Wednesday, October 22, 2014
 |
Home » Unlabelled » BAYERN MUNICH
YAITANDIKA ROMA 7-1 NYUMBANI
KWAKE
BAYERN Munich imeifumua AS Roma mabao
7-1 katika mchezo wa Kundi E Ligi ya
Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa
Olimpico mjini Rome, Italia.
Thomas Muller aliifungia timu ya Pep
Guardiola bao la kwanza dakika ya tisa,
kabla ya Mario Gotze kufunga la pili dakika
ya 23 na Robert Lewandowski kufunga la
tatu baadaye kidogo.
Arjen Robben akafunga la nne akimtungua
kipa Morgan De Sanctis kabla ya Thomas
Muller kufunga la tano kwa mkwaju wa
penalti na Franck Ribery na Xherdan Shaqiri
waliotokea benchi wakafunga bao la sita na
la saba. Bao la kufutia machozi la Roma
lilifungwa na Gervinho dakika ya 66. Mchezo
mwingine wa kundi hilo, Manchester City
ilitoa sare ya 2-2 ugenini dhidi ya CSKA
Moscow. |
0 comments:
Post a Comment