Saturday, October 11, 2014

KOCHA STARS ASEMA KIKOSI CHAKE KIPO TAYARI KUIVAA BENIN

Kocha wa Taifa Stars,
Mart Nooij amesema kikosi
kipo tayari kwa ajili ya
mechi dhidi ya Benin.
Lakini akasisitiza,
haitakuwa mechi laini kama
ambavyo wengi wanafikiri.
"Tumejiandaa vizuri,
tunataka kucheza mpira
mzuri na kushinda, hayo
ndiyo malengo.
"Lakini Benin si timu
laini, hivyo tayari
wachezaji wanajua
wanacheza na timu ngumu
lakini inafungika,"
alisema Nooij raia wa
Uholanzi.
Stars imekuwa kambini kwa
wiki moja sasa ikijiandaa
na mechi hiyo.
Kikosi hicho kitamkosa
Mbwana Samatta ambaye
aliumia katika mechi ya
Ligi ya Mabingwa Afrika
akiitumikia TP Mazembe ya
DR Congo ambayo ilitolewa
kwenye hatua ya nusu
fainali.
Nyota wa nje watakaokuwa
kwenye kikosi hicho ni
pamoja na Thomas Ulimwengu
(TP-DR Congo), Mwinyi
Kazimoto (Al Markhiya-
Qatar) na Juma Luizio
(Zesco-Zambia).

SHEPU YANGU NI KAMA ANDAZI LILILONONA NDIO MAANA NAPATA WANAUME

Mtangazaji wa kituo cha Redio Times, Hadija Shaibu ‘Dida’.Aliweka bayana kwamba anaachika na kupata mwanaume mpya haraka kwa sababu ana shepu ya
kalimati (aina ya andazi linalonona).

MTANGAZAJI wa kituo cha Redio Times, Hadija Shaibu ‘Dida’, juzikati aliamua kutoa siri yake ya moyoni na kuweka wazi juu ya tabia yake ya kuachika na kupata mume mpya mara kwa mara  SOMA ZAID> 

SAMATTA NA BOCCO WATAKOSEKANA KESHO STARS NA BENIN, NOOIJ ATATUMIA MABEKI WATATU…KWA MFUMO UPI?

