KOCHA David Moyes yumo kwenye orodha
fupi ya mwisho ya makocha wanaotakiwa
na Inter Milan ya Italia inayotaka kumtimua
kocha wake wa sasa, Walter Mazzarri.
Kocha huyo wa zamani wa Manchester
United na Everton anapewa nafasi kubwa ya
kurithi mikoba ya Mazzarri, ambaye timu
yake inacheza na Cesena leo akiwa katika
shinikizo baada ya mwanzo mbaya
unaoifanya Inter iwe katika nafasi ya tisa
kwenye msiamo wa ligi hivi sasa.
Moyes mwenyewe amekua akiamini akipata
nafasi ya kufundisha klabu nje ya Uingereza
itakuwa ni fursa nzuri kwake kurejesha
heshima yake- hivyo akifanikiwa mpango
huo atakuwa ametimiza ndoto zake kwa
sasa. |
0 comments:
Post a Comment