Wednesday, October 08, 2014
null
 |
| Mwigizaji Kajala Masanja
Kufuatia matusi ya mama wa staa wa
sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu,
Miriam Sepetu kwenda kwa mwigizaji
Kajala Masanja ‘Kay’, mastaa hao
wamejikuta wakitoana jasho kwenye Kituo
cha Polisi cha Kijitonyama almaarufu
Mabatini jijini Dar mwishoni mwa wiki
iliyopita.Duru za ‘kiubuyu’ zilidai kwamba
Kajala, baada ya kuchoshwa na matusi
hayo ambayo yalianzia kwenye sherehe ya
kuzaliwa kwa Wema, alijikuta akiishiwa
na uzalendo kisha kuingia mzigoni ili
kukomesha matusi hayo kwenye mitandao
ya kijamii.
Ilidaiwa kwamba, Kajala akiwa na timu
yake (Team Kajala) alifanikiwa kumtia
mbaroni dada mmoja aliyetajwa kwa jina
la Matrida akidaiwa kwamba ni mfuasi wa
Wema (Team Wema).
Ilisemekana kwamba Matrida anayetumia
jina la ‘Mat Kiboko Yao’ kwenye ukurasa
wake wa Instagram ndiye ambaye
amekuwa akiongoza jahazi la kumtusi Kay.
Ilizidi kunyunyizwa kwamba sakata hilo la
kuanikwa Instagram lilianza siku mbili
baada ya ile pati ya kuzaliwa ya Wema
ambapo Mat Kiboko Yao alimtukana Kajala
matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini)
kupitia ukurasa wake kwenye mtandao
huo.
Ilidaiwa kwamba Kajala alipoona
amechoka kutukanwa, alitafuta wataalam
ili kujua namna ya kumkamata na
alipomjua ndipo akakimbilia Kituo cha
Polisi cha Mabatini kwenda kutoa taarifa.
RB |
 |
| Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac
Sepetu.Gazeti hili lilifanikiwa kunasa
namba ya jalada la kesi hiyo
iliyosomekaKJN/RB/8854/2014-MATUMIZI YA
MATUSI MTANDAONI.
Ilisemekana polisi walitumia mbinu zao na
kufanikiwa kumkamata Mat Kiboko Yao na
kumweka nyuma ya nondo za mahabusu
kituoni hapo ndipo sarakasi za pande
mbili zikaanza.
KWANZA
Mara tu baada ya Mat Kiboko Yao
kukamatwa mishale ya saa 2:00 usiku,
taarifa zilisambaa kama moto wa kifuu
ndipo Team Wema ikaingia mzigoni kutaka
kumtoa mwanadada huyo lakini
wakagonga mwamba.
WEMA, PETIT MAN WATINGA MABATINI
Ilidaiwa kwamba, baada ya Mat Kiboko
Yao kutiwa mbaroni, Wema na jeshi lake
akiwemo Petit Man walitinga Mabatini kwa
ajili ya kumtoa mwanadada huyo lakini
aligonga mwamba na kumuacha akilala
kituoni hapo.
“Yaani ulikuwa ni usiku wa kutoana jasho
na kupimana ubavu kwamba nani ni nani.
Ilikuwa akitoka Kajala kuhakikisha
kwamba mtuhumiwa wake aachiwi, Wema
naye anatinga kituoni kwa mbwembwe
kutaka Mat Kiboko Yao aachiwe kwa
gharama yoyote.
“Hapo ndiyo ngoma ilikuwa nzito, kila
mmoja alikuwa anamuonyesha mwenzake
kuwa ni zaidi na ni maji marefu hadi
kulipokucha muvi likaendelea,” alisema
shuhuda aliyefuatilia sakata hilo
kinagaubaga. |
 |
| Mama wa staa wa sinema za Kibongo,
Wema Isaac Sepetu, Miriam
Sepetu.WAANDISHI WAPEWA UBUYU,
WATINGA MABATINI
Kulipokucha, waandishi wetu walipewa
ubuyu huo ndipo wakatinga Mabatini kisha
wakatega ‘rada’ zao na kuweka doria.
Wanahabari wetu, wakiwa kituoni hapo
walimshuhudia Kajala akilinda kituoni
hapo asitokee mtu yeyote akamtoa Mat
Kiboko Yao.
Hata hivyo, alipoulizwa Kay kulikoni kuwa
eneo hilo alisema alikuwa ameitwa kwa
ajili ya kusuluhishwa badala ya kupoteza
muda kwa jambo kama hilo.
KAJALA NA KUNDI LAKE
Awali Kay alionekana akiingia kituoni
hapo na kundi lake la watu watatu
akiwemo mwanaume mmoja ambapo yeye
aliingia mpaka kwenye chumba cha mkuu
wa kituo.
Kajala akiwa kwa mkuu wa kituo,
haikujulikana kilichokuwa kikiendelea
ndani kwani kulikuwa na kikao cha muda
mrefu ambapo ghafla Kajala na
mtuhumiwa wake waliyeyuka.
WEMA AINGIA MITINI
Wakati hayo yakiendelea kituoni hapo, si
Wema wala jeshi lake waliofika kwa ajili
ya kumtetea Mat Kiboko Yao ambaye ndiye
kiongozi wa Timu Wema kwa kutukana.
Hata hivyo, baadaye alionekana mmoja wa
marafiki wa karibu ambaye ni ndugu wa
Mat Kiboko Yao aliyekuwa akihaha kumtoa
mwenzake.
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni Mama Wema alimtolea uvivu
Kajala na kumtusi ndipo akafufua upya
kile kidonda cha Sh. milioni 13 ambazo
Wema alimlipia Kay asiende jela na
kinachoonekana, bado fedha hizo ni tatizo
kubwa. |
0 comments:
Post a Comment