| Didier Nicolle ametaja kikosi cha wachezaji
18 kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars
itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mfaransa huyo ameita wachezaji 13
wanaocheza nje ya nchi hiyo akiwemo
kiungo Stephane Sessegnon wa West
Bromwich Albion ya Uingereza kwa ajili ya
mechi hiyo ya Kalenda ya FIFA itakayoanza
saa 11 jioni.
Wachezaji wengine katika kikosi hicho ni
Didier Sossa (AS Dragons FC de I’Oueme,
Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive
du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (FC
Liefering, Austria), Sessi D’almeida (FC
Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed
Aoudo (JS Saoura, Algeria) na Saturnin
Allagbe (US Krake, Benin).
Steve Mounie (HSC Montpellier, Ufaransa),
Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne 63,
Ufaransa), Jordan Adeoti (SM Caen,
Ufaransa), Michael Pote (Omonia Nikosia,
Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux,
Ufaransa) na Seidou Baraze (Kawkab
Marrakech, Morocco).
Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club,
Benin), Nafiou Badarou (ASO Chlef, Algeria),
Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin),
Fortune Ore (US Krake, Benin) na Seibou
Mama (US Krake, Benin).
Msafara wa timu hiyo utaanza kuingia nchini
kesho (Oktoba 9 mwaka huu) kwa nyakati
tofauti, na utakuwa umekamilika (Oktoba 10
mwaka huu). Timu hiyo itafikia hoteli ya JB
Belmont. |
0 comments:
Post a Comment