Tuesday, October 21, 2014
 |
Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family, YP
amefariki dunia usiku wa jana katika hospitali ya
Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu
na ugonjwa wa kifua.
YP
Akizungumza na mdadusiblog leo, kiongozi wa kundi
hilo, Said Fela, amethibitisha msiba huo na
kusema ratiba kamili itatoka leo mchana.
“Mpaka sasa hivi bado hatujaandaa ratiba,
tunasubirika kaka yake kwa sababu huyo mtu
kafariki usiku hospitali. Kwahiyo ndugu zake
wakishakuja ndo watasema tunazikaje, kwa
sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa 7
mchana ratiba itakuwa tayari,” amesema Fela.
“Tatizo alikuwa anaumwa kifua muda tu, lakini
alishaanza kunywa dozi lakini majuzi akazidiwa
na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi
Mungu kampenda zaidi akamchukua. Wazazi wa
marehemu wapo Keko pale, lakini wazazi wake
baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na
kuna kibanda waliachiwa na wazazi wake,
kwahiyo msiba utakuwa Keko.” |
0 comments:
Post a Comment