Thursday, October 09, 2014

ANGALIA MOTO ULIVYOTEKETEZA NYUMBA YA VICTOR COSTA, MKEWE ALIA UMASIKINI

Mke wa beki wa zamani wa Simba, Victor Costa Nampoka amelia na kusema umasikini unaendelea kuwamaliza hasa baada ya nyumba yao kuteketea na moto. Jasmin Badar ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba, amesema anaona anatumbukia tena kwenye vita ya kujikomboa baada ya nyumba hiyo eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam kuteketea.
“Umasikini huu jamani, kama unavyoiona, nyumba yote imeteketea, kweli inatia uchungu sana,” alisema Jasmini ambaye alishinda kwa kishindo kwenye uchaguzi wa Simba.
Masaibu hayo yameikuta familia ya Costa wakati akiwa mkoani Shinyanga na timu yake ya sasa ya Mwadui FC. Costa amesema chanzo cha moto huo ni kibatari kilichowashwa baada ya umeme kukatika na baadaye moto wa kibatari kushika kwenye pazia na kwa kuwa watu hawakuwepo ndani, moto ule ulisambaa. Costa aliongeza kuwa moto huo umeteketeza kila kitu kilichokuwa ndani ya nyumba na hakuna kilichosalimika.

CRD SALEHALLY.COM

MBEYA CITY YAZIPIGA BAO 'LAINII' SIMBA NA YANGA SC...CHEKI KITU HIKI!

Mbeya City wamezidi kupiga hatua kwenye vitu kadhaa ambavyo vingeweza kufanywa na klabu kongwe za Yanga na Simba. Sasa wamekuwa wakivifanya wao kama vile utaratibu wa kuuza jezi ambao unaiwezesha klabu kuingiza fedha nyingi. Safari hii wametengeneza bahasha ambazo zina nembo ya klabu na mdhamini wao mkuu. Huenda hii inaweza isiwe ni biashara au faida, lakini ni sehemu ya kuonyesha kiasi gani wanaidhamini taasisi yao. Si taasisi za kiserikali au binafsi nje ya mpira ndiyo zinaweza kufanya hivyo pekee. Hata Mbeya City.

UNAAMBIWA ILI NIPIGO LINGINE KUBWA SANA WALIOPATA ARSENAL MSIMU HUU

KLABU ya Arsenal imepata pigo baada ya kiungo wake, Mesut Ozil kuumia na anatakiwa nje kwa kipidi chote kilichobaki kumaliza mwaka 2014. Kiungo huyo alikwenda kufanyiwa vipimo vya MRI katika goti lake na Chama cha Soka Ujerumani kimethibitisha atakuwa nje kwa miezi mitatu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hakufanya mazoezi na timu yake ya taifa ya Ujerumani mjini Frankfurt baada ya kuanza kulalamika juu ya hali yake. Mesut Ozil atakuwa nje kwa kipindi chote kilichobaki mwaka 2014 baada ya Chama cha Soka Ujerumani kuthibitisha kuumia kwake goti Ozil hajaonyesha dalili kubwa za maumivu katika miezi ya karibuni na amecheza mechi tisa msimu huu, akifunga bao moja. Taarifa ya Arsenal imesema: "Ozil alilalamika kuwa na maumivu ya goti la kushoto baada ya mechi na klabu ikakishauri Chama cha Soka Ujerumani kumfanyia uchunguzi atakapojiunga na kikosi cha timu ya taifa. "Klabu itamfanyia uchunguzi wa kina na ni mapema sana kusema Ozil atakuwa nje kwa muda mrefu kiasi gani". Ozil, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 42.5 mwaka jana, amekuwa akikandiwa kwa kucheza chini ya kiwango akiwa na jezi ya Arsenal. Habari za kuumia kwake zinazokuja mwezi wa pili ndani ya msimu mpya, ni pigo kwa kochaa Arsene Wenger ambaye sasa idadi ya majeruhi inaongezeka katika timu yake, Ozil akkungana na Aaron Ramsey, Mathieu Debuchy, Olivier Giroud pamoja na Mikel Arteta.

