Thursday, October 09, 2014
 |
| KLABU ya Arsenal imepata pigo baada ya
kiungo wake, Mesut Ozil kuumia na
anatakiwa nje kwa kipidi chote kilichobaki
kumaliza mwaka 2014.
Kiungo huyo alikwenda kufanyiwa vipimo
vya MRI katika goti lake na Chama cha
Soka Ujerumani kimethibitisha atakuwa nje
kwa miezi mitatu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25
hakufanya mazoezi na timu yake ya taifa ya
Ujerumani mjini Frankfurt baada ya kuanza
kulalamika juu ya hali yake.
Mesut Ozil atakuwa nje kwa kipindi chote
kilichobaki mwaka 2014 baada ya Chama
cha Soka Ujerumani kuthibitisha kuumia
kwake goti
Ozil hajaonyesha dalili kubwa za maumivu
katika miezi ya karibuni na amecheza mechi
tisa msimu huu, akifunga bao moja.
Taarifa ya Arsenal imesema: "Ozil
alilalamika kuwa na maumivu ya goti la
kushoto baada ya mechi na klabu
ikakishauri Chama cha Soka Ujerumani
kumfanyia uchunguzi atakapojiunga na
kikosi cha timu ya taifa.
"Klabu itamfanyia uchunguzi wa kina na ni
mapema sana kusema Ozil atakuwa nje kwa
muda mrefu kiasi gani".
Ozil, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 42.5
mwaka jana, amekuwa akikandiwa kwa
kucheza chini ya kiwango akiwa na jezi ya
Arsenal.
Habari za kuumia kwake zinazokuja mwezi
wa pili ndani ya msimu mpya, ni pigo kwa
kochaa Arsene Wenger ambaye sasa idadi
ya majeruhi inaongezeka katika timu yake,
Ozil akkungana na Aaron Ramsey, Mathieu
Debuchy, Olivier Giroud pamoja na Mikel
Arteta. |
KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment