Sunday, December 21, 2014

REAL MADRID MABINGWA WA DUNIA, WABEBA KOMBE AFRIKA

Unaweza kusema kweli huu ni mwaka wa Real Madrid, kwani wamefanikiwa kuitwanga San Lorenzo kwa mabao 2-0 na kubeba ubingwa wa dunia. Madrid wametupia mabao hayo mawili kupitia kwa Sergio Ramos na Gareth Balena kubeba Kombe hilo katika ardhi ya bara maarufu la Afrika. Mechi hiyo ya fainali ya Kombe la Dunia kwa klabu, imepigwa mjini Marakech, Morocco. Cristiano Ronaldo hakuweza kufunga katika mechi hiyo ambayo Madrid imeshinda mara 21 mfululizo. Kwa mwaka huu, Madrid imebeba makombe ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Copa del Rey na Super Cup ya Ulaya.

Posted via Blogaway

Wednesday, November 19, 2014

Njia 5 za kumrudisha mpenzi wako baada ya kuzinguana

Katika uhusiano kunaweza kutokea ugomvi ambao ni wa kawaida na ambao hauhitaji nguvu kubwa kuumaliza lakini upo ule ambao ukitokea ni lazima nguvu ya ziada itumike ili kuweza kurudi katika mazingira ya amani na furaha.
Kutokana na hilo, leo nimeona nizungumzie mbinu tano zinazoweza kukusaidia katika kumrudisha mpenzi wako ambaye mmezinguana lakini bado unampenda.
Kumbuka wapo ambao wanagombana na inakuwa ndiyo mwisho wa uhusiano kutokana na ukweli kwamba hawakuwa wakipendana kwa dhati.
Lakini kwa wewe ambaye unampenda huyo uliyenaye lakini ikatokea kwa namna moja au nyingine ukamzingua, mambo haya matano yatakusaidia katika kumrudisha kwenye penzi lenu.

Kwanza, fanya kila unavyoweza ujue chanzo cha kutofautiana na kufikia hatua ya kugombana. Ukweli ni kwamba, ili kulitatua vizuri tatizo ni lazima kwanza ujue chanzo chake. Ukishindwa kugundua chanzo cha tatizo, basi na wewe unakuwa sehemu ya tatizo.
Utashangaa wapenzi wengi hugombana na mambo kuwa makubwa kabisa kwa sababu ya mambo madogomadogo ambayo walishindwa kuyagundua mapema na matokeo yake yanazaa tatizo kubwa sana.

Pili, muache kwanza hasira zake ziishe. Kila binadamu ameumbwa akiwa na hasira na kwa bahati mbaya ni wachache wanaoweza kuzidhibiti. Ni rahisi mtu kutukana, kupiga au kuharibu vitu akiwa na hasira.
Baada ya kugombana, kila mmoja lazima atakuwa na hasira na njia pekee inayoweza kuepusha matatizo zaidi, ni kujipa muda na kumpa muda mwenzako ili hasira ziyeyuke.
Ukishaona hasira zenu zimekwisha hapo sasa unaweza kuanzisha mada juu ya kilichosababisha mkagombana. Tumia lugha ya upole kwani endapo utakuwa ukifoka au kuzungumza kwa jaziba, huwezi kuondoa tatizo badala yake itakuwa ni kama unaliongeza.

Tatu, mpe uhuru wa kuzungumza. Huwezi kumuelewa mtu kabla hujampa nafasi ya kuzungumza na kumaliza kile alichokusudia kukisema. Endapo tatizo limetokea na upo kwenye hatua za kusaka amani, mpe mwenzako nafasi ya kueleza dukuduku alilo nalo.

Usimkatishe wala kumbishia chochote, muache aongee ulichomuudhi mpaka dukuduku lake liishe kisha na wewe jieleze kwa ustaarabu.

Nne, itakuwa vyema ukaomba msamaha. Hakuna silaha nzuri inayoweza kukusaidia kuushinda ugomvi wowote na kutuliza mambo kabla hayajawa mabaya kama kuomba msamaha.

Hata kama unaona dhahiri huna makosa, omba msamaha kwanza kisha baada ya hapo anza kumuelewesha ‘mtu’ wako kwa upole. Lazima mwisho na yeye atayaona makosa yake na kukuomba msamaha, mtaweza kuepuka kuukuza ugomvi huo.