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

HALIMA MDEE NA WENZAKE WAPATA DHAMANA

Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee. Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wenzake 8 leo wamepata dhamana katika Mahakama ya Kisutu, Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014. Siku ya jana washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Kaluyenda na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu, Kangola aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi, Penina Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari. Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf iliyowataka watawanyike. Shtaka la pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika kinyume na sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

Wednesday, October 08, 2014

Vitu 8 vya kufanya kila asubuhi ili uweze kufikia Mafanikio kimaisha

Haya Msomaji wa mdadisiblog sikiliza nikuambie ni nini hasa mambo ya kufanya kila asubuhi ili uweze kupata mafanikio zaidi kimaisha. Binafsi hivi karibuni nimesoma makala katika moja ya magazeti nnayoyapenda na yalionyesha orodha za watu waliofanikiwa na wanachokifanya mara kwa mara. Kisha, nikaanza kutafiti zaidi kidogo na kupata mambo kadhaa muhimu ambayo yaliendana kwa watu hao. Hapa kwa haraka nitakushirikisha vitu  8 vya kufanya kila asubuhi:-

1. Amka Mapema

Jambo la kwanza la kufanya ukitaka kufanikiwa ni kuhakikisha unaamka mapema sana asubuhi. Watu waliofanikiwa huamka  kuanzia saa 10:30 hadi 11:30 asubuhi. Hapa nawalenga wale wanaoamka saa mbili asubuhi hadi saa tatu.Ukiamka mapema utaweza kupata kifungua kinywa mapema saa 01:30 asubuhi na kuwa na siku ndefu. Watu wengi wenye mafanikio huamka mapema.

2. Fanya Mazoezi

Mbali na kuamka mapema kufanya mazoezi ni jambo la muhimu pia na sio tu kufanya mazoezi bali kufanya mazoezi mapema asubuhi. Watu waliofanikiwa hufanya mazoezi asubuhi si kwa kupunguza miili yao tu bali kujipa afya ya akili katika kupambana na mambo aliyopanga kufanya katika siku hiyo.

3. Pata Kifungua kinywa (Breakfast)

Wote tunajua breakfast ni kitu muhimu ila je, Unajua kama watu waliofanikiwa huhakikisha wanapata breakfast kama jambo la msingi sana? Siongelei chai na maandazi nnaongelea chai nzito yenye vitu kama matunda au juice pamoja na maziwa/mayai ili kupata protini. Hii ni zawadi kubwa unayoweza kuupatia ubongo wako ili kuweza kuurahisishia kazi.

Hakikisha unapata breakfast masaa machache baada ya kuamka na kama jana yake usiku ulichelewa kula basi haishauriwi upate breakfast mapema.

4. Jipatie muda wa kuwa katika ukimywa

Sababu kubwa ya kuamka mapema ni kujipatia wasaa wa kuwa katika hali ya ukimywa. Unapoamka na kufanya mazoezi ni kujipa muda tosha na kuupa ubongo wako fursa ya kuwaza kuhusu mambo yako tu wala si kelele za watoto ndani ya nyumba au watu wengine.

Fikiria kuhusu majukumu yako ya siku hiyo na vitu unavyohitaji kufanya na kama itakusaidia unaweza kuandika chini. Kila siku zinapoenda utajikuta unazoea wasaa huu wa kuwa kimya hata kujiongezea muda wa jambo hili.

5.  Jipange

Kitu kingine ambacho kinafanana kwa watu waliofanikiwa ni pale wanapojipanga jinsi watavyoitumia siku yao. Kila asubuhi panga jinsi ya kutumia siku yako anza na kupanga vifaa vyako vya kazi, panga muda utaotumia kufanya kila jambo ikiwemo kula chakula cha mchana. Tandika kitanda chako na acha nyumba yako katika hali ya usafi. Kila mara unapoacha kufanya baadhi ya mambo haya taarifa za kukuletea mawazo (stress) hutumwa katika ubongo wako.
Ukijipanga utafurahia siku yako na kufanya mambo mengi zaidi kwa umakini unaohitajika.

6.  Achana na mambo ya siku iliyopita.

Kitu muhimu kila asubuhi ni kutoamka ukijilaumu kwa maamuzi na vitu ulivyovikosa jana. Kama uligombana na mtu jana, au mwajiri wako alisema kitu cha kukuudhi, au haukupata ile nyongeza ya mshahara uliyotarajia. Acha mambo ya aina hii. Kama ulimkosea mtu, hakikisha unamuomba msamaha. Achana na yaliyopita na weka akili yako kwa mambo ya leo.

Kila mtu aliyefanikiwa anaianza siku yake kwa kuwa na tabia mpya, mipango mipya na nguvu mpya na sio kujilaumu. Tabia hii itakupa uwezo wa kufanikiwa kwa siku husika.

7. Kuwa na Imani

Anza siku kwa kujitamkia maneno ya kujikumbusha kuwa una uwezo wa kuimaliza siku hii kwa kuchukua fursa zote zitakazo jitokeza, kufanya maamuzi sahihi na kuwa mvumilivu. Fanya Sara kulingana na Imani yako kwa Mungu.

