Wednesday, October 08, 2014
 |
| Rapper wa Tamaduni Muzik, Nikki Mbishi
anatarajia kuachia wimbo mpya ‘Kupanda na
Kushuka’ aliowashirikisha Lady Jaydee, Songa na
One the Incredible.
Nikki amesema ameamua kuwashirikisha wasanii
hao ili kupata kitu tofauti kama muziki
unavyohitaji.
“Unajua muziki sometimes unahitaji vitu fulani
fulani ili uwe mzuri zaidi na hii ni kawaida ya
muziki ulivyo. Kwahiyo tukaona tukifanya kitu
kwa pamoja kitakuwa safi tukaingia studio za
Man Walter tukafanya wimbo ‘Kupanda na
Kushuka’, ni wimbo ambao unaelezea maisha ya
kawaida kupanda na kushuka kwa maisha, leo
umepata kesho umelala njaa lakini ni maisha.
Wimbo utatoka hivi karibuni pamoja na video,”
alisema Mbishi. |
0 comments:
Post a Comment