Wednesday, October 29, 2014

RONALDO APIGA HAT TRICK YA TUZO LA LIGA, MESSI AAMBULIA PATUPU

Cristiano Ronaldo amekomba zawadi tatu 'hat trick' za tuzo ya wachezaji bora Ligi ya Hispania maarufu kama La Liga. Huku mpinzani wake Lionel Messi akiambulia patupu, tuzo tatu alizobeba Ronaldo ni pamoja na Mchezaji Bora, Mfungaji Bora na Mshambuliaji Bora wa La Liga. Ilikuwa furaha kubwa kwa Ronaldo ambaye aliongozana na mpenzi wake Iryna Shayk, mwanamitindo kutoka Urusi. Pamoja na Ronaldo kubeba tuzo hizo, timu yake ya Real Madrid imetawala zaidi kuliko klabu nyingine ya Hispania. Zawadi ya kiungo bora imekwenda kwa Luka Modric huku Sergio Ramos akichukua tuzo ya beki bora. Kipa mpya wa Real Madrid, Keylor Navas amechukua tuzo ya mlinda mlango bora. Kabla ya kutua Madrid, Navas alikuwa akikipiga Levante. Barcelona pia imefanikiwa kupata tuzo tatu, Andrés Iniesta alitangazwa kuwa kiungo bora mshambuliaji, huku Ivan Rakitic na Rafinha wakitwaa tuzo mbili za Fair Play and Breakthrough. Kutokana na mafanikio makubwa msimu uliopita, Kocha wa Atlético, Diego Simeone alibeba tuzo ya Kocha Bora. Mshambuliaji nyota wa Sevilla, Carlos Bacca akachukua tuzo mchezaji Bora kutoka Amerika Kusini na Yacine Brahimi wa Granada akawa Mchezaji Bora kutoka Afrika.

0 comments:

Post a Comment