8. Soma

Ikiwa ni habari kwenye gazeti, soma barua pepe, au soma kurasa chache za kitabu unachokipenda. Kusoma asubuhi ni kuzuri kwa mazoezi ya akili yako.

Nikki Mbishi awashirikisha Jaydee, Songa na One kwenye ‘Kupanda na Kushuka’

Rapper wa Tamaduni Muzik, Nikki Mbishi anatarajia kuachia wimbo mpya ‘Kupanda na Kushuka’ aliowashirikisha Lady Jaydee, Songa na One the Incredible. Nikki amesema ameamua kuwashirikisha wasanii hao ili kupata kitu tofauti kama muziki unavyohitaji. “Unajua muziki sometimes unahitaji vitu fulani fulani ili uwe mzuri zaidi na hii ni kawaida ya muziki ulivyo. Kwahiyo tukaona tukifanya kitu kwa pamoja kitakuwa safi tukaingia studio za Man Walter tukafanya wimbo ‘Kupanda na Kushuka’, ni wimbo ambao unaelezea maisha ya kawaida kupanda na kushuka kwa maisha, leo umepata kesho umelala njaa lakini ni maisha. Wimbo utatoka hivi karibuni pamoja na video,” alisema Mbishi.

LE MAJANGAZ JINSI KAJALA NA WEMA SEPETU WALIVYOTOANA JASHO KITUO CHA POLISI KIJITONYAMA LIVE!!

null
Mwigizaji Kajala Masanja Kufuatia matusi ya mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu kwenda kwa mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, mastaa hao wamejikuta wakitoana jasho kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama almaarufu Mabatini jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.Duru za ‘kiubuyu’ zilidai kwamba Kajala, baada ya kuchoshwa na matusi hayo ambayo yalianzia kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Wema, alijikuta akiishiwa na uzalendo kisha kuingia mzigoni ili kukomesha matusi hayo kwenye mitandao ya kijamii. Ilidaiwa kwamba, Kajala akiwa na timu yake (Team Kajala) alifanikiwa kumtia mbaroni dada mmoja aliyetajwa kwa jina la Matrida akidaiwa kwamba ni mfuasi wa Wema (Team Wema). Ilisemekana kwamba Matrida anayetumia jina la ‘Mat Kiboko Yao’ kwenye ukurasa wake wa Instagram ndiye ambaye amekuwa akiongoza jahazi la kumtusi Kay. Ilizidi kunyunyizwa kwamba sakata hilo la kuanikwa Instagram lilianza siku mbili baada ya ile pati ya kuzaliwa ya Wema ambapo Mat Kiboko Yao alimtukana Kajala matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini) kupitia ukurasa wake kwenye mtandao huo. Ilidaiwa kwamba Kajala alipoona amechoka kutukanwa, alitafuta wataalam ili kujua namna ya kumkamata na alipomjua ndipo akakimbilia Kituo cha Polisi cha Mabatini kwenda kutoa taarifa. RB
Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu.Gazeti hili lilifanikiwa kunasa namba ya jalada la kesi hiyo iliyosomekaKJN/RB/8854/2014-MATUMIZI YA MATUSI MTANDAONI. Ilisemekana polisi walitumia mbinu zao na kufanikiwa kumkamata Mat Kiboko Yao na kumweka nyuma ya nondo za mahabusu kituoni hapo ndipo sarakasi za pande mbili zikaanza. KWANZA Mara tu baada ya Mat Kiboko Yao kukamatwa mishale ya saa 2:00 usiku, taarifa zilisambaa kama moto wa kifuu ndipo Team Wema ikaingia mzigoni kutaka kumtoa mwanadada huyo lakini wakagonga mwamba. WEMA, PETIT MAN WATINGA MABATINI Ilidaiwa kwamba, baada ya Mat Kiboko Yao kutiwa mbaroni, Wema na jeshi lake akiwemo Petit Man walitinga Mabatini kwa ajili ya kumtoa mwanadada huyo lakini aligonga mwamba na kumuacha akilala kituoni hapo. “Yaani ulikuwa ni usiku wa kutoana jasho na kupimana ubavu kwamba nani ni nani. Ilikuwa akitoka Kajala kuhakikisha kwamba mtuhumiwa wake aachiwi, Wema naye anatinga kituoni kwa mbwembwe kutaka Mat Kiboko Yao aachiwe kwa gharama yoyote. “Hapo ndiyo ngoma ilikuwa nzito, kila mmoja alikuwa anamuonyesha mwenzake kuwa ni zaidi na ni maji marefu hadi kulipokucha muvi likaendelea,” alisema shuhuda aliyefuatilia sakata hilo kinagaubaga.
Mama wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu.WAANDISHI WAPEWA UBUYU, WATINGA MABATINI Kulipokucha, waandishi wetu walipewa ubuyu huo ndipo wakatinga Mabatini kisha wakatega ‘rada’ zao na kuweka doria. Wanahabari wetu, wakiwa kituoni hapo walimshuhudia Kajala akilinda kituoni hapo asitokee mtu yeyote akamtoa Mat Kiboko Yao. Hata hivyo, alipoulizwa Kay kulikoni kuwa eneo hilo alisema alikuwa ameitwa kwa ajili ya kusuluhishwa badala ya kupoteza muda kwa jambo kama hilo. KAJALA NA KUNDI LAKE Awali Kay alionekana akiingia kituoni hapo na kundi lake la watu watatu akiwemo mwanaume mmoja ambapo yeye aliingia mpaka kwenye chumba cha mkuu wa kituo. Kajala akiwa kwa mkuu wa kituo, haikujulikana kilichokuwa kikiendelea ndani kwani kulikuwa na kikao cha muda mrefu ambapo ghafla Kajala na mtuhumiwa wake waliyeyuka. WEMA AINGIA MITINI Wakati hayo yakiendelea kituoni hapo, si Wema wala jeshi lake waliofika kwa ajili ya kumtetea Mat Kiboko Yao ambaye ndiye kiongozi wa Timu Wema kwa kutukana. Hata hivyo, baadaye alionekana mmoja wa marafiki wa karibu ambaye ni ndugu wa Mat Kiboko Yao aliyekuwa akihaha kumtoa mwenzake. TUJIKUMBUSHE Hivi karibuni Mama Wema alimtolea uvivu Kajala na kumtusi ndipo akafufua upya kile kidonda cha Sh. milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kay asiende jela na kinachoonekana, bado fedha hizo ni tatizo kubwa.

