 |
Gazeti maarufu la michezo
la AS la nchini Hispania,
limetumia ukurasa mzima
kuelezea ziara ya kikosi
cha wakongwe cha Real
Madrid.
Gazeti hilo limeelezea namna kikosi hicho
kinavyofanya ziara kwa mara ya kwanza barani
Afrika.
Madrid watacheza mechi ya
kirafiki dhidi ya Tanzania
Eleven ambao wameanza
kujifua chini ya Kocha
Charles Boniface Mkwasa.
Mechi hiyo itapigwa
Jumamosi kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam
na Madrid wanatarajia
kuanza kuwasili kesho.
Kati ya wadhamini wa ziara
hiyo na mechi ya kirafiki
ni TSN ambao pia ni
waratibu wa ziara hiyo,
Hoteli ya Sapphire, Bin
Slum, Gazeti la Championi
na kampuni ya ndege ya Fast
Jet. Na salehe ally |
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUNAOMBA UJIUNGE NASI KWA KUBONYA HAPA
0 comments:
Post a Comment