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM WASHAMBULIAJI wawili, Mbwana Ally Samatta na John Raphael Bocco ambao Mholanzi Mart Nooij amekuwa akiwatumia katika mechi zilizopita kucheza pamoja na Thomas Emmanuel Ulimwengu watakosekana kesho kwa sababu wote ni majeruhi. Samatta amebaki Lubumbashi baada ya kuumia akiichezea klabu yake, Tout Puissant Mazembe katika Nusu Fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ES Setif ya Algeria. Mazembe ilitolewa kwa mabao ya ugenini, baada ya sare ya jumla ya 4-4. Bocco wa Azam FC anaendelea kuuguza goti aliloumia Agosti kwenye Robo Fainali ya Kombe la Kagame, dhidi ya El Merreikh ya Sudan mjini Kigali, Rwanda. Azam ilitolewa kwa penalti. Maana yake, kama kocha huyo Mholanzi ataendelea kutumia mfumo wa 4-3-3 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kesho dhidi ya Benin, atalazimika kuwa na wachezaji wa kuziba pengo la wawili hao. Ameonekana ni muumini wa wachezaji wenye maumbo makubwa- na katika kikosi alichoteua zaidi ya Ulimwengu, anabaki na washambuliaji wengine wawili, Mwegane Yeya wa Mbeya City na Juma Luizo wa ZESCO United ya Zambia. Ni hao ambao watachukua nafasi za Samatta na Bocco, au kocha Nooij atabadili mfumo? Tutajua kesho. Kwa kuwa tayari Nooij amesema katika mchezo huo atatumia mabeki watatu wa kati, ili kuwa na ukuta mgumu, mmoja wao akicheza kama kiungo mkabaji ili kuwapunguzia wenzake majukumu- maana yake kuna uwezekano akatumia mfumo wa 4-4-2 kesho. Kama atacheza na wachezaji saba katika ukuta, basi atahitaji japo wachezaji wawili katikati ili kutengeneza uwiano kati ya nyuma na mbele- jambo ambalo linaleta picha ya kutokuwa na washambuliaji watatu kesho. Kama baada ya ukuta wa watu saba atakuwa na viungo wengine wawili katikati- maana yake zitabaki nafasi mbili kwa ajili ya washambuliaji na viungo wa pembeni. Akiongeza kiungo mmoja atakuwa na nafasi tatu. Kuna shauku kubwa ya kutaka kujua kikosi cha Stars kitakuwaje kesho. Nooj amesema mpango wa kutumia mabeki watatu wa kati, unafuatia makosa yaliyofanywa na timu yake katika mechi ya mwisho dhidi ya Burundi ambayo ndani ya dakika 15 za kwanza walijikuta wanafungwa mabao mawili ya haraka haraka dakika ya kwanza na 12. Kwa ujumla, tangu ametua Stars Nooij ameiongoza Stars katika mechi nane na kati ya hizo, ameshinda mbili amefungwa tatu na kutoa sare tatu na katika mechi zote hizo nyavu za Stars zimetikiswa mara 12, huku yenyewe ikifunga mabao tisa. Bila shaka langoni ataendelea kusimama Deo Munishi ‘Dida’, beki ya kulia Shomary Kapombe, kushoto Oscar Joshua na katikati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kevin Yondan. Nani atakuwa beki wa tatu wa kati? Hilo ndilo swali kwa sababu katika mechi zilizopita amekuwa akimtumia Erasto Nyoni katika kiungo mkabaji, lakini kwa kupona Jonas Mkude maana yake anaweza kufanya mabadiliko. Na yatakuwa mabadiliko ambayo yatamfanya Nyoni arudi benchi au ndiyo akawe beki wa tatu wa kati? Said Mourad amekuwa akiingia kwenye mipango ya Nooij anapoamua kuongeza idadi ya mabeki- maana yake naye kesho na anafasi ya kuanza katika 11. Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amerudi katika fomu na viungo wengine Said Ndemla, Himid Mao na Amri Kiemba wote wapo vizuri, lakini Nooij amekuwa akimtumia Mwinyi Kazimoto kama kiungo mchezeshaji- kesho itakuwaje? Washambuliaji wa pembeni wote Mrisho Ngassa, Simon Msuva, Khamis Mcha ‘Vialli’ na Haroun Chanongo nao wapo vizuri maana yake katika mchezo huo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA wanaweza kucheza kwa zamu, lakini je akina nani wataanza? Katika jitihada za kuwa na kikosi cha uhakika, chenye wachezaji bora wa akiba, Nooij amewaita chipukizi beki wa kulia Miraj Adam, beki wa kushoto Edward Charles na beki wa kati Joram Mgeveke- nao bila shaka watapata nafasi kidogo kwenye mchezo wa kesho. Hivi sasa Nooij anajaribu kutengeneza timu ya kampeni za baadaye baada ya kukosa nafasi ya kwenda Morocco mwakani kwenye AFCON na mchezo wa kesho utakuwa hatua nzuri ya kuanzia.

King Majuto ajipanga kufanya filamu ya pamoja na Wema na Diamond

Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto amesema hivi kariburi alimshawishi Wema Sepetu azungumze na mpenzi wake Diamond Platnumz ili wafanye kazi ya pamoja. Mzee Majuto ambaye ni mshindi wa Tuzo za Watu 2014 ya filamu inayopenda, ameiambia Mdadisiblog kuwa amemwachia kazi hiyo Wema ili azungumzee na mzee (Diamond). “Hivi karibuni nilikuwa na Wema, nimemwambia aongee na Diamond ili tufanye filamu ya pamoja,” amesema Majuto. “Mimi, Wema na Diamond, hata Diamond ninaweza kuzungumza naye sema nimeanza na Wema kwanza, akikubali mtasikia tu.” Kwa upande mwingine Majuto amesema ili acheze filamu anahitaji kulipwa shilingi milioni 3. “Umri unaenda sasa biashara za nisaidie nisaide hakuna, kama unanitaka ili tufanye kazi unatakiwa uandae milioni 3.”

