeke wakati alipokuwa akitibiwa maradhi ya kifua kikuu (TB) anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho katika makaburi ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, YP ambaye jina lake halisi ni Yessaya Ambilikile ameugua kwa kipindi cha takribani miezi 2 kabla ya kufikwa na umauti hapo jana.

 BOFYA HAPA KUTAZAMA PICHA 

LIGI YA MABIGWA: MATOKEO YA BARCELONA vs AJAX HAYA HAPA

BARCELONA imeshinda mabao 3-1 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu wa Camp Nou. Neymar alianza kuifungia Barcelona dakika ya nane kabla ya Lionel Messi kufunga la pili dakika ya 24, Muargentina huyo akitimiza jumla ya mabao 69 aliyofunga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Messi alifunga bao lingine ambalo lilikataliwa na refa kwa kuwa aliotea dakika ya tatu ya kipindi cha pili, lakini Sandro Ramirez aliyetokea benchi akaifungia Barca bao la tatu dakika za majeruhi. Bao pekee la Ajax lilifungwa na Anwar El Ghazi aliyetokea benchi pia. Neymar na Messi wote walipumzishwa kabla ya dakika ya 66 kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi wa El Clasico dhidi ya Real Madrid. Mchezo mwingine wa kundi hilo, PSG imeifunga 1-0 APOEL Nicosia, wakati Kundi H, Shakhtar Donetsk imeichapa 7-0 BATE Borisov na FC Porto imeilaza 2-1 Athletic Bilbao.

HIVI NDO JINSI BAYERN MUNICH ILIVOIPIGA KIPIGO CHA MBWA MWIZI AS ROMA UWANJA WA OLIMPICO MJINI ROME

Home » Unlabelled » BAYERN MUNICH YAITANDIKA ROMA 7-1 NYUMBANI KWAKE BAYERN Munich imeifumua AS Roma mabao 7-1 katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Olimpico mjini Rome, Italia. Thomas Muller aliifungia timu ya Pep Guardiola bao la kwanza dakika ya tisa, kabla ya Mario Gotze kufunga la pili dakika ya 23 na Robert Lewandowski kufunga la tatu baadaye kidogo. Arjen Robben akafunga la nne akimtungua kipa Morgan De Sanctis kabla ya Thomas Muller kufunga la tano kwa mkwaju wa penalti na Franck Ribery na Xherdan Shaqiri waliotokea benchi wakafunga bao la sita na la saba. Bao la kufutia machozi la Roma lilifungwa na Gervinho dakika ya 66. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Manchester City ilitoa sare ya 2-2 ugenini dhidi ya CSKA Moscow.

DROGBA 'ACHEKA NA NYAVU' CHELSEA IKIUA 6-0 LIGI YA MABINGWA

CHELSEA imefanya kile kinachoitwa ‘mauaji’ baada ya kuifumua Maribor mabao 6-0 katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge, London. Loic Remy aliifungia bao la kwanza timu ya Jose Moutinho dakika ya 13 kabla ya kuumia na kumpisha mkongwe Didier Drogba aliyekwenda kufunga bao la pili kwa penalti dakika ya 23. John Terry akafunga bao la tatu kwa shuti la mbali dakika ya 30 kabla ya krosi ya Eden Hazard kutumbukizwa nyavuni na beki wa Maribor Mitja Viler katika harakati za kuokoa. Maribor ilipoteza nafasi ya kupata bao la kufutia machozi, baada ya mkwaju wa penalti wa Agim Ibraimi kugonga mwamba na Hazard akafunga bao la tano kwa penalti na la sita dakika ya 90. Katika mchezo mwingine wa Kundi G, Schalke O4 imeifunga 4-3 na Sporting.