Picha 12 za gari alilonunua msanii Shetta na mambo matatu aliyoyasema kwa wanaotaka kufanikiwa.

Lengo lilikua ni kukutana na Shetta kwa ajili ya kufanya interview kuhusu Tour yake ya Kerewa aliyotembea nayo kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania na nje ya Tanzania kwenye maeneo mbalimbali kama Mombasa Kenya, so ilikua iwe hivyo lakini kwa bahati nzuri akawa amekuja na hili gari nikalazimika kumuomba tupate za ndani kidogo itupe nguvu ya kuzichanga. Shetta ni staa wa single kama ‘ Nidanganye ‘ na ‘ kerewa ‘ ambazo zote alimshirikisha staa mwingine wa bongofleva Diamond Platnumz ambapo kwenye hii post ya leo on millardayo.com ameziachia exclusive kadhaa za hatua zake za kimaisha. Anasema kwa yeyote ambae anahitaji mafanikio kwenye hii dunia ni lazima awe na Uvumilivu, uelewa wa kwamba sio kila siku utapata, matumizi mazuri ya kinachopatikana hata kama ni kidogo, kujifunza kuweka akiba, kuishi na watu vizuri bila kujali unamjua au haumjui pamoja na bidii kwenye kila nafasi ndogo unayoipata, hayo ni baadhi ya mambo ambayo anasema yanaweza kukuweka karibu na mafaniko au kukupa mafaniko.
Gari hili ambalo ni aina ya Harrier Lexus ni la tatu toka Shetta aanze kumiliki magari ambapo gharama yake ni shilingi milioni 45 kwenye sehemu mbalimbali za kuuzia magari Tanzania……
Mara nyingi huwa wengi wakiona picha kama hizi wanauliza una nyumba? goodnews ni kwamba kwa sasa Shetta anamalizia kujenga nyumba yake Madale Dar es salaam hivyo ameahidi kushare pichaz na sisi sio kuringishia bali kutoa hamasa kwa vijana wengine wanaomchukulia kama mfano kujifunza na kupata nguvu ya kupambana kuzichanga kutoka kwenye hali ya chini kama yeye alieanzia muziki akiwa shule ya sekondari Jitegemee.

CRD MILARD AYO

SESSEGNON WA WEST BROM AJA NA BENIN KUIVAA STARS, WAMO NA WAKALI NA LIGUE 1 UFARANSA

Didier Nicolle ametaja kikosi cha wachezaji 18 kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mfaransa huyo ameita wachezaji 13 wanaocheza nje ya nchi hiyo akiwemo kiungo Stephane Sessegnon wa West Bromwich Albion ya Uingereza kwa ajili ya mechi hiyo ya Kalenda ya FIFA itakayoanza saa 11 jioni. Wachezaji wengine katika kikosi hicho ni Didier Sossa (AS Dragons FC de I’Oueme, Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (FC Liefering, Austria), Sessi D’almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed Aoudo (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (US Krake, Benin). Steve Mounie (HSC Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (SM Caen, Ufaransa), Michael Pote (Omonia Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco). Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Benin), Nafiou Badarou (ASO Chlef, Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore (US Krake, Benin) na Seibou Mama (US Krake, Benin). Msafara wa timu hiyo utaanza kuingia nchini kesho (Oktoba 9 mwaka huu) kwa nyakati tofauti, na utakuwa umekamilika (Oktoba 10 mwaka huu). Timu hiyo itafikia hoteli ya JB Belmont.

