Thursday, August 21, 2014

KIAFRIKA ZAIDI: KWAHILI HAKUNA MZUNGU ANAYEWEZA…..!!!!!

Picha: Mfahamu ‘baby mama’ wa Professor J, ‘Mama Lisa’

Black Rhyno amewahi kuoa kumzidi kaka yake Professor J lakini hiyo haimaanishi kuwa Mchawi huyo wa Rhymes hana mke mtarajiwa. Kupitia Instagram, Professor J amemweka wazi mwanamke anayeweza kushika wadhifa wa Mrs Joseph Haule. “OF COURSE ni Baba LISA na Mama LISA. …. What more can I SAY?? #MWANALIZOMBE,” ameandika Professor kwenye picha hiyo juu.

CHEKI GAZETI LA MICHEZO LA AS LA HISPANIA LILIVYOANDIKA KUHUSU UJIO WA REAL MADRID

Gazeti maarufu la michezo la AS la nchini Hispania, limetumia ukurasa mzima kuelezea ziara ya kikosi cha wakongwe cha Real Madrid. Gazeti hilo limeelezea namna kikosi hicho kinavyofanya ziara kwa mara ya kwanza barani Afrika. Madrid watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania Eleven ambao wameanza kujifua chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa. Mechi hiyo itapigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Madrid wanatarajia kuanza kuwasili kesho. Kati ya wadhamini wa ziara hiyo na mechi ya kirafiki ni TSN ambao pia ni waratibu wa ziara hiyo, Hoteli ya Sapphire, Bin Slum, Gazeti la Championi na kampuni ya ndege ya Fast Jet. Na salehe ally

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUNAOMBA UJIUNGE NASI KWA KUBONYA HAPA 

Picha: Hii ndo hotel ambayo wachezaji waliochaguliwa kukipiga na wakongwe wa Realmadrid Agosti 23 wameweka kambi

Kikosi cha Tanzania Eleven chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa, kitaweka kambi kwenye hoteli maarufu ya kisasa ya Sapphire Court ya jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo inatarajia kuanza leo na wachezaji wataingia kambini hapo kujiandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya wakongwe wa Real Madrid itakayopigwa jijini Dar es Salaam, Jumamosi. Madrid itaongozwa na Luis Figo aliyewahi kuwa nota wa Barcelona, baadaye Real Madrid na Inter Milan. Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu na tayari tiketi zimeanza kuuzwa katika sehemu mbalimbali.Na mdadisiblog/festosaimon

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI 

WACHEZAJI WA MAN CITY WAZIDI KUJITUNDIKA VITANZI,HUYU NAYE AJITUNDIKA KITANZI CHA MIAKA MINNE

MSHAMBULIAJI Edin Dzeko amesaini Mkataba wa miaka minne na mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City. Mwanasioka huyo wa kimataifa wa Bosnia ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter juu ya kusaini kwake mkataba mpya akisema: "Furaha na kujivuniaa kusaini mkataba wangu mpya na Manchester City. Nipo hapa ambako ni kwangu. Nimerefusha hadi 2018,". Mpachika mabao huyo amefunga mara 65 katika mechi 156 alizoichezea klabu hiyo tangu ajiunge nayo kutoka Wolfsburg mwaka 2011. Na mdadisiblog/,festosaimon

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYEZA HAPA 

SIMBA NA YANGA OKTOBA 12 NA FEBAURI 8, MECHI ZAO NA AZAM FC…RATIBA KAMILI LIGI NZIMA HII HAPA

WATANI wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba SC na Yanga watakutana Oktoba 12, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mzunguko wa kwanza, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ladha ya Ligi Kuu ni mechi baina ya miamba hiyo miwili nchini- na kidogo mechi zinazozihusisha timu hizo na mabingwa watetezi, Azam FC, nazo pia huwa za kukata na shoka. Msimu uliopita, mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya 3-3, Simba wakitoka nyuma kwa 3-0 hadi mapumziko na marudiano, Yanga walisawazisha dakika za lala salama kupata sare ya 1-1. Lakini Simba SC ilijichukulia ubabe wa jumla wa msimu dhidi ya watani wao, baada ya kuwafunga Yanga SC 3-1 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe Desemba mwaka jana Uwanja wa Taifa. Mzunguko wa pili, timu hizo zitakutana Februari 8, mwakani, mchezo wa kwanza Yanga mwenyeji, wa pili Simba mwenyeji. Azam FC na Simba zitakutana Januari 1, mwaka 2015 wakati marudiano yatakuwa ni Aprili 12, mwaka huo. Yanga itamenyana na Azam FC Novemba 9, mwaka huu wakati mchezo wa marudiano utapangiwa siku. Ikumbukwe Septemba 13, Yanga na Azam FC zitafungua pazia la Ligi Kuu kwa mchezo wa Ngao ya Jamii Uwanja wa Taifa.

