Tuesday, September 02, 2014
|
ZENGWE. Manchester United inadaiwa
kubebwa katika usajili wake, baada ya kukiuka
kanuni hususan katika usajili wa mshambuliaji
Radamel Falcao.
Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeandika
kwamba, Falcao amesajiliwa baada ya dirisha
la usajili kufungwa Saa 5:00 usiku jana- wakati
beki Marcos Rojo pamoja kusajiliwa mapema,
lakini bado hajapatiwa visa ya kufanyia kazi.
Inaelezwa Jumatatu ndiyo pazia la usajili
limefungwa, lakini hadi Saa 5:00 usiku
uhamisho wa Falcao ulikuwa haukamilika.
Sheria za usajili zinasema usajili wote uwe
umekamilishwa ifikapo Saa 5:00 usiku wa
kufungwa pazia na baada ya hapo, vielelezo
vyote kama mikataba, makubaliano ya
uhamisho na vibali vya kufanyia kazi
Uingereza lazima viwasilishwe.
Ligi Kuu ya England inaruhusu saa mbili, huo
ni uamuzi wao – lakini uhamisho wa kimataifa
lazima uaendane na mfumo wa FIFA wa
elektroniki (TMS) kufungwa usiku huo.
Mfumo wa FIFA wa TMS ni wa mtandao ambao
unatoa fursa kwa data zote muhimu kuingizwa
ili kuweka sawa uhamisho wa kimataifa.
Angalau usajili wa Rojo wa Pauni Milioni 16
kutoka Sporting Lisbon umekamilika katika
masuala ya kisoka. Amepewa hati ya kimataifa
na Chama cha Soka na aliwasili England wiki
iliyopita kukamilsha dili lake.
Lakini sheria za uhamiaji zinasema wachezaji
wanaoingia nchini humo, lazia wawe na visa za
kufanyia kazi.
Na maofisa wa Ubalozi kwanza watafuatilia
madai ya kwamba kukwama kwa visa yake
kunatokana na ugomvi baina yake na jirani
yake nchini kwao, Argentina mwaka 2010
kabla ya kumpatia visa ya kufanyia kazi, huku
tukio hilo bado linachunguzwa na Polisi.
Lakini wakati wachezaji wa Man United
wamepitishwa pamoja na kuwa nje ya muda au
kukwama kwenye baadhi ya mambo ya msingi
katika usajili wao, wachezaji wengine
wamekwamishwa na hapo ndipo Daily Mail
wanapouliza haki wapi? |
0 comments:
Post a Comment