Uhuru Kenyatta aelekea ICC kama raia ndani ya "t-shirt na jeans" juu kapelo ! Cheki picha hapa

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewasili jijini The Hague, Uholanzi katika Mahakama Maalum ya Kimataifa inayohusika na visa vya uhalifu kwa viongozi wa nchi zilizoridhia mkataba huo, ICC, kwa ajili ya kikao maalum kuhusu kesi inayomkabili. Siku ya Jumatatu, Rais Kenyatta alikabidhi madaraka yake kwa muda kwa Naibu Rais, William Ruto na kusisitiza kuwa anaondoka nchini humo kama raia. Akiwahutubia Wabunge mjini Nairobi, Kenyatta aliwaambia kuwa yuko tayari kuhudhuria kikao maalum alichotakiwa kuhudhuria mjini Hague bila wasiwasi wowote. Kenyatta alitakiwa na majaji wa mahakama hiyo kufika ICC tarehe 8 mwezi huu kufafanua madai a upande wa mashitaka uliodai kuwa serikali ya Kenya imekataa kushirikiana na mahakama hiyo hasa upande wa mashitaka kwa kukataa kuipatia ushahidi unaohitajika katika kesi inayomkabili kama vile rekodi zake za mawasiliano ya simu na taarifa zake za kifedha. Mbali na hilo, Ofisi ya kiongozi wa Mashtaka Jumanne wiki hii imewaomba majaji wa Mahakama hiyo kuamua kuwa Kenya haishirikiani na Ofisi hiyo kuhusu kesi inayomkabili rais Kenyatta. Kenyatta anakabiliwa na kesi inayomtuhumu kupanga, kuchochea na kufadhili machafuko na ghasia baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007. Rais Kenyatta anasema anajiamini na kwamba anajua hana hatia katika tuhuma zinazomkabili. Alisema Kenya ni nchi huru na kwamba haitawahi kuwa chini ya mamlaka nyingine yoyote. Vyombo kadhaa vya habari na mitandao ya kijamii imeripoti kuwa takriban wabunge mia moja walikuwa wanajiandaa kuambatana na Kenyatta kuelekea The Hague katika ishara yao ya kumuunga mkono.

MENINAH AMWANIKA DIAMOND TENA!! AFUNGUKA MENGI KUHUSU MAHUSIANO YAO,AELEZA JINSI WEMA ALIVYO MPA PRESHA

null
Menina Atik a.k.a Menina la diva na Nguli wa Bongo Fleva nchini Nasib Abdul 'Diamond' hatimaye ukweli umepatika baaada ya kuzinasa meseji za meninah alizofunguka kususu mahusiano yake na Diamond. Meseji hizo zimenaswa kutoka kwenye simu ya Meninah ambaye alikuwa akichati naye kuhusu mwenendo mzima wa Mahusiano yake na Diamond kupitia "Chating" hizo Meninah amekiri kwamba Diamond alimtaka kimapenzi na alifikia hatua ya kujitambulisha nyumbani kwao kwa nia ya kumuoa lakini alimtolea njekwa sababu tayari alikuwa na mchumba mwingine na alishavishwa pete. Aidha,Menina aliendelea kubainisha kwamba diamond alianza kulifukuzi penzi lake toka 'Long time' toka alivyokuwa na mpenzi wake Nasri,Diamond aliendelea kupiga Nyayo Nyumbani kwao kila siku "Alikuwa akinisumbua toka niko na mpenzi wangu Nasri mpaka nimeachana naye mpaka leo ananitaka"Alifunguka meninah katika moja ya meseji hizo aliendelea kufunguka na kusema kuwa Diamond alionyesha hisia zake kwa kupeleka taarifa kwenye moja ya magazeti ya udaku kwa minajili ya kumlegeza ili akubali kuwa mpenzi wake. "Sasa yeye(Diamond) akadhani kwamba anitoe kwenye magazeti labda mimni nitaogopa then nitajikuta niko nae, mimi diamond simtaki.....akaa...kwanza wa nini!" Hata hivyo meninah aaliitaja sababu nyingine ya kumpiga chini diamond akisema kwanza tayari yuko na wema na mimi Wema nam-respect halafu amevishwa pete na mchumba;angu nimsaliti yanini ninayempenda..... akangeza na utani"Domo lake lile nitalipeleka wapi;he is noteven cute.......we cant match."Habari ndiyo iyo!!!" Credit udakumagazine

