Wednesday, October 08, 2014
 |
| KOCHA Arsene Wenger ameshtukia ujanja wa
mpinzani wake Jose Mourinho juu ya majeruhi ya
straika Diego Costa.
Wenger anayeinoa Arsenal, ambayo Jumapili
iliyopita ilimenyana na kikosi cha Chelsea alisema
anahisi Mourinho anawachezea akili wapinzani
wake kuhusu madai ya majeruhi ya misuli ya
straika wake huyo.
Alipoulizwa kuhusu maoni yake juu ya straika
huyo ambaye ni kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu
England mpaka sasa msimu huu, Wenger
alitabasamu kisha akasema: “Kusema kweli,
unapomtazama fowadi huyo uwanjani haonekani
kuwa ni majeruhi.
“Amekuwa na tatizo la misuli kwa muda mrefu na
tuliliona hilo kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya msimu uliopita, lakini nilipomtazama kwa
siku za karibuni, ni ngumu kuamini ni aina gani ya
majeruhi ya misuli yanayomsumbua.” |
0 comments:
Post a Comment