Wednesday, October 22, 2014
|
CHELSEA imefanya kile kinachoitwa ‘mauaji’
baada ya kuifumua Maribor mabao 6-0
katika mchezo wa Kundi G Ligi ya
Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa
Stamford Bridge, London.
Loic Remy aliifungia bao la kwanza timu ya
Jose Moutinho dakika ya 13 kabla ya
kuumia na kumpisha mkongwe Didier Drogba
aliyekwenda kufunga bao la pili kwa penalti
dakika ya 23.
John Terry akafunga bao la tatu kwa shuti
la mbali dakika ya 30 kabla ya krosi ya Eden
Hazard kutumbukizwa nyavuni na beki wa
Maribor Mitja Viler katika harakati za
kuokoa.
Maribor ilipoteza nafasi ya kupata bao la
kufutia machozi, baada ya mkwaju wa
penalti wa Agim Ibraimi kugonga mwamba
na Hazard akafunga bao la tano kwa penalti
na la sita dakika ya 90.
Katika mchezo mwingine wa Kundi G,
Schalke O4 imeifunga 4-3 na Sporting. |
0 comments:
Post a Comment