Wednesday, August 20, 2014
 |
REAL Madrid imelazimishwa sare ya kufungana
bao 1-1 na Atletico Madrid katika mchezo wa
kwanza wa Super Cup ya Hispania usiku wa
jana Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Msambuliaji Crisitiano Ronaldo alitolewa
kipindi cha pili kumpisha mchezaji mpya,
James Rodriguez, kabla ya Mcolombia huyo
kuifungia bao la kuongoza Real dakika ya 81.
Atletico Madrid ilikomboa bao hilo zikiwa
zimesalia dakika tatu kupitia kwa Raul Garcia
na sasa Real Madrid itakabiliwa na mtihani
mgumu katika mchezo wa marudiano Uwanja
wa Vicente Calderon.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas,
Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric,
Kroos, Alonso, Bale, Ronaldo/Rodriguez dk45
na Benzema.
Atletico Madrid: Moya, Juanfran, Miranda,
Godin, Siqueira, Mario, Gabi, Koke, Saul/
Griezmann dk56, Raul Garcia, Mandzukic |
0 comments:
Post a Comment