Wednesday, October 22, 2014

SASA ALEX FERGUSON AHAMUA KUPASUA JIBU KUHUSU DAVID MOYES

KOCHA mstaafu, Sir Alex Ferguson amesema hakuwa na cha kufanya juu ya taratibu zilizotumika kumfukuza David Moyes katika klabu ya Manchester United Aprili mwaka huu na kwamba alichanganyikiwa baada ya kugundua hilo. Ferguson alimchagua Moyes kuwa mrithi wake Old Trafford mwaka uliopita baada ya kustaafu na katika kitabu chake cha sasa ameandika kwamba alikuwa kizani dhidi ya uamuzi uliochukuliwa kumfukuza Mscotland mwenzake huyo. "Nilikuwa Aberdeen wakati hilo linatokea", amekumbushia. "Jumatatu, nilikuwa nasafiri kurudi Manchester na aliyekaa pembeni yangu alikuwa ni kijana ambaye anasoma gazeti lenye habari: "David Moyes kufukuzwa".' Sir Alex Ferguson (kushoto) alikabidhi mikoba yake Manchester United kwa David Moyes (kulia) Moyes alifukuzwa baada ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa Everton Aprili mwaka huu, akiwa ameshinda asilimia 50 tu ya mechi zake Ferguson akasema alichganyikiwa katika ndege akiwa anarejea Manchester na hakuwa na uhakika ajibu vipi meseji aliyotumiwa na Moyes. "Sikuwa na hakika mini kilitokea kwa wakati huo haswa," ameandika akizungumzia meseji hiyo. Ferguson ameasema: "Nikazungumza na (Mtendaji Mkuu) Ed Woodward niliporejea na akasema uamuzi wa mwisho wa waliochukua.' Kwa Moyes, Ferguson pia amesema kwamba kocha huyo wa zamani wa Everton ana safari ndefu akiendelea kusaka kazi mpya. "Katika rekodi yake itaonyesha kwamba aliteuliwa kuwa kocha wa Manchester United, kitu ambacho ni nadra,". Moyes alimaliza katika nafasi ya saba akiwa Manchester United msimu uliopita, na wakati Mscotland huyo anaondoka United aliacha rekodi mbaya zaidi ya mechi za nyumbani tangu mwaka 1978 na pointi chache zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya England. Bado alikuwa ana asilimia nzuri ya ushindi zaidi ya Sir Matt Busby, lakini alipoteza mechi 11 kama kocha wa United, akiruhusu mabao 40 katika mechi 34, kabla ya kufukuzwa siku mbili baada ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa Everton, Aprili 22, mwaka huu katika Ligi Kuu. Ryan Giggs alikaimu nafasi yake kumalizia msimu kabla ya Mholanzi, Louis Van Gaal kuajiriwa msimu huu. Hata hivyo, bado United haijawa na mwenendo mzuri chini ya kocha mpya, licha ya kumwaha fedha nyingi kusajili nyota kadhaa.

0 comments:

Post a Comment