Thursday, August 21, 2014
 |
WATANI wa jadi katika soka ya Tanzania,
Simba SC na Yanga watakutana Oktoba 12,
mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara mzunguko wa kwanza,
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ladha ya Ligi Kuu ni mechi baina ya miamba
hiyo miwili nchini- na kidogo mechi
zinazozihusisha timu hizo na mabingwa
watetezi, Azam FC, nazo pia huwa za kukata na
shoka.
Msimu uliopita, mechi ya kwanza timu hizo
zilitoka sare ya 3-3, Simba wakitoka nyuma
kwa 3-0 hadi mapumziko na marudiano, Yanga
walisawazisha dakika za lala salama kupata
sare ya 1-1.
Lakini Simba SC ilijichukulia ubabe wa jumla
wa msimu dhidi ya watani wao, baada ya
kuwafunga Yanga SC 3-1 katika mchezo wa
Nani Mtani Jembe Desemba mwaka jana
Uwanja wa Taifa.
Mzunguko wa pili, timu hizo zitakutana
Februari 8, mwakani, mchezo wa kwanza
Yanga mwenyeji, wa pili Simba mwenyeji.
Azam FC na Simba zitakutana Januari 1,
mwaka 2015 wakati marudiano yatakuwa ni
Aprili 12, mwaka huo.
Yanga itamenyana na Azam FC Novemba 9,
mwaka huu wakati mchezo wa marudiano
utapangiwa siku. Ikumbukwe Septemba 13,
Yanga na Azam FC zitafungua pazia la Ligi Kuu
kwa mchezo wa Ngao ya Jamii Uwanja wa
Taifa. |
0 comments:
Post a Comment