Tano, usiweke kinyongo. Endapo umeamua kuomba msamaha kwa mpenzi wako, au yeye amekuomba msamaha, samehe kwa dhati kutoka ndani ya moyo wako na sahau kile kilichotokea.

Ukisamehe kwa dhati, jifunze na kusahau kwani kusamehe kunaenda sambamba na kusahau. Elewa kwamba mpenzi wako ni binadamu ambaye hajakamilika, wala si malaika.Lazima atakuwa akikosea mara kwa mara, endapo utakuwa ukilimbikiza vinyongo, unafuga matatizo makubwa kwani siku nyingine akikukosea hata jambo dogo, utakumbushia na ya jana na juzi na mwisho ugomvi utakuwa mkubwa sana.

Nihitimishe kwa kusema tu kwamba, walio kwenye uhusiano ni sawa na vikombe vilivyo kabatini, yaani kugongana ni kitu cha kawaida. Cha msingi ni wapenzi kujua njia sahihi za kuondoa tofauti zao na kuendelea kuishi maisha yao ya furaha.
Kumbuka ukigombana na huyo leo kisha ukamuacha na kuhamia kwa mwingine, mfumo wako wa kimapenzi utakuwa wa mashaka na unaweza kuonekana hujatulia kwani utakuwa ukiwabadilisha kila mara kwa kuwa tu huwa unagombana na hujui nini ufanye kumaliza mzozo.

HIKI NDO KITU KIKUBWA ALICHOKIFANYA ROONEY DHIDI YA SCOTLAND

ENGLAND imewalaza wenyeji Scotland mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa usiku huu. Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 32 na Wayne Rooney aliyefunga mabao mawili dakika za 47 na 85, wakati bao pekee la wenyeji lilifungwa na Andrew Robertson dakika ya 83. Kwa kufunga mabao hayo mawili, Rooney amekuwa mchezaji wa tatu kufunga mabao mengi katika historia ya timu ya taifa ya England kutokana na kufikisha mabao 45, akimpita Jimmy Greaves. Kikosi cha Scotland kilikuwa: Marshall/Gordon dk46, Whittaker, R Martin, Hanley/May dk66, Robertson, Maloney, Mulgrew, Brown/D Fletcher dk46, Anya/Bannan dk61, C Martin/ Morrison dk46 na Naismith. England: Forster, Clyne, Cahill/Jagielka dk46, Smalling, Shaw/Gibbs dk66, Oxlade- Chamberlain, Milner, Wilshere/Barkley dk87, Downing/Lallana dk46, Rooney na Welbeck/ Sterling dk46.

JB kuja na filamu ya soka la Bongo

Muigizaji mahari wa filamu, Jacob Stephan aka JB, amesema yupo mbioni kuandaa filamu kuhusu soka la Tanzania. JB ambaye ni shabiki mkubwa Simba alisema hayo kwenye kipindi cha Kili Chart Show cha EATV baada shabiki mmoja kumuuliza kama ana mpango wa kufanya filamu ya aina hiyo. “Kwa sababu wengi wameguswa nitafanya tena filamu nyingine ya mpira, ambayo nitazungumzia moja kwa moja, mpira wa kitanzania, wazo lako nitalifanyiwa kazi na Jerusalem film,” alisema JB.

Baada ya Mabasi ya Mwendokasi, Kivuko cha Mv. Dar, hii ni nyingine kuhusu usafiri Dar.

Baada ya Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi, Treni, Kivuko cha Mv. Dar es Salaam, leo kuna taarifa nyingine nzuri ambayo inahusu jitihada za Serikali kumaliza tatizo sugu la foleni katikati ya jiji la Dar es Salaam. Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha TBC1 , Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli amesema; “… Tuliwatuma wataalamu hawa, na bahati nzuri Chief Executive wa TANROADs hivi karibuni na wataalamu wenzake walienda South Korea.. Serikali ya South Korea imekubali kutufadhili kujenga flyover nyingine pale.. na barabara yenyewe itakuwa na urefu wa karibu kilomita 7.2 na barabara itaanzia Coco Beach, itapita baharini itakuja kutokea Agakhan Hospital na kuja ku-join na barabara nyingine hii ya Alli Hassan Mwinyi… ” “.. Tumepanua maeneo pengine kote.. tuna mradi wa BRT ambao una-involve kilometa zaidi ya ishirini na moja na karibu sasa hivi unaisha chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia, lakini tunapofika pale Salenda pamekuwa na tatizo kubwa na kwa sasa hivi katika traffic count ya magari yanayopita pale kwa siku yamezidi zaidi ya magari hamsini na moja elfu kwa hiyo hawawezi wakaya-accommodate magari yote yanayoweza kupita sehemu hiyo… ”– Dk. Magufuli