ARSENE WENGER AMPA MOURINHO DONGO LINGINE ZITO KUHUSIANA NA DIEGO COSTA

KOCHA Arsene Wenger ameshtukia ujanja wa mpinzani wake Jose Mourinho juu ya majeruhi ya straika Diego Costa. Wenger anayeinoa Arsenal, ambayo Jumapili iliyopita ilimenyana na kikosi cha Chelsea alisema anahisi Mourinho anawachezea akili wapinzani wake kuhusu madai ya majeruhi ya misuli ya straika wake huyo. Alipoulizwa kuhusu maoni yake juu ya straika huyo ambaye ni kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu England mpaka sasa msimu huu, Wenger alitabasamu kisha akasema: “Kusema kweli, unapomtazama fowadi huyo uwanjani haonekani kuwa ni majeruhi. “Amekuwa na tatizo la misuli kwa muda mrefu na tuliliona hilo kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, lakini nilipomtazama kwa siku za karibuni, ni ngumu kuamini ni aina gani ya majeruhi ya misuli yanayomsumbua.”

MPASUKO MZITO WAINYEMELEA SOKA YA TANZANIA KISA ‘BIFU’ LA MALINZI NA KIONGOZI HUYU WA SIMBA

Home » Unlabelled » MPASUKO MZITO WAINYEMELEA SOKA YA TANZANIA KISA ‘BIFU’ LA MALINZI NA KASSIM DEWJI Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM MPASUKO mkubwa unainyemelea soka ya Tanzania kufuatia taarifa za kuwapo uhasama mzito baina ya Rais wa Shirikisho la Soka (TFF), Jamal Malinzi na kigogo wa kundi la Friends Of Simba, Kassim Mohamed Dewji. Mpasuko huo unavuka mipaka kutoka kuwa wa wawili hao- hadi kuwa wa taasisi, yaani Simba SC kwa ujumla na TFF, kila mmoja baina yao akitumia chombo chake katika mapambano. Tayari kuna imani ya Simba SC kuchukiwa na TFF ya Malinzi- na kadhalika TFF wanaami wanapigwa vita na Friends Of Simba (F.O.S). Mara baada ya timu ya taifa, Taifa Stars kutolewa na Msumbiji katika mechi ya kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani, kambi ya Malinzi ilivujisha habari kwamba timu hiyo ilihujumiwa na vigogo wa klabu kubwa. Na siku chache baadaye, Malinzi akasema ataunda Kamati ya kuchunguza tuhuma hizo, vigogo mbalimbali wakiitwa kuhojiwa na akaomba watoe ushirikiano, huku akiweka mkwara ambaye hatatoa ushirikiano atachukuliwa hatua. Wakati bado matokeo ya tuhuma hizo hayajatoka- Simba SC nao wanadai wana ushahidi wa kutosha, Malinzi amekuwa ‘akitia mkono’ kwenye mechi zao za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Simba SC imecheza mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu bila kushinda, ikitoa sare zote, 2-2 na Coastal Union na 1-1 mara mbili mfululizo na Polisi Moro na Stand United, tena mechi zote ikicheza Uwanja wa nyumbani, Taifa, Dar es Salaam. Baada ya sare ya Jumamosi na Stand, Friends Of Simba wakaibua tuhuma kwamba Msaidizi wa Malinzi, Juma Matandika alikuwa na marefa wa mchezo huo siku moja kabla ya mechi. Na tuhuma hizi zinakuja wakati ambao kuna mgogoro mzito baina ya Bodi ya Ligi na Kamati ya Utendaji ya TFF juu ya makato ya asilimia tano kutoka fungu la fedha la udhamini wa ligi hiyo kuingia kwenye mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Serikali, kupitia Wizara inayohusika na michezo imeupoza mgogoro huo kwa kuiagiza TFF ikutane na Klabu za Ligi Kuu kuwasilisha ombi hilo badala ya kutaka kulazimisha kukata asilimia tano, tu kwa mawasiliano yake na uongozi wa Bodi ya Ligi.
Kassim Dewji maarufu kwa jina la utani KD, kwa muda mrefu amekuwa na tenda ya kuwauzia TFF jezi za timu za taifa, lakini tenda hiyo ilikatika baada ya Malinzi kuingia ofisini Oktoba mwaka jana.Inadaiwa kabla ya tenda hiyo kukatika, Malinzi aliwahi kuwa na kikao na Dewji ambacho mwisho wake ni matokeo ya tenda hiyo kufa. Inadaiwa, tangu hapo wawili wamekuwa na uhasama wa chinichini hadi sasa unaelekea kuwawazi.Inadaiwa sababu kubwa ya Malinzi kuonekana anataka kumbeba Michael Wambura katika uchaguzi wa Simba SC ni kwa kuhofia F.O.S. wakiingia madarakani kwenye klabu hiyo atakuwa na wakati mgumu TFF.Na uhusiano wa Malinzi na Friends of Simba ulianza kuingia doa wakati huo wa uchaguzi wa Simba SC- kwani F.O.S. waliona Rais huyo wa TFF anawasaliti baada ya kumsaidia kwa hali na mali wakati wa uchaguzi wa shirikisho.F.O.S. wanadai wao ndio waliombeba Malinzi katika uchaguzi wa TFF baada ya aliyekuwa mpinzaniwake mkubwa, Athumani Nyamlani kuwa anasaidiwa na mahasimu wa Simba SC, Yanga SC.
Jezi za sasa za Taifa Stars baada yaMalinzi kumkatia tenda DewjiMalinzi na Dewji wote hawakupatikana kuzungumzia tuhuma hizo- ingawa BIN ZUBEIRY inaendelea na jitihada za kuwatafuta kwa ajili ya kuelezea hilo.Dewji alipokea simu mara moja wiki iliyopita na kusema yuko kwenye kikao apigiwe baadaye, lakini baada ya hapo akawa hapokei simu. Malinzi alikwepa kuzungumzia hayo wiki iliyopita akidai ana haraka na tangu hapo amekuwa hapokei simu pia.

HABARI MBAYA ZAIDI MASIKIONI KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED.

Manchester United msimu huu imejaribu kujiimarisha katika idara ya ushambuliaji kwa kufanya usajili wa kuvunja rekodi nchini Uingereza wakiwa na nia ya kutaka kurejesha makali yao yaliyopotea msimu uliopita lakini uwepo wa majeruhi takribani tisa ndani ya kikosi cha mashetani wekundu hao kinaifanya klabu hiyo kuweweseka.
Hivi karibuni klabu hiyo imetokea kumuamini mlinzi kinda Paddy McNair aliyekuwa akishirikiana vyema na Muajentina Marcos Rojo katika kuimalisha ulinzi wa katikati wa klabu hiyo lakini katika kile kinachoonekana kama kuandamwa na jinamizi la mkosi wa majeruhi kijana huyu naye amelipotiwa kupata maumivu ya misuli daraja la tatu aliyoyapata siku ya Jumapili wakati timu yake ya Manchester United ilipokipiga dhidi ya Everton na kupata ushindi wa magoli 2:1. Kuumia kwa McNair kunatimiza idadi ya walinzi watano wa wa klabu ya Manchester United wanaokaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi ambapo wengine ni Luke Shaw (kifundo cha mguu), Jonny Evans (kifundo cha mguu), Phil Jones (misuli) na Chris Smalling (nyama za paja).
Wachezaji Ander Herrera (mbavu), Jesse Lingard (kifundo cha mguu), Michael Carrick (mguu) na Ashley Young (nyonga) nao wanaungana na walinzi hao watano katika orodha ya majeruhi ndani ya United wakati Wayne Rooney anaendelea kutumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo dhidi ya West Ham.
Wakati Manchester United ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya majeruhi, Arsenal wao wanashika nafasi ya pili katika orodha hiyo na kibaya zaidi ni kuwa idadi kubwa ya wachezaji walio majeruhi kwenye kikosi cha Mfaransa Wenger ni wale wa kikosi cha kwanza. Mikel Arteta, Aaron Ramsey, Mathieu Debuchy, Olivier Giroud na Theo Walcott ni miongoni mwa wachezaji majeruhi wa klabu ya Arsenal na wengi wao ni wachezaji wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Ifuatayo ni orodha ta majeruhi katika vilabu mbali mbali vya EPL mpaka hivi leo: ORODHA YA WACHEZAJI MAJERUHI KWA VILABU VYA PREMIER LEAGUE KWA MSIMU WA 2014/2015. Manchester United -9 Arsenal- 7 Burnley -7 Everton -7 Newcastle -7 West Ham -7 Liverpool- 6 Southampton- 5 Chelsea -4 Stoke City- 4 Swansea City- 4 Aston Villa- 3 Hull City -3 Sunderland- 3 West Brom -3 Crystal Palace- 2 Leicester City- 2 Manchester City -2 Queens Park Rangers- 2

SAMAHANI BINTI MDOGO APONZWA NA UZURI WAKE, ACHARANGWA VITU NA MABINTI WENZAKE KISA WIVU!

