Tuesday, October 21, 2014
 |
MWANASOKA amefariki dunia baada ya
kuanguka vibaya aliporuka samasoti
kushangilia bao katika mchezo wa Ligi Kuu
ya jimbo la Mizoram nchini India.
Peter Biaksangzuala amefariki akiwa
hospitali Jumapili baada ya kuangukia
kichwa chake aliporuka samasoti
kushangilia bao aliloifungia Bethlehem
Vengthlang FC - klabu yenye maskani yake
Kaskazini Mashariki kwa jimbo la Mizoram.
Mchezaji huyo aliyekuwa ana umri wa miaka
23 alifunga bao hilo dakika ya 62
kuisawazishia timu yake dhidi ya Chanmari
West FC Jumanne katika mchezo wa Ligi na
akataka kushangilia kwa staili ya mfungaji
bora wa kihistoria wa Kombe la Dunia,
Miroslav Klose. |
 |
Biaksangzuala alikosea katika kuruka kwake
na akapigiza kichwa chini, kabla ya
kupatiwa huduma ya kwanza uwanjani na
kisha kutolewa nje kwa machela.
Biaksangzuala alikimbizwa katika hospitali
ya Aizawl Civil ambako vipimo vya CT
vilionyesha amepata madhara makubwa kwa
undani na mara moja akahamishiwa chumba
cha wagonjwa walio chini ya uangalizi
maalum.
Chanzo kimesema: "Alijaribu kushangilia
kama Mjerumani Klose, lakini akakosea kwa
bahati mbaya. Alikaa hospitali kwa siku
tano, lakini madaktari hawakufanikiwa
kuokoa uhai wake,".
Taarifa nchini India zinasema kwamba
Biaksangzuala alichangia macho yake wakati
akiwa amelazwa hospitali.
Kwa ajili ya kumbukumbu ya kiungo huyo,
Bethlehem Vengthlang FC imeamua
kuipumzisha jezi namba 21 na Chama cha
Soka Mizoram kimetoa taarifa |
 |
Peter Biaksangzuala (aliyezungushiwa duara
kulia) amefariki dunia baada ya kuumia
akishangilia bao |
 |
Biaksangzuala akikimbia kwenda kushangilia
bao lake dhidi ya Chanmari West FC |
0 comments:
Post a Comment