Wednesday, October 08, 2014

Vitu 8 vya kufanya kila asubuhi ili uweze kufikia Mafanikio kimaisha

Haya Msomaji wa mdadisiblog sikiliza nikuambie ni nini hasa mambo ya kufanya kila asubuhi ili uweze kupata mafanikio zaidi kimaisha. Binafsi hivi karibuni nimesoma makala katika moja ya magazeti nnayoyapenda na yalionyesha orodha za watu waliofanikiwa na wanachokifanya mara kwa mara. Kisha, nikaanza kutafiti zaidi kidogo na kupata mambo kadhaa muhimu ambayo yaliendana kwa watu hao. Hapa kwa haraka nitakushirikisha vitu  8 vya kufanya kila asubuhi:-

1. Amka Mapema

Jambo la kwanza la kufanya ukitaka kufanikiwa ni kuhakikisha unaamka mapema sana asubuhi. Watu waliofanikiwa huamka  kuanzia saa 10:30 hadi 11:30 asubuhi. Hapa nawalenga wale wanaoamka saa mbili asubuhi hadi saa tatu.Ukiamka mapema utaweza kupata kifungua kinywa mapema saa 01:30 asubuhi na kuwa na siku ndefu. Watu wengi wenye mafanikio huamka mapema.

2. Fanya Mazoezi

Mbali na kuamka mapema kufanya mazoezi ni jambo la muhimu pia na sio tu kufanya mazoezi bali kufanya mazoezi mapema asubuhi. Watu waliofanikiwa hufanya mazoezi asubuhi si kwa kupunguza miili yao tu bali kujipa afya ya akili katika kupambana na mambo aliyopanga kufanya katika siku hiyo.

3. Pata Kifungua kinywa (Breakfast)

Wote tunajua breakfast ni kitu muhimu ila je, Unajua kama watu waliofanikiwa huhakikisha wanapata breakfast kama jambo la msingi sana? Siongelei chai na maandazi nnaongelea chai nzito yenye vitu kama matunda au juice pamoja na maziwa/mayai ili kupata protini. Hii ni zawadi kubwa unayoweza kuupatia ubongo wako ili kuweza kuurahisishia kazi.

Hakikisha unapata breakfast masaa machache baada ya kuamka na kama jana yake usiku ulichelewa kula basi haishauriwi upate breakfast mapema.

4. Jipatie muda wa kuwa katika ukimywa

Sababu kubwa ya kuamka mapema ni kujipatia wasaa wa kuwa katika hali ya ukimywa. Unapoamka na kufanya mazoezi ni kujipa muda tosha na kuupa ubongo wako fursa ya kuwaza kuhusu mambo yako tu wala si kelele za watoto ndani ya nyumba au watu wengine.

Fikiria kuhusu majukumu yako ya siku hiyo na vitu unavyohitaji kufanya na kama itakusaidia unaweza kuandika chini. Kila siku zinapoenda utajikuta unazoea wasaa huu wa kuwa kimya hata kujiongezea muda wa jambo hili.

5.  Jipange

Kitu kingine ambacho kinafanana kwa watu waliofanikiwa ni pale wanapojipanga jinsi watavyoitumia siku yao. Kila asubuhi panga jinsi ya kutumia siku yako anza na kupanga vifaa vyako vya kazi, panga muda utaotumia kufanya kila jambo ikiwemo kula chakula cha mchana. Tandika kitanda chako na acha nyumba yako katika hali ya usafi. Kila mara unapoacha kufanya baadhi ya mambo haya taarifa za kukuletea mawazo (stress) hutumwa katika ubongo wako.
Ukijipanga utafurahia siku yako na kufanya mambo mengi zaidi kwa umakini unaohitajika.

6.  Achana na mambo ya siku iliyopita.

Kitu muhimu kila asubuhi ni kutoamka ukijilaumu kwa maamuzi na vitu ulivyovikosa jana. Kama uligombana na mtu jana, au mwajiri wako alisema kitu cha kukuudhi, au haukupata ile nyongeza ya mshahara uliyotarajia. Acha mambo ya aina hii. Kama ulimkosea mtu, hakikisha unamuomba msamaha. Achana na yaliyopita na weka akili yako kwa mambo ya leo.

Kila mtu aliyefanikiwa anaianza siku yake kwa kuwa na tabia mpya, mipango mipya na nguvu mpya na sio kujilaumu. Tabia hii itakupa uwezo wa kufanikiwa kwa siku husika.

7. Kuwa na Imani

Anza siku kwa kujitamkia maneno ya kujikumbusha kuwa una uwezo wa kuimaliza siku hii kwa kuchukua fursa zote zitakazo jitokeza, kufanya maamuzi sahihi na kuwa mvumilivu. Fanya Sara kulingana na Imani yako kwa Mungu.

8. Soma

Ikiwa ni habari kwenye gazeti, soma barua pepe, au soma kurasa chache za kitabu unachokipenda. Kusoma asubuhi ni kuzuri kwa mazoezi ya akili yako.

0 comments:

Post a Comment