Tuesday, October 21, 2014
 |
Watu saba kati ya 100 Kijiji cha
Kenyamanyori, Kata ya Turwa, Wilaya ya
Tarime walioshiriki kunywa dawa ya
mganga wa kienyeji aliyeletwa kutoka
Busia nchini Kenya wameingia kwenye
wakati mgumu baada ya kushindwa
kutimiza masharti ya kulipa Sh3 milioni
kila mmojaWanakijiji hao walikusanyika
juzi asubuhi baada ya kengele ya kijiji
kugongwa na uongozi, huku wakieleza
kwamba
ilikuwa siku ya nne kwa kengele hiyo
kugongwa lengo likiwa ni kuzungumzia
wizi unaoendeshwa na watu
wasiojulikana.Inadaiwa wizi wa kuvunja
maduka umekithiri kijijini hapo, baada ya
wanakijiji hao kuwasili eneo la mikutano,
walielezwa kusudio la kengele kuwa
ilikuwa ni kutokana na kukithiri kwa
matukio ya uhalifu.
Miongoni mwa waliovunjiwa duka ni Ayubu
Wambura, anayedaiwa kuleta mganga
kutoka Busia nchini Kenya kuwabaini
wahusika, hivyo kila mmoja aliombwa
kunywa dawa ya mganga huyo au kuacha
maana ni hiyari. |
BOFYA HAPA KUSOMA ZAID
0 comments:
Post a Comment