Wednesday, August 20, 2014

RATIBA LIGI KUU YATOKA; YANGA SC KUANZA NA MTIBWA SUGAR MOROGORO, AZAM NA POLISI MORO, SIMBA NA COASTAL DAR

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC wataanza na Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Septemba 20, mwaka huu, wakati Yanga SC waliomaliza nafasi ya pili wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro siku hiyo. Washindi wa tatu, Mbeya City wataanza na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya Septemba 20 na washindi wa nne, Simba SC wataanza na Coastal Union ya Tanga Septemba 21, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu zitakuwa kati ya Stand United watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. ITAENDELEA:

FIFA YAIPIGA NYUNDO NZITO TIMU YA BARCELONA

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limepiga nyundo kwenye kidonda baada ya kuizua Barcelona kusajili hadi Januari 2016. Awali Barcelona ilikata rufaa kwa Fifa ikipinga adhabu hiyo, badala yake Fifa imetia msisitizo kuhusiana na adhabu hiyo. Sasa Barcelona itaendelea kusubiri kufanya usajili hadi mwaka keshokutwa!. Na mdadisiblog/festosaimon

CHID BENZ AMWAGA MACHOZI CLOUDS ALIVYOKUWA ANAELEZEA STORY YA DIAMOND KABLA HAJAKUWA STAR

Chidi Benz alitabiri mbele ya Diamond Platnumz (wakati bado underground) kuwa angekuja kuwa msanii mkubwa. Hata hivyo maneno muhimu ambayo rapper huyo alimwambia Diamond ni kuwa asije kunywa pombe wala kuvuta (unga/bangi) maishani mwake. Chidi ambaye Jumanne hii ameachia single yake mpya 'Mpaka Kuche' aliyowashirikisha Diamond na AY, alikuwa akihojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM. Katika kuashiria kuwa hiyo ilikuwa ni interview iliyogusa sehemu ya katikati kabisa ya moyo wake, Chidi alijikuta akibubujikwa na machozi. Chidi alikumbushia siku Diamond alipompigia simu kujitambulisha kwake kuwa ni msanii mchanga anayetaka kumshirikisha kwenye wimbo wake. Hata hivyo siku Diamond amefanikiwa kumpata Chidi hewani ilikuwa ni baada ya kujaribu kumtafuta kwa siku nyingi bila mafanikio na aliwahi kumweleza mama yake namna alivyo na hamu ya kumshirikisha rapper huyo aliyekuwa akimkubali. Baada ya kumpigia simu, Chidi anadai alimuambia Diamond aende kwao maghorofani Ilala wakazungumze vizuri. "Sasa nikamuona (Diamond) nikajua huyo dogo ndio yule niliwaambiaga watu kuwa ‘huyu dogo ana sura moja hivi imekaa.. sura yake lazima utaiongelea tu, lazima utasema kitu, namuona atakuja kuwa staa tu, simjui lakini the way alivyo, atakuja kuwa staa,” alikumbushia Chidi.

DIVA WA CLOUDS FM ATUBU KUMKOSEA MSANII CHID BENZ BAADA YA KUMCHAFUA HUKO INSTAGRAM!!!

Mwanadada mtangazaji wa Clouds FM, Loveness maarufu kama DIVA..jana kupitia ukurasa wake wa Instagram alikili kumkosea msanii wa Bongo flava, Chid Benz....kutokana na comment yake ya siku za hivi karibuni kuhusiana na issue ya Chid kumpiga Ray C... Soma hapa alichokiandika!!!

DUNGA AWATOSA ALVES, MARCELO, AITA KIKOSI CHAKE KUWAVAA COLOMBIA

Kocha wa Brazil, Dunga ametangaza kikosi chake kwa ajili ya ya mechi za kirafiki dhidi ya Colombia, mechi itakayopigwa Septemba 5 jijini Miami, na dhidi ya Ecuador Septemba 9 jijini New Jersey, Marekani. Kati ya wachezaji aliowaita ni Miranda wa Atlético de Madrid na Filipe Luís. Lakini Dunga akaamua kuwaacha mabeki Dani Alves wa Barcelona na Marcelo wa Real Madrid. Nahodha Thiago Silva anayekipiga PSG pia ni mgonjwa, hivyo pia amemuacha katika kikosi chake. Wachezaji waliocheza Kombe la Dunia 2014 ambao Dunga amewaita ni Jefferson, David Luiz, Maicon, Luiz Gustavo, Fernandinho, Ramires, Oscar, Hulk, Willian and Neymar.

HAYA NDO MTOKEO YA MECHI KATI YA REALMADRID VS ATLETICO SUPER CUP YA KWANZA BERNABEU

REAL Madrid imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Atletico Madrid katika mchezo wa kwanza wa Super Cup ya Hispania usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu. Msambuliaji Crisitiano Ronaldo alitolewa kipindi cha pili kumpisha mchezaji mpya, James Rodriguez, kabla ya Mcolombia huyo kuifungia bao la kuongoza Real dakika ya 81. Atletico Madrid ilikomboa bao hilo zikiwa zimesalia dakika tatu kupitia kwa Raul Garcia na sasa Real Madrid itakabiliwa na mtihani mgumu katika mchezo wa marudiano Uwanja wa Vicente Calderon. Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric, Kroos, Alonso, Bale, Ronaldo/Rodriguez dk45 na Benzema. Atletico Madrid: Moya, Juanfran, Miranda, Godin, Siqueira, Mario, Gabi, Koke, Saul/ Griezmann dk56, Raul Garcia, Mandzukic

ORIJINO KOMEDI WAPATA PIGO JINGINE, MENEJA WAO AWAKIMBIA. SOMA HAPA

Kundi maarufu la vichekesho ambalo kwa sasa ni kama halipo, limepata pigo kubwa baada ya aliyekuwa meneja wao, mtangazaji nyota wa zamani wa televisheni, Christina Mosha maarufu kama Seven, kuwamwaga na hivyo kuachana nao. Akizungumza na gazeti hili juzikati, Seven alisema ameachana nao baada ya mkataba wake wa sasa kumzuia kufanya kazi na watu wengine zaidi ya walio chini ya mwajiri wake mpya. “Hivi sasa niko na Sony, wao wananizuia kufanya kazi na wasanii ambao hawako nao, hivyo baada ya mkataba wangu na wao kumalizika, nimeamua kuachana nao. Mimi ni mwakilishi wa Sony barani Afrika, ninashughulika na wasanii toka nchi tofauti za Afrika, kama Senegal, Kenya na kwingineko kasoro Afrika Kusini,” alisema.

COUTINHO AITWA BRAZIL MPYA BAADA YA KOCHA DUNGA KUBOMOA KIKOSI KILICHOVURUNDA KOMBE LA DUNIA

KOCHA mpya wa Brazil, Carlos Dunga amekibomoa kikosi cha timu hiyo kilichovurunda Kombe la Dunia kwa kuwatema wachezaji 13 na kuita wengine wapya. Philippe Coutinho ni miongoni mwa ingizo jipya la wachezaji baada ya Kombe la Dunia baada ya Dunga kuvutiwa na kazi yake akiichezea Liverpool, wakati Neymar aliyepona majeruhi yake yaliyomfanya akose mechi mbili za mwisho za Kombe la Dunia ameitwa pia. Kikois cha wachezaji 22 kimetajwa jana kwa ajili ya mechi mbili za kiradiki dhidi ya Colombia na Ecuador. Na mdadisiblog,/festosaimon

