Monday, October 20, 2014

BAADA YA MAMBO KUMFIKA SHINGONI: MISS TZ 2014 AKIMBILIA KANISANI

Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu aliopotangazwa mshindi. Ziba masikio, fanya yako! Wakati watu wakichonga juu ya sakata la madai ya kuwa na mtoto na utata juu ya umri wake, Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu anadaiwa kukimbilia kanisani. Habari za uhakika zilidai kwamba, baada ya kutwaa taji hilo hivi karibuni na kuibua sintofahamu, mrembo huyo alikimbilia kwenye Kanisa la Ufunuo kwa Nabii Yaspi Bendera lilipo Yombo-Buza jijini Dar kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha ndoto yake ya kuwa Miss Tanzania. Ilidaiwa kwamba, Sitti ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Temeke kwa leseni ya CCM, Abbas Zuberi Mtemvu, akiongozana na mama yake, walikwenda kwenye kanisa hilo kwa ajili ya kutoa shukrani kwa wema aliomtendea Mungu. “Watu wanaendelea kumsema mtoto wa mwenzao huku yeye anamshukuru Mungu kwa sababu hata kabla hajatwaa taji hilo alikuwa akisali hapa hivyo Mungu amepokea maombi yake na si vinginevyo kama watu wanavyomsimanga,” alisema muumini mmoja wa kanisa hilo.

 BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI 

0 comments:

Post a Comment