Binti mdogo wa miaka 15 raia wa Argentina Julia Alvarez amepatwa na majanga yaliyomfanya apoteze muonekano wake mzuri baada ya mabinti wawili wenye wivu kumcharanga uso wake kwa visu kisa uzuri wake uliopitiliza! Julia anasema alikuwa anatembeakurudi nyumbani akitokea mji wa Juan Domingo Peron huko northern Argentinian ndipo wasichana hao wawili mmoja ana miaka 18 na mwingine 16 walipomvaa bila huruma. "Kila mtu anasema wewe ni mzuri sana..huwezi kuonekena mzuri tena tukishamalizana na wewe hapa..na watu watakuita majina mabaya'' Julia alisema haya ni maneno aliyoambiwa kabla ya kucharangwa visu usoni.

 BOFYA HAPA KUCHEK PICHA ZINGNE 

Maneno ya bango hili la Walimu ndiyo yalisababisha Polisi walirukie

Maandamano ya walimu kuingia katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani, juzi yalipata mtafaruku baada ya polisi kuyaingilia na kuchana bango mojawapo lililohoji posho za wajumbe wa Bunge la Katiba. Bango hilo la kitambaa cheupe lilikuwa na maandishi yanayohoji posho ya Sh300,000 (Sh230,000 kama posho ya kujikimu na Sh70,000 ambazo ni posho ya vikao) waliyokuwa wanapata wajumbe wa Bunge la Katiba, yakilinganishwa na kazi kubwa wanayofanya walimu. Ujumbe wenyewe ulisomeka hivi: “Haki iko wapi? Usawa uko wapi? Posho ya Mjumbe Bunge la Katiba Tsh 300,000/= mshahara wa Mwalimu Tsh 370,000/= kwa mwezi. No big results without big salary”. Hata hivyo bango hilo lilichanwa hatua chache kabla ya walimu hao hawajaingia uwanjani humo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), mkoani Kagera Dauda Bilikesi, alisema amesikia habari za bango hilo kuharibiwa lakini akasema asingezungumza kwa kina kuhusu suala hilo kwa kuwa hayo yamepita.

SOMA MANENO MAZITO YA T.I.D MNYAMA

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khalid Mohammed ‘TID Mnyama’ amesema, yeye ni msanii wa kimataifa tangu siku nyingi ingawa amekuwa hapewi sapoti anayostahili kupata. Akizunguza jijini Dar es Salaam, muimbaji huyo ambaye hivi karibuni alirekodi wimbo na msanii wa Afrika Kusini, Tumi, amesema kile wanachokifanya wasanii wapya wanaotaka kwenda kimataifa kwa sasa, yeye alikifanya miaka mingi iliyopita. Unajua kama kufanya muziki kimataifa mimi tayari nilishaenda zamani sana, maana nikikumbuka video zangu nimeshafanya mahojiano na MTV Base, Channel O na pia nimefanya kazi na wasanii kutoka Nigeria na Afrika Kusini

KWA WALE WADADA MAMBURULAA WA MJINI MNAOPENDA KUIGA, IGENI NA HII SASA KAMA MNAWEZA!!

HAYA NDIO MAISHA YA WANACHUO KWA SASA WANAFUNZI WAZIDI KUWA MAMBURULAA

Wanafunzi wakijipiga picha Bafuni Hostel Kwakweli maisha ya chuoni ni experience tosha, kuna kila aina ya mambo mi naamini kama umepitia maisha ya chuo, umeshakaa hostel basi utakuwa umejifunza mengi sana, na hakuna jipya baada ya hapo. Wapo watu wanaokuja chuoni wakiwa wapole na watiifu, lakini wape muda tu kidogo utaona mara tayari ana boyfriend mara tayari nae ameshaanza kwenda club. Mambo ni mengi sana Vyuoni, kama mpenzi wako ameenda chuoni ujue kuna kazi hapo ndugu yangu muombee tu MUNGU amlinde, vishawishi ni vingi na kuepukika ni ngumu sana inahitaji ujasiri mno. YABIDI KUWA MAKINI TU

Tuesday, October 07, 2014

SHILOLE AKUTWA NA DOGODOGO NYINGINE...NUH MZIWANDA HANA CHAKE TENA

Baada ya kutokuwa na maelewano mazuri kati ya nuhu mziwanda na mpeni wake shilole hivi sasa tetesi zimeibuka upya kwamba wawili hao hawako pamoja tena , hii imefatia kuzagaa kwa picha ambayo shilole amepiga akiwa na njemba mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja,