Wednesday, October 08, 2014
 |
| Home » Unlabelled » MPASUKO MZITO
WAINYEMELEA SOKA YA TANZANIA KISA
‘BIFU’ LA MALINZI NA KASSIM DEWJI
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MPASUKO mkubwa unainyemelea soka ya
Tanzania kufuatia taarifa za kuwapo
uhasama mzito baina ya Rais wa Shirikisho
la Soka (TFF), Jamal Malinzi na kigogo wa
kundi la Friends Of Simba, Kassim Mohamed
Dewji.
Mpasuko huo unavuka mipaka kutoka kuwa
wa wawili hao- hadi kuwa wa taasisi, yaani
Simba SC kwa ujumla na TFF, kila mmoja
baina yao akitumia chombo chake katika
mapambano.
Tayari kuna imani ya Simba SC kuchukiwa
na TFF ya Malinzi- na kadhalika TFF
wanaami wanapigwa vita na Friends Of
Simba (F.O.S).
Mara baada ya timu ya taifa, Taifa Stars
kutolewa na Msumbiji katika mechi ya
kuwania kupangwa kwenye makundi ya
kuwania tiketi ya Kombe la Mataifa ya Afrika
(AFCON) mwakani, kambi ya Malinzi
ilivujisha habari kwamba timu hiyo
ilihujumiwa na vigogo wa klabu kubwa.
Na siku chache baadaye, Malinzi akasema
ataunda Kamati ya kuchunguza tuhuma
hizo, vigogo mbalimbali wakiitwa kuhojiwa
na akaomba watoe ushirikiano, huku
akiweka mkwara ambaye hatatoa ushirikiano
atachukuliwa hatua.
Wakati bado matokeo ya tuhuma hizo
hayajatoka- Simba SC nao wanadai wana
ushahidi wa kutosha, Malinzi amekuwa
‘akitia mkono’ kwenye mechi zao za Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba SC imecheza mechi tatu mfululizo za
Ligi Kuu bila kushinda, ikitoa sare zote, 2-2
na Coastal Union na 1-1 mara mbili
mfululizo na Polisi Moro na Stand United,
tena mechi zote ikicheza Uwanja wa
nyumbani, Taifa, Dar es Salaam.
Baada ya sare ya Jumamosi na Stand,
Friends Of Simba wakaibua tuhuma kwamba
Msaidizi wa Malinzi, Juma Matandika
alikuwa na marefa wa mchezo huo siku
moja kabla ya mechi.
Na tuhuma hizi zinakuja wakati ambao kuna
mgogoro mzito baina ya Bodi ya Ligi na
Kamati ya Utendaji ya TFF juu ya makato ya
asilimia tano kutoka fungu la fedha la
udhamini wa ligi hiyo kuingia kwenye mfuko
wa Maendeleo ya Vijana.
Serikali, kupitia Wizara inayohusika na
michezo imeupoza mgogoro huo kwa
kuiagiza TFF ikutane na Klabu za Ligi Kuu
kuwasilisha ombi hilo badala ya kutaka
kulazimisha kukata asilimia tano, tu kwa
mawasiliano yake na uongozi wa Bodi ya
Ligi. |
 |
| Kassim Dewji maarufu kwa jina la utani KD, kwa muda mrefu amekuwa na tenda ya kuwauzia TFF jezi za timu za taifa, lakini tenda hiyo ilikatika baada ya Malinzi kuingia ofisini Oktoba mwaka jana.Inadaiwa kabla ya tenda hiyo kukatika, Malinzi aliwahi kuwa na kikao na Dewji ambacho mwisho wake ni matokeo ya tenda hiyo kufa. Inadaiwa, tangu hapo wawili wamekuwa na uhasama wa chinichini hadi sasa unaelekea kuwawazi.Inadaiwa sababu kubwa ya Malinzi kuonekana anataka kumbeba Michael Wambura katika uchaguzi wa Simba SC ni kwa kuhofia F.O.S. wakiingia madarakani kwenye klabu hiyo atakuwa na wakati mgumu TFF.Na uhusiano wa Malinzi na Friends of Simba ulianza kuingia doa wakati huo wa uchaguzi wa Simba SC- kwani F.O.S. waliona Rais huyo wa TFF anawasaliti baada ya kumsaidia kwa hali na mali wakati wa uchaguzi wa shirikisho.F.O.S. wanadai wao ndio waliombeba Malinzi katika uchaguzi wa TFF baada ya aliyekuwa mpinzaniwake mkubwa, Athumani Nyamlani kuwa anasaidiwa na mahasimu wa Simba SC, Yanga SC. |
 |
| Jezi za sasa za Taifa Stars baada yaMalinzi kumkatia tenda DewjiMalinzi na Dewji wote hawakupatikana kuzungumzia tuhuma hizo- ingawa BIN ZUBEIRY inaendelea na jitihada za kuwatafuta kwa ajili ya kuelezea hilo.Dewji alipokea simu mara moja wiki iliyopita na kusema yuko kwenye kikao apigiwe baadaye, lakini baada ya hapo akawa hapokei simu. Malinzi alikwepa kuzungumzia hayo wiki iliyopita akidai ana haraka na tangu hapo amekuwa hapokei simu pia. |
0 comments:
Post a Comment