Posted via Blogaway
MDADISIBLOG
Katika uhusiano kunaweza kutokea ugomvi ambao ni wa kawaida na ambao hauhitaji nguvu kubwa kuumaliza lakini upo ule ambao ukitokea ni lazima nguvu ya ziada itumike ili kuweza kurudi katika mazingira ya amani na furaha.
Kutokana na hilo, leo nimeona nizungumzie mbinu tano zinazoweza kukusaidia katika kumrudisha mpenzi wako ambaye mmezinguana lakini bado unampenda.
Kumbuka wapo ambao wanagombana na inakuwa ndiyo mwisho wa uhusiano kutokana na ukweli kwamba hawakuwa wakipendana kwa dhati.
Lakini kwa wewe ambaye unampenda huyo uliyenaye lakini ikatokea kwa namna moja au nyingine ukamzingua, mambo haya matano yatakusaidia katika kumrudisha kwenye penzi lenu.
Kwanza, fanya kila unavyoweza ujue chanzo cha kutofautiana na kufikia hatua ya kugombana. Ukweli ni kwamba, ili kulitatua vizuri tatizo ni lazima kwanza ujue chanzo chake. Ukishindwa kugundua chanzo cha tatizo, basi na wewe unakuwa sehemu ya tatizo.
Utashangaa wapenzi wengi hugombana na mambo kuwa makubwa kabisa kwa sababu ya mambo madogomadogo ambayo walishindwa kuyagundua mapema na matokeo yake yanazaa tatizo kubwa sana.
Pili, muache kwanza hasira zake ziishe. Kila binadamu ameumbwa akiwa na hasira na kwa bahati mbaya ni wachache wanaoweza kuzidhibiti. Ni rahisi mtu kutukana, kupiga au kuharibu vitu akiwa na hasira.
Baada ya kugombana, kila mmoja lazima atakuwa na hasira na njia pekee inayoweza kuepusha matatizo zaidi, ni kujipa muda na kumpa muda mwenzako ili hasira ziyeyuke.
Ukishaona hasira zenu zimekwisha hapo sasa unaweza kuanzisha mada juu ya kilichosababisha mkagombana. Tumia lugha ya upole kwani endapo utakuwa ukifoka au kuzungumza kwa jaziba, huwezi kuondoa tatizo badala yake itakuwa ni kama unaliongeza.
Tatu, mpe uhuru wa kuzungumza. Huwezi kumuelewa mtu kabla hujampa nafasi ya kuzungumza na kumaliza kile alichokusudia kukisema. Endapo tatizo limetokea na upo kwenye hatua za kusaka amani, mpe mwenzako nafasi ya kueleza dukuduku alilo nalo.
Usimkatishe wala kumbishia chochote, muache aongee ulichomuudhi mpaka dukuduku lake liishe kisha na wewe jieleze kwa ustaarabu.
Nne, itakuwa vyema ukaomba msamaha. Hakuna silaha nzuri inayoweza kukusaidia kuushinda ugomvi wowote na kutuliza mambo kabla hayajawa mabaya kama kuomba msamaha.
Hata kama unaona dhahiri huna makosa, omba msamaha kwanza kisha baada ya hapo anza kumuelewesha ‘mtu’ wako kwa upole. Lazima mwisho na yeye atayaona makosa yake na kukuomba msamaha, mtaweza kuepuka kuukuza ugomvi huo.
Tano, usiweke kinyongo. Endapo umeamua kuomba msamaha kwa mpenzi wako, au yeye amekuomba msamaha, samehe kwa dhati kutoka ndani ya moyo wako na sahau kile kilichotokea.
Ukisamehe kwa dhati, jifunze na kusahau kwani kusamehe kunaenda sambamba na kusahau. Elewa kwamba mpenzi wako ni binadamu ambaye hajakamilika, wala si malaika.Lazima atakuwa akikosea mara kwa mara, endapo utakuwa ukilimbikiza vinyongo, unafuga matatizo makubwa kwani siku nyingine akikukosea hata jambo dogo, utakumbushia na ya jana na juzi na mwisho ugomvi utakuwa mkubwa sana.