MAUAJI YA KUTISHA NDANI YA KANISA LA PAG BUKOBA, TAZAMA PICHA ZA TUKIO HILO

Katika hali isiyo ya kawaida,watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wamevamia Kanisa la PAG tawi la Kagemu kata ya Kitendaguro manispaa ya Bukoba na kumua muumini mmoja kwa kumcharanga mapanga hadi kufa na mwenzake kujeruhiwa ,hawakuiba chochote ikiwemo simu zao. Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na imani za kidini kwamba waliohusika na tukio hilo ni wapinzani ya dini yao.
Mtoa habari aliyegoma kutaja jina amesema chanzo cha mgogoro huo na kifo cha muumini ambaye ni mwalimu katika shule ya sekondari KAGEMU ni baada ya marehemu kuoa mwanamke wa dini nyingine ( inaifadhiwa ) na kumbadilisha dini huyo mkewe na hapo waumini wa dini ya mkewe walianza vitimbwi kwa kanisa hilo na hadi mauaji hayo kumekuwa na vurugu za kila mara baina ya pande mbili.
Polisi bado wanachunguza na watatoa taarifa baadae ,mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha maiti bukoba mjini ,majeruhi amelazwa hospital ya mkoa .

SUAREZ AREJEA RASMI UWANJANI HAPO JANA NA HATOA KALI NYINGINE KATIKATI YA MECHI BAADA YA .....

null
MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameichezea tena kwa mara ya kwanza Uruguay baada ya miezi minne ya kutumikia adhabu ya FIFA kwa kumng'ata begani Giorgio Chiellini wa Italia- kufuatia kuiongoza Uruguay kupata sare ya ugenini 1-1 na Saudi Arabia. Mshambuliaji huyo mpya wa Barcelona mwenye umri wa miaka 27, alipiga shut zuri la mpira wa adhabu ambalo liligongwa mwamba kabla ya beki Hassan Muath Fallatah kujifunga dakika ya 47. Hata hivyo, bao la Suarez ambaye alipunguziwa adhabu na Mahakama ya Usuluhishi ya FIFA (CAS) na kuruhusiwa kucheza mechi zisizo za mashindano, bao lake halikudumu kufuatia Naif Hazazi aliyetokea benchi kuisawazishia Saudi Arabia dakika ya mwisho. Amerudi; Luis Suarez akipongezwa na wenzake jana baada ya kusababisha bao la kuongoza la Uruguay Baada ya mechi, mchezaji huyo aliyehamia Barcelona kutoka Liverpool msimu huu kwa dau la Pauni Milioni 75, alisema: "Furaha kuvaa jezi hii tena ambayo inanipa mimi raha mno. Huwei kupoteza mapenzi yako kwa jezi. Uruguay!' Suarez, ambaye katikati ya mchezo aliomba ruhusa kwenda chooni mara moja na akakubaliwa na refa, kwa ujumla alicheza vizuri kwenye mchezo huo kabla ya kumpisha mwenzake dakika ya 70.

YULE DEMU TRAFKI ALIYEPIGA PICHA AKIPIGWA MABUSU KICHAKANI HUYU HAPA SASA AKIWA HANA SARE..!

Wezee Nimekutana na Hiyo Picha Instagram, Yule Polisi wa Kike Traffic Watu wamechimba Mpaka Wamepata Picha zake
Akiwa Bila sare za Kazini....

Baadhi ya Comment ni Hizi Hapa :

-mwambie alete CV mi ntamwajiri

-Aje kwangu atalelewa kuliko alivyokuwa huko!Contact pls

-Kajazia Sana hata Ingekuwa Mimi Ningekula Mzigo, hiyo ni ajali kazini

“Nimechoshwa kila siku kusikia Diamond, sasa ni bora nimtafute..." MTOTO MZURI MENINA AFUNGUKA YA MOYONI!

Akipiga stori na gazeti hili, Meninah ambaye ni zao kutoka shindano la kuibua vipaji vya kuimba, Bongo Star Search ‘BSS’ 2012 alisema;


“Nimechoshwa kila siku kusikia Diamond, sasa ni bora nimtafute mwanaume yeyote tu kisha nimtambulishe ili ijulikane siko na Diamond,” alisema Meninah ambaye yupo mbioni kuachia ngoma mpya ya Kaniganda.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa Meninah anatoka kimapenzi na Diamond, pia Diamond ameshafika kwao kujaribu kutoa mahari ili amuoe.

BAADA YA TRAFIKI SASA NI ZAMU YA POLICE...ANGALIA PICHA ALIOPIGA ASKARI HUYU AKIWA AMELEWA CHAKARI

Jamani sidhani kama kuna haja hata ya kutia neno hapa, picha yenyewe inajieleza! Wadhani hali hii inaashiria nini katika suala zima la nidhamu jeshini?!
Shuka hapo chini utoe maoni yako tafadhali!