MAMBO YAIVA ZIARA YA REAL MADRID NCHINI… FIGO, OWEN NA KAREMEBU WATUA KESHO DAR

MWANASOKA bora wa zamani wa dunia, Mreno Luis Filipe Madeira Caeiro Figo anatarajiwa kutua kesho na msafara wa kwanza ya magwiji wa Real Madrid tayari kwa mchezo dhidi ya magwiji wa Tanzania Agosti 23 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Figo ataongozana na nyota wengine wawili waliowika Real Madrid muongo uliopita, mshambuliaji Michael Owen aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi Kombe la Dunia mwaka 1998 Ufaransa na mwanasoka bora wa Oceania mara mbili 1995 na 1998 Christian Karembeu. Figo aliyestaafu Mei 31 mwaka 2009, alipiga tuzo mbili mfululizo mwaka 2000, Mwanasoka Bora Ulaya na Dunia na anakuja Tanzania kuwakumbushia watu enzi zake anatamba Real Madrid. Mapokezi makubwa yameandaliwa kwa ajili ya magwiji hao Real Madrid ambao sasa wanakuja kwa awali na hadi Agosti 22 kikosi kizima kitakuwa kimekamilika Dar es Salaam. Mkurugenzi wa makampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), Farough Baghozah ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba magwiji hao watapokewa kwa maandamano Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na kupelekwa hoteli ya Ladger Plaza, Bahari Beach. Kikosi cha magwiji wa Tanzania, kitakachomenyana na Real Madrid kinaendelea mazoezi Uwanja wa Karume kwa wiki sasa kwa ajili ya mchezo huo wa kihistoria. Makipa maarufu waliowahi kuwika nchini, Mwameja Mohamed na Manyika Peter wamejumuishwa katika kikosi cha Tanzania All Stars kitakachomenyana na magwiji hao wa Real Madrid. Chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ na Wasaidizi Freddy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, Daktari Mwanandi Mkwankemwa na viongozi Mtemi Ramadhani, Hassan Mnyenye, Omar Gumbo na Hamisi Kisiwa kikosi hicho kitaingia kambini Dar es Salaam kujiandaa kwa mchezo huo wa Agosti 23, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wengine walioItwa ni mabeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu, Abubakar Kombo, George Masatu, Habib Kondo, Viungo Suleiman Matola, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo. Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka, Madaraka Suleiman na Akida Makunda. Wachezaji waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Real Madrid watakuja nchini. Katika ziara hiyo, pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania Agosti 23, pia watafanya utalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro. Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuja na Real nchini ni pamoja na Wanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Mfaransa Zinadine Zidane, Mreno Luis Figo na Mbrazil, Ronaldo Lima. Na mdadisiblog,/festosaimon

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG HII 

Barcelona wameitaja hii ndio bei ya Suarez lakini kuna mambo yanachanganya.

Tunafahamu kwamba Luis Suarez alijiunga na Barcelona mwaka huu wa 2014 akitokea Liverpool aliyoichezea toka mwaka 2011-2014 na kuifungia magoli 69 kwenye mechi 110 alizocheza. Sasa ishu imekuja kwenye ada ya uhamisho kwenda Barca ambapo club hiyo imeweka wazi jana kwamba ilimchukua kwa pounds milioni 65 kutoka Liverpool. Kuna mchanganyiko umetokea baada ya hiyo bei kutajwa kwa sababu Liverpool walisema bei waliyomuuza mng’ataji huyu ni Pound milioni 75.

HII NDIO SABABU YA MIMI KUAMUA KUTAFUTA MKWANJA KWA NGUVU ZOTE ILI SIKUMOJA NIJE KUWAPATA WATOTO KAMA HAWA

BAYERN WALIVUNJA 'PROMISI', WALIMUAMBIA GUARDIOLA KWAMBA, KROOS HATOUZWA

Bayern Munich walivunja ahadi waliyompa Kocha Pep Guardiola kwamba kiungo Toni Kroos hatouzwa. Uongozi wa Bayern ulimuahidi Guardiola ambaye alisisitiza kiungo huyo ni muhimu sana. Lakini mwisho ilishindikana, akauzwa kwa wababe wa Hispania, Real Madrid. Pamoja na kuwa na Xabi Alonso ambaye ni mmoja wa viungo nyota, Madrid imemwaga mamilioni kumtwaa Kroos ambaye tayari ameanza kuonyesha cheche. Na mdadisiblog/festosaimon

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI PUNDE ZITUFIKIAPO