Tuesday, October 21, 2014
 |
Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amevilaumu
vyombo vya habari kwa kueneza habari za uongo
kuhusiana umri na maisha yake binafsi. Mtemvu
amesema hayo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. “Ukweli ni kwamba nina miaka 23 na cheti hicho
hapo kinajielezea, mkitaka mnaweza kwenda hizo
sehemu wanazotoa vyeti mkawauliza,” alisema
Sitti. Mtemvu alisema cheti chake cha zamani cha
kuzaliwa kilipotea akidai kuwa ni kutokana na
maisha yake ya kusafiri mara kwa mara. |
 |
Sitti Mtemvu na mama yake wakiondoka baada
ya kukutana na waandishi wa habari
“Kwahiyo ilibidi pale walipohitaji cheti nilete
kingine,” alijitetea.
“Sikutegemea hayo maswali leo kwahiyo sikuja
nimejiandaa kihivyo,” alijibu mrembo huyo baada
ya waandishi wa habari kumtaka awape ripoti
yoyote ya polisi kuhusiana na kupotea kwa cheti
chake cha mwanzo.
Cheti cha kuzaliwa alichonacho sasa kinaonesha
kuwa kilitolewa September 9 mwaka huu. |
 |
Hashim Lundega akionesha cheti cha kuzaliwa
cha Sitti Mtemvu
Sitti alitumia pia fursa hiyo kukanusha tetesi
kuwa ana mtoto. “Sina mtoto, na mkitaka
tunaweza kwenda hospitali sababu naona kama
mmekuwa mkiniandama kwa vitu ambavyo si vya
kweli,” alisema.
Akijibu swali la kuonekana kwa passport yake
inayoonesha kuwa alizaliwa mwaka 1989 na huku
kwenye cheti alichoonesha kikionesha amezaliwa
May 31, 1991, Sitti alisema:
Sitogusia hilo suala kwasababu mimi nilivyokuwa
nakuja kuomba ‘Umiss Tanzania’ niliombwa cheti
cha kuzaliwa sasa hivyo vitu vingine ni personal
life, kwahiyo sidhani hata nyie kama kuna mtu
atakuja anachukua passport yetu, ama driving
licence ya kweli au feki na kuiweka kwenye
mtandao kama ni kitu ambacho mngependelea.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Lino
International Agency Limited Hashim Lundenga
alisema kuwa nafasi ipo wazi kwa wale wenye
mashaka na umri na maisha ya Sitti kupeleka
vielelezo halisi ambavyo watavifanyia kazi. |
 |
Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited
Hashim Lundenga akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari, kushoto ni
Miss Tanzania, Sitti Mtemvu
“Tukishapata proof tutazifanyia kazi vizuri sana
na mwenye haki atapata. Sisi hatuwezi kumvua
taji, vitahusika BASATA na wizara husika,”
alisema Lundenga.
Kuhusu Sitti kudanganya kuwa na umri wa miaka
18 kama watu walivyodai ndivyo alivyosema,
Lundega alidai kuwa hayo yamezushwa
mtandaoni na kwenye shindano hilo hakuna
aliyesema hivyo.
“Unaamini kwamba Sitti ana miaka 18?” alihoji
Lundenga. “Sasa kama huamini yote yametoka
kwenye vyombo vya habari. Sisi tunaamini cheti
cha kuzaliwa, sasa kama kuna mtu ana doubt na
cheti cha kuzaliwa aende RITA akafanye
uchunguzi wake.” |
0 comments:
Post a Comment