Wednesday, August 20, 2014
 |
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, Azam FC wataanza na Polisi
Morogoro Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi, Dar es Salaam Septemba 20, mwaka
huu, wakati Yanga SC waliomaliza nafasi ya pili
wataanza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri,
Morogoro siku hiyo.
Washindi wa tatu, Mbeya City wataanza na JKT
Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya
Septemba 20 na washindi wa nne, Simba SC
wataanza na Coastal Union ya Tanga Septemba
21, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi nyingine za ufunguzi za Ligi Kuu
zitakuwa kati ya Stand United
watakaoikaribisha Ndanda ya Mtwara Uwanja
wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT
wataikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting
watakuwa wenyeji wa Prisons Uwanja wa
Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
ITAENDELEA: |
0 comments:
Post a Comment