Thursday, October 23, 2014
 |
Kwa sasa tuna miss Tanzania mpya aitwaye
Sitti Mtemvu ambaye kwa maelezo yake
anasema ana miaka 23 huku ushahidi mwingine
ukionyesha kua ana zaidi ya miaka 23. Baada ya
kuchaguliwa tu watu wengi walianza kulalamika
kua Sitti alipewa ushindi huo kwa kupendelewa
jambo ambalo hata mimi naona ni la kweli.
Jana mwandaaji wa mashindano hayo Lundenga
aliitsha mkutano na waandishi wa habari na
kutoa ufafanuzi ya kua mshindi huyo hana miaka
18 kama watu wanavyosema na kuweka
vithibitisho ya kua Sitti ana miaka 23 kama cheti
chake kinavyosema. Uongo ambao nauona hapa
tumedanganywa ni kuhusu hicho cheti ambacho
mimi nakiona ni feki ni kua kilitengenezwa mda
mfupi kabla ya kuanza mashindano huku cheti
cha kwanza ambacho ndicho kilichotumika
kutengeneza hadi Passport yake inayoonyesha
kua kazaliwa mwaka 1989 kikiwa kimepotea.
Na alipoulizwa kilivyopotea ulienda kutoa taarifa
kituo gani cha polisi aligoma kutaja. Kwa nini
agome na wakati ilikua rahisi tu kutaja jina la
kituo cha polisi kama kweli alienda kutoa
taarifa?? ni maswali mengi aliulizwa lakini
akagoma hii ni dalili kua miss Tanzania wetu ni
magumashi matupu. Haiwezekani mtu
tunayemwamini akaiwakilishe Tanzania katika
mashindano ya dunia ashindwe kujibu maswali
muhimu kabisa kuhusu umri wake.
Hii ni aibu kubwa kwa Lundenga na nahisi
atakua amejifunza kitu na hatarudia kupitisha
mamiss kimagumashi hivi, na naamini hata yeye
roho inamuuma kwa alichokifanya.
Unaweza tazama video ya mahojiano hayo hapa
chini : |
0 comments:
Post a Comment