BATA BATANI: MAISHA YA INSTAGRAM NI ZAIDI YA MAIGIZO..WATU WANAJUA KULA RAHA ASIKWAMBIE MTU!

Instagram ni zaidi ya uionavyo, watu wanajua kula raha asikwambie Mtu jionee mwenyewe… maisha mazuri hadi unashawishika kutaka kujua zaidi wanafanya nini…ntajaribu kuwatafuta hawa watupe siri ya mafanikio yao. 1. Vera Sidika anapenda clubs yaani mdada yeye ni full ku party. What I like from her she has a talent ni mchoraji balaa anaonekana msomi pia alisema karudi shule big up @queenveebossette naomba tuongee zaidi kuhusu vipaji vyako naamini watu watabaki vinywa wazi.. 2. Starlisha huyu naye ni mrembo wa instagram yeye anapenda kula sehemu nzuri, kupiga picha akiendesha magari mazuri na selfie za kumwaga. Mungu ni mkubwa kapunguza mabifu, sikuhizi yeye ni mshauri na mhamasishaji wa masuala mbali mbali ya maendeleo, hii inampa heshima safi sana @chaggabarbie naomba nijue siri ya utulivu wako, inapendeza sana. 3. Huddah kama hayuko airport, hotelini basi swimming pool @huddahthebosschick unapenda kuogelea we mtoto, umekaa kibiashara tu mara photo shoot, lebel yako ya mavazi iko hewan na mengine atleast unaonekana unafanya kazi. Hizo bikini ukiziweka sokoni utauza sana. Hongera 4. Masogange, picha nyingi yuko kitandani, kama sio kitandani bafuni kama sio nje ya nyumba then anarudi kitandani anajipiga mapicha weee hadi analala. Hongera nawe @officialagnes Mungu kakupendelea sana. Kuna wengine humu nashindwa kuwaelezea kwakweli…sitaki kujua sana maisha binafsi ya mtu ila natamani kujifunza au tujifunze kupitia hao “mastaa” Hakuna asiyependa kupiga mapicha all the time kalala, anaogelea, kwenye mahoteli makubwa na maboti anaenjoy maisha kama mnaweza kupiga mapicha hayo jamani tuonesheni na kazi zenu nasi tutamani kufikia huko??

MWALIMU APIGANA NGUMI NA MWANAFUNZI WAKE DARASANI, WANAFUNZI WAREKODI VIDEO BADALA YA KUAMULIA

Mwalimu wa sayansi katika shule ya Santa Monica High School alimstukia mwanafunzi huyu akijaribu kuuzia wanafunzi wenzake bangi darasani. Alipomkabili kuhusu tendo hilo, mwanafunzi huyo alimsukuma mwalimu huyo na ghafla ngumi zikaanza kurushwa hewani. Mwanafunzi huyo, Blair Moore, alikamatwa na polisi na kufunguliwa mashitaka ya kuingiza madawa, na kisu shuleni.
Wanafunzi wengi walikuwa upande wa mwalimu huyo, ikiwemo kuanzisha

HII NDIYO ARSENAL ILIYOITWA 'ARSENAL KWELI'

Hii ilikuwa Arsenal kweli; Wachezaji wa zamani wa Arsenal, kutoka kulia Thierry Henry, Robert Pires na Patrick Vieira na Ashley Cole aliyeipa mgongo kamera walioiwezesha The Gunners kushinda taji la mwisho la Ligi Kuu ya England mwaka 2004, tena wakiweka rekodi ya kutofungwa. Arsene Wenger kwa miaka sasa anapambana kurudisha enzi za mafanikio haya Arsenal.