Wednesday, November 12, 2014

Nuh mziwanda afunguka kuhusu kupewa kichapo na mpenzi wake kila anapokosea

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amefunguka kuwa watu wanaomsema vibaya kuhusu yeye kupewa kichapo na mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wanakosea kwani anaamini kufanywa hivyo ni mahaba. Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Mziwanda alisema kuna taarifa zimeenea kuwa huwa anapigwa na Shilole pindi anapokosea lakini ukweli si kupigwa ‘live’ bali ni kupigwa kimahaba. ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake ‘Nuh Mziwanda’. “Jamani kupigwa wanakozungumzia watu sielewi lakini mimi ananipiga kimahaba, wanaosema kuwa mpenzi wangu ananipiga washindwe, watuache kwa raha zetu,”alisema Shilole. Tupe maoni yako hapo Chini kuhusu wawili hawa..!!

Saturday, November 01, 2014

Hiki ndicho kilichotokea ligi kuu England leo, matokeo ya michezo yote yapo hapa

Haya ndiyo matokeo ya ligi hiyo kwa leo;-

Newcastle1 – 0 Liverpool FT

Arsenal 3 – 0 Burnley FT

Chelsea 2 – 1 QPR FT

Everton 0 – 0 SwanseaFT

Hull 0 – 1 Southampton FT

Leicester 0 – 1 West Brom FT

Stoke 2 – 2 West Ham FT

DE GEA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MAN UNITED KWA ASILIMIA 70

MASHABIKI wa Manchester United
wamemchagua kipa David de Gea kuwa
Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa klabu
hiyo, baada ya Mspanyola huyo kupata
asilimia 70 ya jura zilizopigwa kwenye
mtandao.
Licha ya kushindwa kuzuia nyavu zake
kutikiswa katika mchezo wowote mwezi huo,
De Gea alikuwa katika kiwango kizuri wakati
United ikiifunga Everton kabla ya kutoa sare
na West Brom ugenini na baadaye na vinara
wa Ligi Kuu England, Chelsea nyumbani.
Mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka
23 alipangua mkwaju wa penalti Leighton
Baines na kuokoa michomo miwili ya hatari
ya The Toffees dakika za mwishoni,
kuiwezesha timu ya Old Trafford kupata
pointi moja, kabla ya kuokoa mchomo
mwingine wa Eden Hazard wakati Mbelgiji
hjuyo alipopata nafasi nzuri ya kufunga timu
hiyo ikitoka 1-1 na kikosi cha Jose
Mourinho.

ARSENAL YAUA 3-0 ENGLAND, SANCHEZ MBILI PEKE YAKE

ARSENAL imeng’ara katika Ligi Kuu ya
England kufuatia ushindi wa mabao 3-0
dhidi ya Burnley Uwanja wa Emirates,
London.
Hadi mapumziko hakuna bao lililokuwa
limepatikana na iliwachukia hadi robo ya
mwisho ya mchezo, The Gunners kuanza
kuhesabu mabao yao.
Alexis Sanchez alifunga bao la kwanza
dakika ya 70, kabla ya Callum Chambers
kuongeza la pili dakika ya 72 na Sanchez
tena kuwainua vitini mashabiki wa Arsenal
dakika ya 90.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny,
Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs,
Arteta/Ramsey dk63, Flamini, Oxlade-
Chamberlain/Walcott dk80, Cazorla, Sanchez
na Welbeck/Podolski dk80.
Burnley; Heaton, Trippier, Duff, Shackell,
Ward, Arfield 6, Jones, Marney/Chalobah
dk80, Boyd, Ings na Sordell/Jutkiewicz d