Nihitimishe kwa kusema tu kwamba, walio kwenye uhusiano ni sawa na vikombe vilivyo kabatini, yaani kugongana ni kitu cha kawaida. Cha msingi ni wapenzi kujua njia sahihi za kuondoa tofauti zao na kuendelea kuishi maisha yao ya furaha.
Kumbuka ukigombana na huyo leo kisha ukamuacha na kuhamia kwa mwingine, mfumo wako wa kimapenzi utakuwa wa mashaka na unaweza kuonekana hujatulia kwani utakuwa ukiwabadilisha kila mara kwa kuwa tu huwa unagombana na hujui nini ufanye kumaliza mzozo.
Haya ndiyo matokeo ya ligi hiyo kwa leo;-
Newcastle1 – 0 Liverpool FT
Arsenal 3 – 0 Burnley FT
Chelsea 2 – 1 QPR FT
Everton 0 – 0 SwanseaFT
Hull 0 – 1 Southampton FT
Leicester 0 – 1 West Brom FT
Stoke 2 – 2 West Ham FT
MASHABIKI wa Manchester United
wamemchagua kipa David de Gea kuwa
Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa klabu
hiyo, baada ya Mspanyola huyo kupata
asilimia 70 ya jura zilizopigwa kwenye
mtandao.
Licha ya kushindwa kuzuia nyavu zake
kutikiswa katika mchezo wowote mwezi huo,
De Gea alikuwa katika kiwango kizuri wakati
United ikiifunga Everton kabla ya kutoa sare
na West Brom ugenini na baadaye na vinara
wa Ligi Kuu England, Chelsea nyumbani.
Mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka
23 alipangua mkwaju wa penalti Leighton
Baines na kuokoa michomo miwili ya hatari
ya The Toffees dakika za mwishoni,
kuiwezesha timu ya Old Trafford kupata
pointi moja, kabla ya kuokoa mchomo
mwingine wa Eden Hazard wakati Mbelgiji
hjuyo alipopata nafasi nzuri ya kufunga timu
hiyo ikitoka 1-1 na kikosi cha Jose
Mourinho.
ARSENAL imeng’ara katika Ligi Kuu ya
England kufuatia ushindi wa mabao 3-0
dhidi ya Burnley Uwanja wa Emirates,
London.
Hadi mapumziko hakuna bao lililokuwa
limepatikana na iliwachukia hadi robo ya
mwisho ya mchezo, The Gunners kuanza
kuhesabu mabao yao.
Alexis Sanchez alifunga bao la kwanza
dakika ya 70, kabla ya Callum Chambers
kuongeza la pili dakika ya 72 na Sanchez
tena kuwainua vitini mashabiki wa Arsenal
dakika ya 90.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny,
Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs,
Arteta/Ramsey dk63, Flamini, Oxlade-
Chamberlain/Walcott dk80, Cazorla, Sanchez
na Welbeck/Podolski dk80.
Burnley; Heaton, Trippier, Duff, Shackell,
Ward, Arfield 6, Jones, Marney/Chalobah
dk80, Boyd, Ings na Sordell/Jutkiewicz d
REAL Madird imeichapa Granada mabao 4-0
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania,
maarufu La Liga jioni ya leo Uwanja wa
Nuevo Los Carmenes.
Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano
Ronaldo aliifungia Real Madrid bao la
kwanza dakika ya pili, kabla ya James
Rodriguez kufunga la pili kipindi cha kwanza,
Karim Benzema kufunga la tatu dakika ya 54
na James Rodriguez kukamilisha ushindi huo
dakika za mwishoni.
Ushindi huo, unaifanya Real ipae kileleni
mwa La Liga kwa kufikisha pointi 24 baada
ya kucheza mechi 10, lakini imecheza mechi
moja zaidi dhidi ya Barca, wanaochuana nao
kwenye mbio za ubingwa.