THIERRY HENRY KUREJEA ARSENAL JANUARI...AMA ATAKWENDA PSG AU MONACO, AKIMALIZA MKATABA NEW YORK DESEMBA ....! JIBU LIPO HAPA

DESEMBA GWIJI wa Arsenal, Thierry Henry anavitoa udenda vigogo vya Ufaransa, Paris Saint- Germain na Monaco kwa mujibu wa taarifa nchini humo kwamba klabu hizo zinamtaka kumng'oa mshambuliaji huyo New York. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37, ambaye amekuwa akiichezea New York Red Bulls tangu mwaka 2010, atamaliza Mkataba wake na timu hiyo ya MLS mwishoni mwa mwaka na atakuwa tayari kurejea Ulaya Januari. Tetesi zimetawala kwamba Henry anajiandaa kustaafu, lakini Mshika Bunduki huyo wa zamani anaweza kurudi Arsenal kwa mara ya tatu au gazeti la Le10 Sport limesema Henry anaweza kujiunga na moja ya vigogo vya Ligue 1. Tetesi zinasema Henry anaweza kurejea tena Arsenal, ama akaenda kujiunga na PSG au Monaco Januari Mkuu wa Idara ya kabumbu wa New York, kocha wa zamani wa Liverpool, Gerard Houllier, amezungumzia tetesi kwamba Henry anaweza kucheza Ligi Kuu ya Ufaransa. "Ikiwa bado ana uwezo wa kucheza katika Ligue 1? Ndiyo, hakuna tatizo," Houllier ameliambia Le10 Sport. "Hadi sasa hakuna uamuzi uliochukuliwa, kwa namna moja au nyingine. Thierry bado hajaamua kuacha soka,"amesema Houllier.

Friday, October 10, 2014

BREAKING: Msanii wa bongofleva Baba Levo amepata ajali… maelezo yako hapa

Ni saa tisa kasoro mchana Msanii wa bongofleva Baba Levo anaipiga simu millardayo.com na kuongea kwa tabu kwenye usikivu ulio mdogo na kusema kwamba amepata ajali kwenye pori karibu na eneo linaitwa Uluwila akiwa anatokea Tabora kwenda Mpanda. Alikua kwenye Basi liitwalo AM ambapo ghafla wakiwa kwenye kona ilitokea Coaster ikiwa na abiria ambayo dereva wake alikua akikwepa barabara mbovu hivyo ikabidi ahamie kwenye upande wa pili wa barabara ambako ndiko lilikua linapita basi la kina Baba Levo ambalo hakuliona sababu ni kwenye kona. Dereva wa basi la kina Baba Levo ilibidi ahame upande wake ili ahamie kwenye upande wa magari yanayopanda ambao ndio upande sahihi wa ile Coaster kupita ambapo juhudi zake hazikufanikiwa kwani wote walikua kwenye spidi na yule dereva wa Coaster alihama kwenye ule upande baada ya kuona atagongana uso kwa uso na basi la kina Baba Levo ila bahati mbaya wakawa wote wamejikuta upande mmoja na wakagongana uso kwa uso. Mwenye makosa anatajwa kuwa ni mwenye Coaster ambapo pamoja na Baba Levo kuumia usoni na mwilini kwa kuchanwachanwa na vioo vya mbele vilivyopasuka kwenye basi, ameweza kuona kuna baadhi ya watu wamefariki ambapo kati yao ni waliopasuka vichwa na shingo. Dereva wa basi la kina Baba Levo hajaumia sana wala basi halijaumia sana, Coaster ndio imefumuka upande wa juu wote na kuharibika sehemu nyingine pia huku kilichosababisha Baba Levo kuumia ni kwamba alikua amekaa pale juu ya Injini ya Basi kwenye kigodoro kutokana na basi hilo kujaa. Baba levo anajisikia vibaya kiasi na kwa sasa yuko na wenzake kama 20 pamoja na Askari mwenye silaha waliekua pamoja kwenye Basi…. wanatembea kutafuta kijiji chenye network ili kuomba msaada manake baadhi ya abiria wamebanwa kwenye hiyo Coaster na hawajatolewa.

CRD MILLARDAYO

HUYU NDO DIRECTOR NA CAMERMAN ANAYEKUJA KWA KASI HAPA BONGO

Director na camera man anaekuja kwa kasi tanzania katika tansia ya filam unaweza wasiliana nae kupitia namba 0718 858182

WACHEZAJI WANAONGOZA KUFUNGA NA KUOKOA PENATI BARANI ULAYA – HAZARD, RONALDO, MESSI NANI ZAIDI?

Jumapili iliyopita, rekodi ya Leighton Baines kufunga penati zote alizowahi kupewa apige ilifikia tamati baada ya golikipa wa David De Gea wa Manchester United aliiokoa penati ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England.

