Tuesday, September 02, 2014

BAADA YA FALCAO HUYU NDO MCHEZAJI MWINGINE ALIYEKAMILISHA USAJILI WAKE MAN UNITED HAPO JANA

KLABU ya Manchester United imemsajili Daley Blind kwa dau la Pauni Milioni 14 katika jitihada za kocha Louis van Gaal kutatua tatizo la safu ya ulinzi Old Trafford. Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uholanzi mara moja amwatumia salamu mashabiki wa timu hiyo kwa kusema; "Ni heshima kusajiliwa na United. Siwezi kusubiri kufanya kazi na klabu dunia,". Inamaanisha Van Gaal ametumia zaidi ya Pauni Milioni 150 kwa usajili wa kipindi hiki - ambacho ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutumiwa na klabu hiyo kwa miaka mitano iliyopita, huku Radamel Falcao naye akiwa mbioni kukamilisha uhamisho wa mkopo

 BONYA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI PUNDE ZITUFIKIAPO 

0 comments:

Post a Comment