Wednesday, October 08, 2014
 |
| Maandamano ya walimu kuingia katika Uwanja
wa Kaitaba mjini Bukoba kuadhimisha Siku ya
Walimu Duniani, juzi yalipata mtafaruku baada
ya polisi kuyaingilia na kuchana bango
mojawapo lililohoji posho za wajumbe wa Bunge
la Katiba.
Bango hilo la kitambaa cheupe lilikuwa na
maandishi yanayohoji posho ya Sh300,000
(Sh230,000 kama posho ya kujikimu na
Sh70,000 ambazo ni posho ya vikao) waliyokuwa
wanapata wajumbe wa Bunge la Katiba,
yakilinganishwa na kazi kubwa wanayofanya
walimu.
Ujumbe wenyewe ulisomeka hivi: “Haki iko
wapi? Usawa uko wapi? Posho ya Mjumbe
Bunge la Katiba Tsh 300,000/= mshahara wa
Mwalimu Tsh 370,000/= kwa mwezi. No big
results without big salary”.
Hata hivyo bango hilo lilichanwa hatua chache
kabla ya walimu hao hawajaingia uwanjani
humo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda.
Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania
(CWT), mkoani Kagera Dauda Bilikesi, alisema
amesikia habari za bango hilo kuharibiwa lakini
akasema asingezungumza kwa kina kuhusu
suala hilo kwa kuwa hayo yamepita. |
0 comments:
Post a Comment