Wednesday, November 19, 2014
|
Baada ya Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi,
Treni, Kivuko cha Mv. Dar es Salaam, leo kuna
taarifa nyingine nzuri ambayo inahusu jitihada
za Serikali kumaliza tatizo sugu la foleni
katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha TBC1 , Waziri
wa Ujenzi Dk. John Magufuli amesema; “…
Tuliwatuma wataalamu hawa, na bahati nzuri
Chief Executive wa TANROADs hivi karibuni na
wataalamu wenzake walienda South Korea..
Serikali ya South Korea imekubali kutufadhili
kujenga flyover nyingine pale.. na barabara
yenyewe itakuwa na urefu wa karibu kilomita
7.2 na barabara itaanzia Coco Beach, itapita
baharini itakuja kutokea Agakhan Hospital na
kuja ku-join na barabara nyingine hii ya Alli
Hassan Mwinyi… ”
“.. Tumepanua maeneo pengine kote.. tuna
mradi wa BRT ambao una-involve kilometa
zaidi ya ishirini na moja na karibu sasa hivi
unaisha chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia,
lakini tunapofika pale Salenda pamekuwa na
tatizo kubwa na kwa sasa hivi katika traffic
count ya magari yanayopita pale kwa siku
yamezidi zaidi ya magari hamsini na moja
elfu kwa hiyo hawawezi wakaya-accommodate
magari yote yanayoweza kupita sehemu
hiyo… ”– Dk. Magufuli |
0 comments:
Post a Comment