Thursday, October 09, 2014
 |
| Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza
la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima
Mdee.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na
wenzake 8 leo wamepata dhamana katika
Mahakama ya Kisutu, Dar. Kesi yao
kutajwa tena Oktoba 21, 2014.
Siku ya jana washtakiwa hao walipanda
kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi
Kaluyenda na kusomewa mashtaka mawili
na Wakili wa Serikali Mkuu, Kangola
aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa
Kawe, Mdee, Rose Moshi, Penina Peter,
Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia
Fanuel, Edward Julius, Martha Mtiko na
Beatus Mmari.
Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa
makosa mawili la kwanza washtakiwa wote
wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa
Ufipa wilayani Kinondoni, walikaidi amri
ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf
iliyowataka watawanyike.
Shtaka la pili washtakiwa wote wanadaiwa
Oktoba, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa
ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo
moja walikusanyika kinyume na sheria
wakitaka kwenda ofisi ya rais |
KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment