Tuesday, October 21, 2014

Picha: Sitti Mtemvu akanusha kuwa na mtoto, asema ana miaka 23, hatovuliwa taji

Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amevilaumu vyombo vya habari kwa kueneza habari za uongo kuhusiana umri na maisha yake binafsi. Mtemvu amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. “Ukweli ni kwamba nina miaka 23 na cheti hicho hapo kinajielezea, mkitaka mnaweza kwenda hizo sehemu wanazotoa vyeti mkawauliza,” alisema Sitti. Mtemvu alisema cheti chake cha zamani cha kuzaliwa kilipotea akidai kuwa ni kutokana na maisha yake ya kusafiri mara kwa mara.
Sitti Mtemvu na mama yake wakiondoka baada ya kukutana na waandishi wa habari “Kwahiyo ilibidi pale walipohitaji cheti nilete kingine,” alijitetea. “Sikutegemea hayo maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo,” alijibu mrembo huyo baada ya waandishi wa habari kumtaka awape ripoti yoyote ya polisi kuhusiana na kupotea kwa cheti chake cha mwanzo. Cheti cha kuzaliwa alichonacho sasa kinaonesha kuwa kilitolewa September 9 mwaka huu.
Hashim Lundega akionesha cheti cha kuzaliwa cha Sitti Mtemvu Sitti alitumia pia fursa hiyo kukanusha tetesi kuwa ana mtoto. “Sina mtoto, na mkitaka tunaweza kwenda hospitali sababu naona kama mmekuwa mkiniandama kwa vitu ambavyo si vya kweli,” alisema. Akijibu swali la kuonekana kwa passport yake inayoonesha kuwa alizaliwa mwaka 1989 na huku kwenye cheti alichoonesha kikionesha amezaliwa May 31, 1991, Sitti alisema: Sitogusia hilo suala kwasababu mimi nilivyokuwa nakuja kuomba ‘Umiss Tanzania’ niliombwa cheti cha kuzaliwa sasa hivyo vitu vingine ni personal life, kwahiyo sidhani hata nyie kama kuna mtu atakuja anachukua passport yetu, ama driving licence ya kweli au feki na kuiweka kwenye mtandao kama ni kitu ambacho mngependelea.” Kwa upande wake Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited Hashim Lundenga alisema kuwa nafasi ipo wazi kwa wale wenye mashaka na umri na maisha ya Sitti kupeleka vielelezo halisi ambavyo watavifanyia kazi.
Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited Hashim Lundenga akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kushoto ni Miss Tanzania, Sitti Mtemvu “Tukishapata proof tutazifanyia kazi vizuri sana na mwenye haki atapata. Sisi hatuwezi kumvua taji, vitahusika BASATA na wizara husika,” alisema Lundenga. Kuhusu Sitti kudanganya kuwa na umri wa miaka 18 kama watu walivyodai ndivyo alivyosema, Lundega alidai kuwa hayo yamezushwa mtandaoni na kwenye shindano hilo hakuna aliyesema hivyo. “Unaamini kwamba Sitti ana miaka 18?” alihoji Lundenga. “Sasa kama huamini yote yametoka kwenye vyombo vya habari. Sisi tunaamini cheti cha kuzaliwa, sasa kama kuna mtu ana doubt na cheti cha kuzaliwa aende RITA akafanye uchunguzi wake.”

HILI NI PIGO LINGINE KUBWA LILILOPATA SANAA YA MUZIKI TANZANIA

Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family, YP amefariki dunia usiku wa jana katika hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua. YP Akizungumza na mdadusiblog leo, kiongozi wa kundi hilo, Said Fela, amethibitisha msiba huo na kusema ratiba kamili itatoka leo mchana. “Mpaka sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunasubirika kaka yake kwa sababu huyo mtu kafariki usiku hospitali. Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndo watasema tunazikaje, kwa sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa 7 mchana ratiba itakuwa tayari,” amesema Fela. “Tatizo alikuwa anaumwa kifua muda tu, lakini alishaanza kunywa dozi lakini majuzi akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi Mungu kampenda zaidi akamchukua. Wazazi wa marehemu wapo Keko pale, lakini wazazi wake baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na kuna kibanda waliachiwa na wazazi wake, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”

KOCHA WA SIMBA PATRICK PHIRI ANUNUA STAA WA JAGWANI

KOCHA wa Simba, Patrick Phiri, amepanga kufumua kikosi chake katika usajili wa dirisha dogo hapo Desemba ambapo ametamka kuwa anahitaji kuwa na makipa wanne wenye ushindani mkubwa na kusisitiza ni lazima afanye uamuzi mgumu juu ya hilo huku akitaka uongozi umnunulie kipa wa Yanga, Juma Kaseja. Kwa sasa Simba ina makipa watatu; Ivo Mapunda, Hussein Sharif ‘Casillas’ na Manyika Peter ambaye usajili wake ni wa U-20. Hiyo inamaanisha kwamba Kaseja akitua Simba uwezekano wa Mapunda kurejea Ligi Kuu Kenya ni mkubwa kama ilivyoanza kuvumishwa kwani Simba itakuwa na makipa wanne na nafasi yake kucheza itakuwa finyu. Phiri ameliambia Mwanaspoti kuwa alipatwa na wakati mgumu baada ya makipa wake wawili kuumia Ivo na Casillas na kubakiwa na mmoja tu Manyika ambaye hata hivyo alionyesha kiwango cha juu katika mechi yao na Yanga iliyochezwa Jumamosi iliyopita na kutoka suluhu. Baada ya mechi hiyo, Phiri alisema kuwa Manyika ana kiwango kikubwa lakini anahitaji awepo na kipa mbadala huku akitamani kumnasa Kaseja ambaye aliwahi kuidakia Simba kwa miaka 10. “Binafsi huwa namkubali Kaseja kuwa ni kipa bora kutokana na uwezo wake wa kudaka, ningependa kuwa naye kwani nimewahi kumfundisha na ninajua uwezo wake, nina makipa watatu ambao ni wazuri lakini kuelekea mechi ya Yanga wawili walikuwa na majeruhi, nilikuwa katika wakati mgumu ingawa nilimwamini Manyika,” Phiri alisema. “Nikisajili kipa mzoefu itanibidi niwe na uamuzi mgumu katika upangaji kwani ni lazima nikimtumia Manyika kutokana na uwezo aliokuwa nao, nikimkalisha benchi nitaua kiwango chake, atakuwepo kipa namba moja lakini wote watadaka kulingana na mechi zilivyo.” Kaseja kwa sasa hapati nafasi ya kudaka katika kikosi cha Yanga kwani kocha Marcio Maximo amemwamini kipa Deo Munishi ‘Dida’. Kuhusu safu ya ulinzi, Phiri alisema: “Pale kati Joseph Owino na Hassan Isihaka wanatosha sina haja ya kusajili, lakini beki wa pembeni ndio kuna tatizo kwani wapinzani wetu wamegundua tatizo hilo, hivyo nitaimarisha pembeni, kiungo mkabaji ambapo kwa sasa namtegemea sana Jonas Mkude. Nitaongeza na straika mmoja.” Kwa hesabu za Phiri basi uongozi wa Simba ambao msimu huu umesajili wachezaji 29 na kubakiwa na nafasi moja ili wafike 30 watalazimika kupunguza baadhi ya wachezaji wao ili wasajili wachezaji ambao kocha atapendekeza katika nafasi husika. Phiri aliongeza: “Matokeo haya (mfululizo wa sare) sio mazuri kabisa kwetu, tunahitaji ushindi, lakini pia ni bora tumetoka sare na Yanga kuliko wangetufunga maana ingeleta shida zaidi, tunaenda kucheza na Prisons ambao sijawaona uwezo wao hivyo lazima niongeze mbinu za kiufundi kuhakikisha ushindi ugenini unapatikana.” Simba ilianza mazoezi yake jana Jumatatu jioni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

ALIYEBANWA NA CANNAVARO, YONDANI AWAPIGA MAN UNITED BONGE LA BAO

Yule mshambuliaji wa timu ya taifa ya Benin aliyeshindwa kufurukuta mbele ya mabeki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani jana amepiga bonge la bao akiichezea timu yake dhidi ya Manchester United. Stephane Sessegnon amefunga bao hilo kwa shuti kali la kasi ya kilomita 91 kwa saa na kuifanya West Bwrom iongoze kwa bao moja dhidi ya Man United. Mshambuliaji huyo alitua jijini Dar es Salaam na kuingoza Benin iliyotandikwa kwa mabao 4-0 dhidi ya Taifa Stars. Bao lake lilikuwa moja ya mabao manne bora kwenye mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bao 2-2.

DUNIA INA MAMBO: DAWA YA KUKAMATA WEZI YAZUA BALAA...

Watu saba kati ya 100 Kijiji cha Kenyamanyori, Kata ya Turwa, Wilaya ya Tarime walioshiriki kunywa dawa ya mganga wa kienyeji aliyeletwa kutoka Busia nchini Kenya wameingia kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kulipa Sh3 milioni kila mmojaWanakijiji hao walikusanyika juzi asubuhi baada ya kengele ya kijiji kugongwa na uongozi, huku wakieleza kwamba ilikuwa siku ya nne kwa kengele hiyo kugongwa lengo likiwa ni kuzungumzia wizi unaoendeshwa na watu wasiojulikana.Inadaiwa wizi wa kuvunja maduka umekithiri kijijini hapo, baada ya wanakijiji hao kuwasili eneo la mikutano, walielezwa kusudio la kengele kuwa ilikuwa ni kutokana na kukithiri kwa matukio ya uhalifu. Miongoni mwa waliovunjiwa duka ni Ayubu Wambura, anayedaiwa kuleta mganga kutoka Busia nchini Kenya kuwabaini wahusika, hivyo kila mmoja aliombwa kunywa dawa ya mganga huyo au kuacha maana ni hiyari.

 BOFYA HAPA KUSOMA ZAID 

NDOA YA RAIS WA DUNIA MATATANI SOMA HAPA HABARI KAMILI LIVE!!

WASHINGTON -Michelle Obama has had enough. According to a bombshell new report, the First Lady and Barack Obama are sleeping in separate White House bedrooms. Michelle is also preparing to boot her hubby of 21 years out of their ritzy Chicago home - and seriously discussing divorce. “The smart money says the marriage is doomed,” a source told the National Enquirer. “Barack and Michelle have had a rocky go for years and mainly stayed together for their daughters and his political career. “But now Michelle is mad AS hell. She feels violated in front of the whole world, and screamed at him, ‘I’ve had enough.’ “She’s met with divorce lawyers and told Barack that she wants a life apart from him. “Michelle will stay in the White House for the rest of Barack’s term for appearances’ sake, but she made it clear they’ll be leading separate lives. “She’s moving into one of the vacant bedrooms in the family’s private living quarters, and she’s preparing to move his clothes and personal things out of their million-dollar house in Chicago.” Michelle was left furious after Barack was photographed brazenly flirting with Denmark’s dishy female prime minister, Helle Thorning-Schmidt, during the service for former South African president Nelson Mandela. Obama, 52, laughed and whispered with the 46-year-old Danish beauty throughout the solemn ceremony, at one point cavalierly caressing her shoulder. “Barack already had enough headaches with his public approval rating plummeting after the disastrous rollout of his ‘Obamacare’ health plan. Now he’s walked smack into the worst marital crisis of his life,” said the White House insider.

PERUZI KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI MBALIMBALI YA LEO JUMANNE ...HAPA

HUYU NDO MCHEZAJI ALIYEFARIKI AKIJARIBU KUSHANGILIA BAO KAMA MIROSLAV KLOSE

MWANASOKA amefariki dunia baada ya kuanguka vibaya aliporuka samasoti kushangilia bao katika mchezo wa Ligi Kuu ya jimbo la Mizoram nchini India. Peter Biaksangzuala amefariki akiwa hospitali Jumapili baada ya kuangukia kichwa chake aliporuka samasoti kushangilia bao aliloifungia Bethlehem Vengthlang FC - klabu yenye maskani yake Kaskazini Mashariki kwa jimbo la Mizoram. Mchezaji huyo aliyekuwa ana umri wa miaka 23 alifunga bao hilo dakika ya 62 kuisawazishia timu yake dhidi ya Chanmari West FC Jumanne katika mchezo wa Ligi na akataka kushangilia kwa staili ya mfungaji bora wa kihistoria wa Kombe la Dunia, Miroslav Klose.
Biaksangzuala alikosea katika kuruka kwake na akapigiza kichwa chini, kabla ya kupatiwa huduma ya kwanza uwanjani na kisha kutolewa nje kwa machela. Biaksangzuala alikimbizwa katika hospitali ya Aizawl Civil ambako vipimo vya CT vilionyesha amepata madhara makubwa kwa undani na mara moja akahamishiwa chumba cha wagonjwa walio chini ya uangalizi maalum. Chanzo kimesema: "Alijaribu kushangilia kama Mjerumani Klose, lakini akakosea kwa bahati mbaya. Alikaa hospitali kwa siku tano, lakini madaktari hawakufanikiwa kuokoa uhai wake,". Taarifa nchini India zinasema kwamba Biaksangzuala alichangia macho yake wakati akiwa amelazwa hospitali. Kwa ajili ya kumbukumbu ya kiungo huyo, Bethlehem Vengthlang FC imeamua kuipumzisha jezi namba 21 na Chama cha Soka Mizoram kimetoa taarifa
Peter Biaksangzuala (aliyezungushiwa duara kulia) amefariki dunia baada ya kuumia akishangilia bao
Biaksangzuala akikimbia kwenda kushangilia bao lake dhidi ya Chanmari West FC

EPL: HIKI NDO KILICHOIPATA MANCHESTER UNITED DHIDI YA WEST BROM USIKU HUU

BROM, SESSEGNON 'ALIYETIWA MFUKONI' TAIFA AWATIA KIMOJA, SARE 2-2 BAO la dakika ya 87 la kiungo Daley Blind limeinusuru Manchester United kulala mbele ya West Brom Albion baada ya kupata sare ya 2-2 ugenini katika mchezo wa Ligi Kuu England usiku huu. Blind alifunga bao zuri kutoka umbali wa mita 23, likiwa bao lake la kwanza tangu ajiunge na Mashetani hao Wekundu msimu huu. Stephane Sessegnon aliyeshindwa kufurukuta mbele ya Tanzania, Taifa Stars akiichezea Benin ikifungwa 4-1 katika mchezo wa kirafiki Oktoba 12 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, leo aliifungia WBA bao la kwanza dakika ya nane akimalizia krosi ya Andre Wisdom. Marouane Fellaini aliyetokea benchi dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Ander Herrera, aliisawazishia Manchester United dakika ya 48 akimalizia pasi ya Angel di Maria. Mzaliwa wa Burundi, Saido Berahino akaifungia bao lililoelekea kuwa la ushindia West Brom dakika ya 66 akimalizia pasi ya Chris Brunt, kabla ya Blind ‘kuchomoa’ dakika za lala salama. Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Rafael, Jones, Rojo, Shaw, Blind, Herrera/Fellaini dk46, Januzaj, Mata/Falcao dk72, Di Maria/Ashley Young dk76, Van Persie West Brom: Myhill, Wisdom, Lescott, Dawson, Pocognoli, Gardner, Brunt, Morrison, Dorrans, Sessegnon/Youssuf Mulumbu dk86 na Berahino.

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MSANII DAVIDO ALIVYOKUA AKIONDOKA TANZANIA!

Msanii Kutoka Nigeria, Adedeji Adelek maarufu kama ‘Davido' Ameweza kuwashukuru Watanzania kwa mapokezi waliyompatia pia pamoja na kushare jukwaa moja na Msanii kutoka Marekani T.I amesema hayo kupitia ukurasa wa Istragram pindi alivyokuwa anaondoka nchini Tanzania.
"Kwa heri Tanzania 26464! it was great sharing the stage with trouble man 31...thank you Clouds fm for napkin it possible and bless my brother @diamondplatnumz for welcoming me well" Aliandika DavidoLicha ya kwamba Aliweza kupikwa Mikwara na baadhi ya Vyombo vya Habari vya hapa nchi kuziiwa kufanya show hiyo.

Monday, October 20, 2014

BAADA YA KUFANYIWA KITU MBAYA KATIKA FIESTA 2014 DIAMOND PLATINUM AHAMUA KUWANYAMAZISHA WANAFKI KWA NJIA HII

Ommy Dimpoz atoboa siri ya picha anayoonekana akishuka kwenye treni ‘tusiamini kila tukionacho mtandaoni’

Baada ya kusambaa kwa picha ya Ommy Dimpoz anayoonekana akiwa kama kijana wa kijijini aliyetua mjini Dar es Salaam na watu wengi kuhisi ni picha yake ya zamani aliyopigwa wakati anatua Dar (kitu ambacho si kweli), ameamua kuelezea hisia zake. Akiweka picha nyingine kwenye Instagram lakini awamu hii akiwa na Vanessa Mdee (ambayo inaonesha kuwa ni moja ya kazi zake zitakazokuja), Ommy amesema amejifunza mengi kutokana na jinsi watu walivyoiongelea picha hiyo.
Ommy na Vanessa Mdee “Wiki iliyopita nimejifunza mambo mengi sana baada ya ile picha niliyodandia treni kusambaa kwenye mitandao kuna watu waliongelea km utani,kuna watu walinikebehi,wengine waliweka kwenye mitandao na kunitusi kabisa,”ameandika Ommy. “Ila nilichogundua Sio kila tunachokiona kwenye mitandao kina ukweli tujaribu kuwa wachunguzi,tuache mambo ya kucopy na kupaste jambo la mwisho kabisa siri ya Maisha anaijua mungu usimdharau mtu kwa muonekano unayemuona mshamba eti amekukuta mjini kesho ndo huyo huyo atakayekupa ajira tupendane tusidharauliane……Asante @vanessamdee kwa kupokea na fuko langu.”

TEAM DIAMOND YAZUNGUMZIA SUALA LA KUZOMEWA KWA DIAMOND KWENYE FIESTA

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amesema haoni kama wameathirika na kundi la watu waliomzomea msanii huyo wakati akitumbuiza Jumamosi hii kwenye show ya Serengeti Fiesta, Leaders Club jijini Dar es Salaam. Tale amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa walikuwa na taarifa kuhusu mpango huo hata kabla ya show na hivyo walijiandaa. “Tulikuwa tumemjenga kisaikolojia, kwahiyo hiyo ni sehemu ya kazi na mashabiki ingekuwa wanapiga kelele kama tumekosea show kweli, lakini sio hivyo. Show ilikuwa sawa,” amesema Tale. “Tunachojua sisi msanii wetu anafanya vizuri na sasa hivi nguvu zetu tumeelekeza katika tuzo. Wananchi wakaze kumpigia kula katika tuzo Channel O na MTV, sie sasa hivi tunasonga mbele, tunachojua chema chajiuza, kibaya chajitembeza.”

