Saturday, November 01, 2014

DE GEA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MAN UNITED KWA ASILIMIA 70

MASHABIKI wa Manchester United
wamemchagua kipa David de Gea kuwa
Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa klabu
hiyo, baada ya Mspanyola huyo kupata
asilimia 70 ya jura zilizopigwa kwenye
mtandao.
Licha ya kushindwa kuzuia nyavu zake
kutikiswa katika mchezo wowote mwezi huo,
De Gea alikuwa katika kiwango kizuri wakati
United ikiifunga Everton kabla ya kutoa sare
na West Brom ugenini na baadaye na vinara
wa Ligi Kuu England, Chelsea nyumbani.
Mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka
23 alipangua mkwaju wa penalti Leighton
Baines na kuokoa michomo miwili ya hatari
ya The Toffees dakika za mwishoni,
kuiwezesha timu ya Old Trafford kupata
pointi moja, kabla ya kuokoa mchomo
mwingine wa Eden Hazard wakati Mbelgiji
hjuyo alipopata nafasi nzuri ya kufunga timu
hiyo ikitoka 1-1 na kikosi cha Jose
Mourinho.

0 comments:

Post a Comment