Tuesday, October 21, 2014

ANGEL DIMARIA AZUA HOFU KUBWA MANCHESTER UNITED

WINGA Angel di Maria alionekana hayuko vizuri akiwa ameketi kwenye benchi la Manchester United usiku wa jana, huku amekandamizia barafu katika nyonga yake kwenye mchezo huo ulioisha kwa sare ya 2-2 na West Bromwich Albion. Muargentina huyo, aliyesajiliwa kwa dau la rekodi United, alikuwa kivutio Uwanja wa The Hawthorns, lakini kulikuwa kuna wasiwasi juu ya kiungo huyo baada ya kutolewa dakika ya 76. Di Maria amekuwa katika kiwango babu kubwa tangu asajiliwe kwa Pauni Milioni 60 kutoka Real Madrid msimu huu na ameendeleza mwanzo wake mzuri usiku wa jana. Alimsetia Marouane Fellaini kufunga bao la kusawazisha kipindi cha pili, kabla ya kumpisha Ashley Young. Amecheza mechi tano hadi sasa Manchester United na amefunga mabao matatu na kusaidia manne.
Di Maria (aliyekaa chini kulia) akiwa amekandamizia barafu kwenye nyonga yake huku Chris Smalling, Ander Herrera na Ryan Giggs wakimuangalia kwenye benchi jana Uwanja wa The Hawthorns

0 comments:

Post a Comment