DOWNLOAD NGOMA MPYA YA MOMUSIC ~SIMAMA

MILIONI 58 ZAFUTA BAO TATU ZA WAZI SIMBA

MATAJIRI wa Simba wamefurahishwa na matokeo ya suluhu waliyopata dhidi ya Yanga na kusema bila kambi yao ya nchini Afrika Kusini wangeweza kufungwa si chini ya mabao 3-0 na Yanga. Kabla ya matokeo hayo ya juzi Jumamosi pale Uwanja wa Taifa, Simba ilikuwa Afrika Kusini ambako iliweka kambi ya siku nane kujiandaa na mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao ulimalizika suluhu. Akizungumza na Mwanaspoti, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji ‘KD’, alisema kikosi chao kilikuwa katika hali mbaya ya kuweza kupoteza vibaya mechi dhidi ya Yanga na wasingefanya jitihada hizo wangejikuta wanapata kipigo cha aibu. Dewji ambaye ndiye aliyekuwa mmoja wa waratibu wa kambi hiyo, alisema Yanga kabla ya mchezo huo walikuwa katika morali nzuri kuliko Simba. Alisema kambi na gharama mbalimbali walizoziingia zimewagharimu zaidi ya Dola 350,000 ambazo ni sawa na Sh58 milioni. “Hatukuwa katika hali nzuri, tulilazimika kutumia akili hiyo ya haraka kuinusuru klabu kupata kipigo cha aibu maana tuliangalia timu yetu kulinganisha na Yanga na kubaini endapo tusingeandaa ile kambi tungeweza kupata kipigo cha aibu cha si chini ya bao 3-0,”alisema Dewji. Matokeo hayo yamewakera mabosi wa Yanga waliokuwa wanataka ushindi kuziba kelele za Simba huku wachezaji kilio chao ni kukosa Sh80 milioni walizoahidiwa endapo wangeshinda huku Simba nao wakikosa Sh100 milioni ambazo wangepewa kama wangeishinda Yanga. “Tulipambana sana hasa sisi mabeki, lakini tatizo lilikuwa mbele katika umaliziaji tu, tulikuwa tunalala na fedha uongozi ulituletea Sh80 milioni taslimu na ukatuhoji nani akabidhiwe lakini ndiyo hivyo tumechemsha,” alisema kwa huzuni beki mmoja wa Yanga.

CRD:Mwanaspoti

HILI NI PIGO LINGINE KUBWA LILILOIPATA TASNIA YA FILAMU TANZANIA MCHANA WA LEO

Mdogo wa aliyekuwa muigizaji na muongozaji wa filamu marehemu George Otieno ‘Tyson’ aitwaye Benson Okumu Otieno 'Benii' enzi za uhai wake.

Mdogo wa aliyekuwa muigizaji na muongozaji wa filamu marehemu George Otieno ‘Tyson’ aitwaye Benson Okumu Otieno 'Benii' amefariki dunia ghafla katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar mchana leo. Msiba upo Sinza Vatican

Benii alikuwa muigizaji na muongozaji wa filamu mbalimbali nchini. Mipango ya mazishi ya kumpeleka kwao Kenya
GPL

HESHIMA: WEMA SEPETU APIGWA BAO NA FLORA MVUNGI NA MUMEWE H.BABA!

HESHIMA! Wanandoa, muigizaji Flora Mvungi ‘H.Mama’ na mwanamuziki Hamis Ramadhan ‘H.Baba’ wamemfunika mwigizaji Wema Sepetu kwa kupanga ghorofa. Mjengo wa wanandoa, muigizaji Flora Mvungi ‘H.Mama’ na mwanamuziki Hamis Ramadhan ‘H.Baba’ Akizungumzia mjengo huo walioupanga maeneo ya Mbezi-Jogoo, jijini Dar, H. Mama alisema yeye na mume wake wameamua kupanga nyumba hiyo si kwa sababu ya kumfunika mtu bali wanapenda kuwa huru na kuishi vizuri.
Flora Mvungi ‘H.Mama’ akiwa ndani ya mjengo hup na familia yake. “Hatushindani na mtu katika maisha yetu bali cha msingi tunaangalia nafsi zetu zinataka nini, kuhusu gharama yake, niache kidogo,” alisema Flora.Wema amepanga nyumba ya kawaida maeneo ya Kijitonyama jijini Dar.

