Wednesday, August 20, 2014
 |
Kundi maarufu la vichekesho ambalo kwa
sasa ni kama halipo, limepata pigo kubwa
baada ya aliyekuwa meneja wao, mtangazaji
nyota wa zamani wa televisheni, Christina
Mosha maarufu kama Seven, kuwamwaga
na hivyo kuachana nao.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Seven
alisema ameachana nao baada ya mkataba
wake wa sasa kumzuia kufanya kazi na
watu wengine zaidi ya walio chini ya
mwajiri wake mpya.
“Hivi sasa niko na Sony, wao wananizuia
kufanya kazi na wasanii ambao hawako
nao, hivyo baada ya mkataba wangu na
wao kumalizika, nimeamua kuachana nao.
Mimi ni mwakilishi wa Sony barani Afrika,
ninashughulika na wasanii toka nchi tofauti
za Afrika, kama Senegal, Kenya na
kwingineko kasoro Afrika Kusini,” alisema. |
0 comments:
Post a Comment