Monday, September 01, 2014

IKIWA YAMEBAKI MASAA DIRISHA LA USAJIL KUFUNGWA HIZI NI TETESI ZA USAJILI ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA

Arsenal huenda wanakaribia kumsajili Alessio Cerci, 27, kutoka Torino baada ya mchezaji huyo kuachwa katika kikosi kitakachocheza na Inter Milan Jumapili (Daily Star), Arsenal wanakaribia kumsajili kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin, 24, baada ya kukubali kutoa pauni milioni 24 (CaughtOffSide), Manchester United huenda ikashuhudia wachezaji 11, ama wakiondoka, au kuingia Old Trafford kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu (Daily Star), Real Madrid wapo tayari kuwajaribu tena Manchester City kumtaka Alvaro Negredo, 29 (Mirror), Louis van Gaal alimshawishi Robin van Persie kuahirisha upasuaji wa goti kabla ya Kombe la Dunia, lakini sasa huenda akamkosa mshambuliaji huyo wakati fulani msimu huu (Daily Mirror), Juventus wanaamini kukamilisha uhamisho wa Radamel Falcao. Real sasa wanamtaka Javier Hernandez (Gazetta dello Sport), Arsenal wameacha kumfuatilia Loic Remy wa QPR ambaye anajiandaa kujiunga na Chelsea (BBC).

0 comments:

Post a Comment