RONALDO AFUNGA REAL MADRID IKISHINDA 4-0 LA LIGA NA KUPANDA KILELENI

REAL Madird imeichapa Granada mabao 4-0
katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania,
maarufu La Liga jioni ya leo Uwanja wa
Nuevo Los Carmenes.
Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano
Ronaldo aliifungia Real Madrid bao la
kwanza dakika ya pili, kabla ya James
Rodriguez kufunga la pili kipindi cha kwanza,
Karim Benzema kufunga la tatu dakika ya 54
na James Rodriguez kukamilisha ushindi huo
dakika za mwishoni.
Ushindi huo, unaifanya Real ipae kileleni
mwa La Liga kwa kufikisha pointi 24 baada
ya kucheza mechi 10, lakini imecheza mechi
moja zaidi dhidi ya Barca, wanaochuana nao
kwenye mbio za ubingwa.

Friday, October 31, 2014

TORRES AFUNGUKA RASMI KUHUSU MOURINHO JUU YA KUONDOKA KWAKE CHELSEA

Mshambuliaji nyota wa Chelsea anayekipiga AC Milan kwa mkopo amesema hakuondoka katika klabu hiyo ya London kwa kulazimishwa na Kocha Jose Mourinho. Torres raia wa Hispania amesema ulikuwa ni uamuzi wake kufanya na maneno yake yameondoa taarifa za utata kwamba Mourinho ndiye alimtaka kwenda Milan kwa mkopo wa miaka miwili.

RASMI ANGA FIFA YAACHIA NEMBO YA KOMBE LA DUNIA 2018, WANA ANGA WA WAITANGAZA

NEMBO ITAKAYOTUMIKA KWENYE KOMBE LA DUNIA MWAKA 2018 NCHII RUSSIA IMEANIKWA HADHARANI KUPITIA WANA ANGA WA NCHI HIYO. WALE JAMAA AMBAO HUENDA MWEZINI. SASA IKO WAZI NA INAJULIKANA IKIWA NI BAADA YA ILE YA ZAKUMI YA AFRIKA KUSINI MWAKA 2010 NA ILE YA BRAZIL 2014.

Wednesday, October 29, 2014

RONALDO APIGA HAT TRICK YA TUZO LA LIGA, MESSI AAMBULIA PATUPU

Cristiano Ronaldo amekomba zawadi tatu 'hat trick' za tuzo ya wachezaji bora Ligi ya Hispania maarufu kama La Liga. Huku mpinzani wake Lionel Messi akiambulia patupu, tuzo tatu alizobeba Ronaldo ni pamoja na Mchezaji Bora, Mfungaji Bora na Mshambuliaji Bora wa La Liga. Ilikuwa furaha kubwa kwa Ronaldo ambaye aliongozana na mpenzi wake Iryna Shayk, mwanamitindo kutoka Urusi. Pamoja na Ronaldo kubeba tuzo hizo, timu yake ya Real Madrid imetawala zaidi kuliko klabu nyingine ya Hispania. Zawadi ya kiungo bora imekwenda kwa Luka Modric huku Sergio Ramos akichukua tuzo ya beki bora. Kipa mpya wa Real Madrid, Keylor Navas amechukua tuzo ya mlinda mlango bora. Kabla ya kutua Madrid, Navas alikuwa akikipiga Levante. Barcelona pia imefanikiwa kupata tuzo tatu, Andrés Iniesta alitangazwa kuwa kiungo bora mshambuliaji, huku Ivan Rakitic na Rafinha wakitwaa tuzo mbili za Fair Play and Breakthrough. Kutokana na mafanikio makubwa msimu uliopita, Kocha wa Atlético, Diego Simeone alibeba tuzo ya Kocha Bora. Mshambuliaji nyota wa Sevilla, Carlos Bacca akachukua tuzo mchezaji Bora kutoka Amerika Kusini na Yacine Brahimi wa Granada akawa Mchezaji Bora kutoka Afrika.

RAY C AHAMUA KUMFUTIA KESI CHID BENZ KESI!

Rehema Chalamila ‘Ray C’. WAKATI nyota wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ akikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na madawa ya kulevya akiwa njiani kuelekea Mbeya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliyekuwa amemfungulia kesi ya kumpiga katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, amefuta shauri hilo na kumsamehe. Akipiga stori na gazeti hili, Ray C alisema ameamua kumsamehe kwa sababu yeye ni mtu wa Mungu na anaamini yanayomtokea ni ishara ya kumtambulisha kuwa matumizi ya dawa za kulevya hayafai. “Mimi ni mtu wa Mungu, nimemsamehe na wala sitaki kesi naye, lakini kumsamehe mimi peke yangu hakusaidii, Watanzania wote kwa pamoja tumuombee ili jambo hili limalizike na likiisha, ninamuomba aje tushiriki pamoja katika tiba ya Methadone,” alisema. Ray C maarufu kama kiuno bila mfupa, alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuandika waraka katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram, akimsihi Chid Benz kuachana na matumizi hayo ya madawa ya kulevya.
Nyota wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’. “Pole kaka yangu Chid Benz, naumia kuona tatizo ulilokuwa nalo bado haujalitafutia jibu, mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi pamoja. Tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu,” yalisomeka baadhi ya maandishi yake mtandaoni. Ray C aliendelea kuandika kuwa kitendo cha kukamatwa kwake na madawa hayo kitakuwa ni jibu zuri kwake kuwa anakoenda si salama na kumtaka abadili njia na kuungana naye kwenye tiba ya Methadone kwani ndiyo kiboko ya madawa ya kulevya.
Kamanda Nzowa. Chid Benz alikamatwa akiwa na kete 14 za madawa ya kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, alikuwa bado hajafikishwa mahakamani kukabiliana na tuhuma hizo.

HIKI NDO KITU KIKUBWA ALICHOKIFANYA BALOTEL AKITOKEA BENCHI USIKU HUU DHIDI YA SWANSEA

KLABU ya Liverpool imeichapa Swansea mabao 2-1 katika mchezo wa Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Capital One Cup usiku huu Uwanja wa Anfield. Jordan Henderson alipewa beji ya Unahodha, kocha Brendan Rodgers akifanya mabadiliko ya wachezaji tisa katika kikosi chake cha kwanza. Winga wa Swans, Marvin Emnes aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 65, kabla ya Mario Balotelli aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Rickie Lambert kusawazisha zikiwa zimesalia dakika tano. Federico Fernandez alitolewa kwa kadi nyekundu dakika za mwisho kwa kumchezea rafu Philippe Coutinho kabla ya Dejan Lovren kuifungia Liverpool bao la ushindi dakika za majeruhi na kuwapeleka Wekundu hao Robo Fainali.

CPL:MATOKEO YA CHELSEA vs SHREWBURY HAYA HAPA

KLABU ya Chelsea imetinga Robo Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup baada ya kuichapa mabao 2-1 Shrewsbury usiku huu. Chelsea ilipata bao la kwanza mapema tu kipindi wakati mkongwe, Didier Drogba alipomalizia pasi maridadi ya mwanasoka wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah. Lakini Shrewsbury ikapata bao la kusawazisha kupitia kwa Andrew Mangan aliyetokea benchi dakika ya 77, kabla ya Jermaine Grandison kujifunga dakika nne baadaye kuipa ushindi timu ya Jose Mourinho.

Tuesday, October 28, 2014

Kingine alichozungumza Jackie Chan kuhusiana na mtoto wake kukamatwa na dawa za kulevya.

Mkali wa movie kutoka Hong Kong China, Jackie Chan ameomba vyombo vya habari ‘vijichunge’ na namna vinavyoandika taarifa kuhusiana na kitendo cha mtoto wake kukamatwa na dawa za kulevya kwa kuwa kufanya hivyo si kumuumiza yeye (Jackie Chan) bali ni kumuumiza mama wa mtoto huyo. Jackie Chan amesema kupitia tukio hilo amejifunza kuwa baba bora kitu ambacho hakukijua siku za nyuma. Mtoto wa staa huyo, Jaycee Chan alikamatwa kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi zaidi ya gramu 100 ndani ya nyumba yake, na baadaye kushitakiwa kwa kuuza dawa hizo. Jackie Chan ambaye amekuwa balozi wa kupinga dawa za kulevya tangu mwaka 2009, amesononeshwa na pia ameomba radhi kwa kosa alilotenda mwanae ambapo hii imekuwa mara yake ya kwanza kujibu swali linalohusiana na kesi ya mtoto wake, akisema kupitia hilo amejifunza kuwa baba bora.