BAADA YA MAMBO KUMFIKA SHINGONI: MISS TZ 2014 AKIMBILIA KANISANI

Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu aliopotangazwa mshindi. Ziba masikio, fanya yako! Wakati watu wakichonga juu ya sakata la madai ya kuwa na mtoto na utata juu ya umri wake, Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu anadaiwa kukimbilia kanisani. Habari za uhakika zilidai kwamba, baada ya kutwaa taji hilo hivi karibuni na kuibua sintofahamu, mrembo huyo alikimbilia kwenye Kanisa la Ufunuo kwa Nabii Yaspi Bendera lilipo Yombo-Buza jijini Dar kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha ndoto yake ya kuwa Miss Tanzania. Ilidaiwa kwamba, Sitti ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Temeke kwa leseni ya CCM, Abbas Zuberi Mtemvu, akiongozana na mama yake, walikwenda kwenye kanisa hilo kwa ajili ya kutoa shukrani kwa wema aliomtendea Mungu. “Watu wanaendelea kumsema mtoto wa mwenzao huku yeye anamshukuru Mungu kwa sababu hata kabla hajatwaa taji hilo alikuwa akisali hapa hivyo Mungu amepokea maombi yake na si vinginevyo kama watu wanavyomsimanga,” alisema muumini mmoja wa kanisa hilo.

 BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI 

OMMY DIMPOZ: ASANTE VANESSA MDEE KWA KUNIPOKEA FUKO LANGU

Baada ya kusambaa kwa picha ya Ommy Dimpoz anayoonekana akiwa kama kijana wa kijijini aliyetua mjini Dar es Salaam na watu wengi kuhisi ni picha yake ya zamani aliyopigwa wakati anatua Dar (kitu ambacho si kweli), ameamua kuelezea hisia zake.Akiweka picha nyingine kwenye Instagram lakini awamu hii akiwa na Vanessa Mdee (ambayo inaonesha kuwa ni moja ya kazi zake zitakazokuja), Ommy amesema amejifunza mengi kutokana na jinsi watu walivyoiongelea picha hiyo.

 BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI 

ALICHOFANYIWA DIAMOND FIESTA…NIMEAMINI MAISHA BILA UNAFKI HAYAENDI

Nakumbuka miaka mitano iliyopita aliyekuwa nguli wa filamu Nchini Tanzania marehemu “”Steven Kanumba”” alienda kwenye jumba la Big Brother….

amini usiamini bila sababu yyte ya maana watanzania ndo walikuwa wa kwanza kuanza kumsema kuwa hajui kuvaa, nani alimchagua , hajui kiingereza mpaka kufikia kumuigiza!!! Walisahau hata watu maruufu kama Messi na wengine wengi hawajui kuongea kabisa lugha hiyo..

Baada ya kifo chake watanzania hawahawa wakaanza kusema alikuwa nguli aliyetuwakilisha vizuri nje ya nchi na kulia sana!!!kumbe wakati akiwa hai tulikuwa tunamshusha chini..

Miaka mitano baadae Tanzania imempata mtu anayeiwakilisha vizuri nje ya mipaka na kuitangaza vizuri nchi yake..

Pasipokuwa na sababu za msingi (chuki binafsi tu)anapangiwa njama za kuzomewa na kuabishwa katika ardhi ya nchi yake ambayo kwa namna moja au nyingine kuna watu wameifahamu sababu yake!! Ukiuliza sababu za wengi wao kumchukia ni mafanikio yake lakini hata kama humpendi mtu hivi ndo hadi umzomee kwa kiasi kile !!!

leo na kesho naye huyu akitoka utaskia hawahawa waliokuwa wanamzomea wanaanza kusema jamaa alikuwa anatuwakilisha vizuri sana , ametutangaza sana kimataifa!! lakini Watanzania wenzake ndio vinara wa kumuangusha..

Si lazima kila mtu ampende Diamond ila kutumia nguvu kubwa sana kumuangusha mtu ni ishara ya uwoga na Roho ya kimaskini…

Nimeamini “”maisha bila unafki hayaendi”