SASA ALEX FERGUSON AHAMUA KUPASUA JIBU KUHUSU DAVID MOYES

KOCHA mstaafu, Sir Alex Ferguson amesema hakuwa na cha kufanya juu ya taratibu zilizotumika kumfukuza David Moyes katika klabu ya Manchester United Aprili mwaka huu na kwamba alichanganyikiwa baada ya kugundua hilo. Ferguson alimchagua Moyes kuwa mrithi wake Old Trafford mwaka uliopita baada ya kustaafu na katika kitabu chake cha sasa ameandika kwamba alikuwa kizani dhidi ya uamuzi uliochukuliwa kumfukuza Mscotland mwenzake huyo. "Nilikuwa Aberdeen wakati hilo linatokea", amekumbushia. "Jumatatu, nilikuwa nasafiri kurudi Manchester na aliyekaa pembeni yangu alikuwa ni kijana ambaye anasoma gazeti lenye habari: "David Moyes kufukuzwa".' Sir Alex Ferguson (kushoto) alikabidhi mikoba yake Manchester United kwa David Moyes (kulia) Moyes alifukuzwa baada ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa Everton Aprili mwaka huu, akiwa ameshinda asilimia 50 tu ya mechi zake Ferguson akasema alichganyikiwa katika ndege akiwa anarejea Manchester na hakuwa na uhakika ajibu vipi meseji aliyotumiwa na Moyes. "Sikuwa na hakika mini kilitokea kwa wakati huo haswa," ameandika akizungumzia meseji hiyo. Ferguson ameasema: "Nikazungumza na (Mtendaji Mkuu) Ed Woodward niliporejea na akasema uamuzi wa mwisho wa waliochukua.' Kwa Moyes, Ferguson pia amesema kwamba kocha huyo wa zamani wa Everton ana safari ndefu akiendelea kusaka kazi mpya. "Katika rekodi yake itaonyesha kwamba aliteuliwa kuwa kocha wa Manchester United, kitu ambacho ni nadra,". Moyes alimaliza katika nafasi ya saba akiwa Manchester United msimu uliopita, na wakati Mscotland huyo anaondoka United aliacha rekodi mbaya zaidi ya mechi za nyumbani tangu mwaka 1978 na pointi chache zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya England. Bado alikuwa ana asilimia nzuri ya ushindi zaidi ya Sir Matt Busby, lakini alipoteza mechi 11 kama kocha wa United, akiruhusu mabao 40 katika mechi 34, kabla ya kufukuzwa siku mbili baada ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa Everton, Aprili 22, mwaka huu katika Ligi Kuu. Ryan Giggs alikaimu nafasi yake kumalizia msimu kabla ya Mholanzi, Louis Van Gaal kuajiriwa msimu huu. Hata hivyo, bado United haijawa na mwenendo mzuri chini ya kocha mpya, licha ya kumwaha fedha nyingi kusajili nyota kadhaa.

Tuesday, October 21, 2014

MSIBA MWINGINE TENA....! BAADA YA KUONDOKEWA NA YP HUYU NI MSANII MWINGINE ALIYEFARIKI SIKU YA LEO

Ni masaa machache tu yamepita tangu muziki wa kizazi kipya Tanzania, Bongo Fleva kumpoteza aliyekuwa staa wa muziki huo kutoka kundi la TMK Wanaume Family, aliyekuwa akifahamika kwa jina la YP, taarifa nyingine ya simanzi inahusu msiba wa aliyekuwa muigizaji wa Bongo Muvi. Katika ukurasa wake wa instagram, muigizaji na mchekeshaji maarufu anayefahamika kwa jina la Kitale ama Mkude Simba (@mkudesimbaoriginal), amepost picha ya muigizaji aliyefariki masaa machache yaliyopita pia. Shery Mwana Kwa mujibu wa Kitale, muigizaji huyo ambaye jina lake halisi ni , aliwahi kushiriki na Kitale katika movie mbali mbali ikiwemo Kipotabo na Nyumba Nne.

ANGEL DIMARIA AZUA HOFU KUBWA MANCHESTER UNITED

WINGA Angel di Maria alionekana hayuko vizuri akiwa ameketi kwenye benchi la Manchester United usiku wa jana, huku amekandamizia barafu katika nyonga yake kwenye mchezo huo ulioisha kwa sare ya 2-2 na West Bromwich Albion. Muargentina huyo, aliyesajiliwa kwa dau la rekodi United, alikuwa kivutio Uwanja wa The Hawthorns, lakini kulikuwa kuna wasiwasi juu ya kiungo huyo baada ya kutolewa dakika ya 76. Di Maria amekuwa katika kiwango babu kubwa tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 60 kutoka Real Madrid msimu huu na ameendeleza mwanzo wake mzuri usiku wa jana. Alimsetia Marouane Fellaini kufunga bao la kusawazisha kipindi cha pili, kabla ya kumpisha Ashley Young. Amecheza mechi tano hadi sasa Manchester United na amefunga mabao matatu na kusaidia manne.
Di Maria (aliyekaa chini kulia) akiwa amekandamizia barafu kwenye nyonga yake huku Chris Smalling, Ander Herrera na Ryan Giggs wakimuangalia kwenye benchi jana Uwanja wa The Hawthorns