Wednesday, August 20, 2014
 |
Kocha wa Brazil, Dunga
ametangaza kikosi chake kwa
ajili ya ya mechi za
kirafiki dhidi ya Colombia,
mechi itakayopigwa Septemba
5 jijini Miami, na dhidi ya
Ecuador Septemba 9 jijini
New Jersey, Marekani.
Kati ya wachezaji aliowaita
ni Miranda wa Atlético de
Madrid na Filipe Luís.
Lakini Dunga akaamua
kuwaacha mabeki Dani Alves
wa Barcelona na Marcelo wa
Real Madrid.
Nahodha Thiago Silva
anayekipiga PSG pia ni
mgonjwa, hivyo pia
amemuacha katika kikosi
chake.
Wachezaji waliocheza Kombe
la Dunia 2014 ambao Dunga
amewaita ni Jefferson,
David Luiz, Maicon, Luiz
Gustavo, Fernandinho,
Ramires, Oscar, Hulk,
Willian and Neymar. |
0 comments:
Post a Comment