Wakati Nick Cannon ametoka kufunika Tattoo
yenye jina la mke wake Mariah Carey ambaye
wametengana kwa kuongeza mchoro mwingine
juu yake hivi karibuni, msanii wa Bongo Fleva Nuh
Mziwanda ameongeza Tattoo ya pili ya mpenzi
wake Shilole kwenye mkono wake.
Nuh amesema mchoro huo wa pili kwenye mwili
wake una sura ya Shishi baada ya ile ya kwanza
ambayo ni jina la ‘Shishi Bybee’.
“Tattoo ya pili ni sura aisee sura ya mpenzi
wangu Shishi,” ameiambia 255 ya XXL ya Clouds
Fm. “nimetaka kuweka maana ya jina pamoja na
sura yake unajua jina tu lilikuwepo kukamilisha
upendo ule na thamani na shkurani kwake so
nilichora ile Shishi Bybee ya maneno halafu
baadae nimechora sura yake, nimechora mkono
ule ule, so hii shishi Bybee iko nyuma ya mkono
wangu halafu hii sura yake iko mbele.” |
0 comments:
Post a Comment