Monday, October 27, 2014

NUH MZIWANDA AHAMUA TENA KUWANYAMAZISHA WANAFKI KWA KUCHORA TATOO NYINGINE YENYE PICHA YA MPENZI WAKE SHILOLE

Wakati Nick Cannon ametoka kufunika Tattoo yenye jina la mke wake Mariah Carey ambaye wametengana kwa kuongeza mchoro mwingine juu yake hivi karibuni, msanii wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda ameongeza Tattoo ya pili ya mpenzi wake Shilole kwenye mkono wake. Nuh amesema mchoro huo wa pili kwenye mwili wake una sura ya Shishi baada ya ile ya kwanza ambayo ni jina la ‘Shishi Bybee’. “Tattoo ya pili ni sura aisee sura ya mpenzi wangu Shishi,” ameiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm. “nimetaka kuweka maana ya jina pamoja na sura yake unajua jina tu lilikuwepo kukamilisha upendo ule na thamani na shkurani kwake so nilichora ile Shishi Bybee ya maneno halafu baadae nimechora sura yake, nimechora mkono ule ule, so hii shishi Bybee iko nyuma ya mkono wangu halafu hii sura yake iko mbele.”
Mziwanda ameongeza kuwa mchoro huo umegharimu shilingi laki nne na nusu. “Tattoo nimechora juzi, tumetumia kama laki nne hivi nne na nusu ukijumlisha na usafiri sababu jamaa alikua katoka Arusha. Ile ya mwanzo iligharimu kama laki mbili mbili na nusu”.

Sunday, October 26, 2014

HII NDO TIMU ANAYOTARAJIA KUTUA DAVID MOYES

KOCHA David Moyes yumo kwenye orodha fupi ya mwisho ya makocha wanaotakiwa na Inter Milan ya Italia inayotaka kumtimua kocha wake wa sasa, Walter Mazzarri. Kocha huyo wa zamani wa Manchester United na Everton anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Mazzarri, ambaye timu yake inacheza na Cesena leo akiwa katika shinikizo baada ya mwanzo mbaya unaoifanya Inter iwe katika nafasi ya tisa kwenye msiamo wa ligi hivi sasa. Moyes mwenyewe amekua akiamini akipata nafasi ya kufundisha klabu nje ya Uingereza itakuwa ni fursa nzuri kwake kurejesha heshima yake- hivyo akifanikiwa mpango huo atakuwa ametimiza ndoto zake kwa sasa.

Saturday, October 25, 2014

JE UNAFAMAMU NI WASANII GANI WA BONGO WALIMSHTUA SANA DAVIDO KWENYE FIESTA 2014 DAR

Unaambiwa weekend iliyopita kwenye Fiesta ya Dar es salaam mwimbaji Davido wa Nigeria alitumia dakika zake zote kutazama screen zilizokua zimewekwa nyuma ya stage ya Fiesta baada ya kusikia shangwe zilizokua zinapigwa baada ya Wakali wengine kupewa time ya kumiliki stage. Alilazimika kutazama TV hizo kwa umakini baada ya kuona shangwe walilopata WEUSIambapo mashabiki walikua wanaimba nyimbo zao kwa muda mrefu ambapo Davido kabla ya kuuliza alitumia muda mrefu kuwatazama kwa makini baada ya kushangazwa na shangwe walilokua wanapata WEUSI hawa.
Baada ya Wakali hawa kumaliza show Davido alianza kuuliza ni kina nani na wana umaarufu kiasi gani ambapo mmoja wa marafiki zake amesema stori hazikuishia uwanjani kwenye Fiesta bali mpaka Hotelini Davido alionyesha kushangazwa na shangwe la WEUSI na kuwaongelea tena. Hii itafanya idadi ya Wasanii wa bongo wanaofahamika na Davido iongezeke manake alipokuja juzi Tanzania alihojiwa muda mfupi tu baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege na kusema msanii pekee wa Tanzania anaemfahamu ni Diamond Platnumz. Mengine aliyoyasema ni kwamba kwenye album yake mpya inayotoka mwanzoni mwa 2015 wameshirikishwa wasanii wachache kutoka Afrika ambao ni pamoja na Diamond na Mafikizolo na kwamba kuna wasanii wawili wakubwa wa kimataifa aliowashirikisha ambao hatowataja kwa sasa