Wednesday, October 08, 2014
 |
| Lengo lilikua ni kukutana na Shetta kwa ajili ya
kufanya interview kuhusu Tour yake ya Kerewa
aliyotembea nayo kwenye mikoa mbalimbali ya
Tanzania na nje ya Tanzania kwenye maeneo
mbalimbali kama Mombasa Kenya, so ilikua
iwe hivyo lakini kwa bahati nzuri akawa
amekuja na hili gari nikalazimika kumuomba
tupate za ndani kidogo itupe nguvu ya
kuzichanga.
Shetta ni staa wa single kama ‘ Nidanganye ‘ na
‘ kerewa ‘ ambazo zote alimshirikisha staa
mwingine wa bongofleva Diamond Platnumz
ambapo kwenye hii post ya leo on
millardayo.com ameziachia exclusive kadhaa
za hatua zake za kimaisha.
Anasema kwa yeyote ambae anahitaji
mafanikio kwenye hii dunia ni lazima awe na
Uvumilivu, uelewa wa kwamba sio kila siku
utapata, matumizi mazuri ya kinachopatikana
hata kama ni kidogo, kujifunza kuweka akiba,
kuishi na watu vizuri bila kujali unamjua au
haumjui pamoja na bidii kwenye kila nafasi
ndogo unayoipata, hayo ni baadhi ya mambo
ambayo anasema yanaweza kukuweka karibu
na mafaniko au kukupa mafaniko. |
 |
| Gari hili ambalo ni aina ya Harrier Lexus ni la
tatu toka Shetta aanze kumiliki magari ambapo
gharama yake ni shilingi milioni 45 kwenye
sehemu mbalimbali za kuuzia magari
Tanzania…… |
 |
| Mara nyingi huwa wengi wakiona picha kama
hizi wanauliza una nyumba? goodnews ni
kwamba kwa sasa Shetta anamalizia kujenga
nyumba yake Madale Dar es salaam hivyo
ameahidi kushare pichaz na sisi sio kuringishia
bali kutoa hamasa kwa vijana wengine
wanaomchukulia kama mfano kujifunza na
kupata nguvu ya kupambana kuzichanga
kutoka kwenye hali ya chini kama yeye
alieanzia muziki akiwa shule ya sekondari
Jitegemee. |
CRD MILARD AYO
0 comments:
Post a Comment