Baines, alikuwa na rekodi ya kufunga penati 12 kati ya 12 mbili zlizopewa, lakini akaikosa penati penati yake ya 13 katika uwanja wa Old Trafford, hivyo rekodi yake kushuka mpaka kufikia 92.3%.

Baada ya Baines kuharibu rekodi yake ya kuwa na asilimia 100 katika ufungaji wa penati – je nani mwingine ambaye ana rekodi ya 100% katika ufungaji penati katika ligi kubwa barani ulaya.

Nimejaribu kufanya utafiti wa wachezaji wapigaji penati kuanzia msimu wa 2010-11 – hii tafiti iliwahusu wachezaji waliopiga 10 au zaidi na matokeo yalionyesha kama ifuatavyo…………

Best in Europe and England
– Eden Hazard (Chelsea): 16 penalties, 16 goals = 100%

Best in La Liga
– Cristiano Ronaldo (Real Madrid): 37 penalties, 35 goals = 94.6%

Best in the Bundesliga
– Sejad Salihovic (Hoffenheim): 24 penalties, 21 goals = 87.5%
Best in Serie A
Giuseppe Rossi (Fiorentina): 13 penalties, 12 goals = 92.3%

Best in Ligue 1
Ryad Boudebouz (Bastia): 11 penalties, 11 goals = 100%

MAGOLIKIPA WANAONGOZA KUOKOA PENATI

1. Julio Cesar (ex-QPR, now at Benfica): 11 penalties faced, six conceded.

2. Samir Handanovic (Inter Milan): 29 penalties faced, 16 conceded.

3. Asmir Begovic (Stoke): 12 penalties faced, seven conceded.

4. Bernd Leno (Bayer Leverkusen): 20 penalties faced, 12 conceded.

5. Kevin Trapp (Frankfurt): 13 penalties faced, eight conceded.

SAHAU KABISAA KUHUSU DIEGO COSTA.....! HUYU NDO MCHEZAJI BORA WA EPL MPAKA SASA

By Aidan Charlie Seif Mechi saba tayari zimechezwa na kila timu tukielekea katika mechi za kimataifa, ebu tuangalia nin nani amekuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya England mpaka kufikia hatua hii. Diego Costa? Sio kwangu mimi. Kura yangu inaenda kwa muargentina Angel di Maria. Ndio ni kweli Costa amekuwa na mwanzo mzuri, lakini amekuja na kuikuta timu ambayo ilitakiwa kushinda taji la ligi msimu uliopita – kama wasingepoteza zile points mwishoni mwa ligi dhidi ya Norwich, Sunderland, Crystal Palace na Aston Villa. Costa amekuja kuikuta timu iliyotulia na kupangwa vizuri, na sio klabu iliyo kwenye anguko baada ya kuwa na msimu mbaya.
Mwanzo mzuri wa Costa umewekwa kwenye kivuli na alichofanya Di Maria ndani ya Manchester United, ambapo amekutana na changamoto kubwa zaidi. Ikiwa Di Maria ataendelea na fomu aliyonayo hivi na United na kufanikiwa kuwapeleka Champions League, kwa hakika jambo hilo litakuwa ni kubwa zaidi kuliko kitu chochote atakachokifanya mchezaji yoyote wa Chelsea msimu huu. Tulichambue hili: Manchester United walikuwa wanatia aibu msimu uliopita. Baada ya zaman za ushindi za Ferguson, akaingia David Moyes. Mchezaji aliyekaa United kwa miaka 12 Rio Ferdinand alipotoa kauli kwamba Moyes alimfanya awe na mashaka juu ya kila kitu kuhusu hatma ya timu hapo unaweza kuona jahazi la Old Trafford lilivyokuwa likizama. Hali ilikuwa mbaya kiasi cha kufikia Nemanja Vidic akakakmilisha uhamisho wake na kuutangaza katikati ya msimu – uliona lini mchezaji mkubwa wa United anafanya hivyo chini ya utawala wa Fergie?
