Tuesday, October 21, 2014
 |
Yule mshambuliaji wa timu
ya taifa ya Benin
aliyeshindwa kufurukuta
mbele ya mabeki Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ na
Kelvin Yondani jana
amepiga bonge la bao
akiichezea timu yake dhidi
ya Manchester United.
Stephane Sessegnon
amefunga bao hilo kwa
shuti kali la kasi ya
kilomita 91 kwa saa na
kuifanya West Bwrom
iongoze kwa bao moja dhidi
ya Man United.
Mshambuliaji huyo alitua
jijini Dar es Salaam na
kuingoza Benin
iliyotandikwa kwa mabao
4-0 dhidi ya Taifa Stars.
Bao lake lilikuwa moja ya
mabao manne bora kwenye
mechi hiyo iliyoisha kwa
sare ya bao 2-2. |
0 comments:
Post a Comment