Huku wachezaji wakubwa wakipoteza hali ya kuitumikia klabu, United walikuwa wakielekea kwenye muelekeo mbaya kabisa. Walimaliza katika nafasi ya 7 na hawakushinda kikombe chochote. Baadae wachezaji watatu wa safu ya ulinzi wakaondoka – Ferdinand, Vidic na Patrice Evra. Wachezaji wakubwa na wazoefu kwenye kikosi. Kibaya zaidi kocha mpya akashindwa kuanza kazi mpaka Uholanzi ilipomaliza kampeni yake ya kugombea ubingwa wa dunia, na hata alipoanza kazi akaanza kuandamwa na balaa la majeruhi tena kwa wacheza muhimu – ukiangalia haya yote utafahamu uzito wa kazi iliyopo kuirudisha Manchester United ilipokuwa. Sawa wametumia fedha – na walihitaji kufanya hivyo ukiangalia namna hali ilivyokuwa mbaya. Lakini kwa mambo yote yalikuwa yakiizunguka United – Louis Van Gaal anastahili sifa. Usajili wa gaharama na mkubwa zaidi ulikuwa wa Di Maria. Wachezaji wanaonunuliwa kwa fedha nyingi inabidi wafanya mambo kwa kulingana na thamani yao – United walihitaji hilo kwa haraka kutoka kwa winga huyo wa kiargentina, na wamelipata hilo jambo. Baadhi ya wachezaji walionunuliwa kwa fedha nyingi kwenye Premier League wamehangaika kufanya mambo aliyofanya Di Maria – Robinho na Juan Mata ni mifano. And then tuangalie dili za uhamisho zinazomfanya Di Maria aonekane ni bargain kwa ada ya uhamisho wa £60million. Andy Carroll, Mesut Ozil na Fernando Torres wote walinunuliwa kwa fedha zilizovunja rekodi kwenye premier league na vilabu vyao. Carroll – £35m ya majeruhi. Ozil – £42m ya uvivu na kushindwa kukubaliana na ukweli wa kukataliwa na Real Madrid. Torres – £50m ya mshambuliaji anayekosa magoli lango likiwa wazi.
Di Maria amekuwa na kiwango kizuri mno. Ni jambo la furaha kuangalia akicheza soka. Ikiwa uamuzi wa kumchagua mchezaji bora wa mwaka utafanywa kwa kuangalia mfungaji bora wa mmoja wa wachezaji wa timu bingwa, then Costa au Fabregas watachukua tuzo hiyo. Lakini Di Maria anaongoza ukarabati wa Manchester United mpya. Ameingia na kuikuta timu ikiwa haina muelekeo wa kueleweka. Lakini tumeanza kuona mabadiliko – tayari ameipeleka United kwenye top 4, hata kama ni kwa muda lakini unaona timu ina ueleko mzuri. Wakati wachezaji wa United waliporipotiwa kumkasirikia Van Gaal kwa kumpumzisha Di Maria walipocheza Leicester, then utaona ni wazi namna mchezaji huyo alivyokuwa na umuhimu mkubwa. Kwa ada ya £60m anategemewa kutimiza matarajio ya waajiri wake Manchester United kwa haraka. Hana ulinzi wa safu nzuri ya mabeki nyuma pia. Costa ameingia kwenye kikosi cha Chelsea akikikuta kimaimarika. Di Maria kaingia kwenye timu ambayo haipo sawa na anahitaji kuundwa upya.

CHEKI PICHA ZA MWANAMKE ALIYEVUA NGUO KWA STAGE BAADA YA MZUKA KUMPANDA!

Haikupita ‘taimu’ kwani mzazi huyo alipotelewa na uungwana pale alipojikuta akisimama na kuanza kuserebuka sambamba na mwanaye. Kadri mapigo ya Vijana wa Masauti yalivyozidi kuchanganya, ndivyo midadi ya ‘mtu mzima’ ilivyozidi kupanda na kuanza kukata kiuno isivyo kawaida hukuakichojoa kiwalo kimoja baada ya kingine....mzuka wangu ukinipanda......Mzuka ulipokolea barabara, mama alijikuta akivua miwani yake ‘tintedi’ kwani ilikuwa ikimnyima raha kwa kutoona vizuri kwenye giza. Baada ya miwani vilifuatia viatu, blauzi na kubakiza sidiria, huku chini akishusha ‘skini jinsi’ yake na kusababisha bikini na viungo nyeti kuwa nje nje mbele ya mwanaye aliyekuwa akiangalia pembeni kwa aibu kuu.
...hata nguo huwa navua...!Mizuka ya mama huyo ilishindwa kutulizwa mpaka wasamaria walipoamrisha Vijana wa Masauti kuzima muziki ndipo mzazi huyo akatulia na kwenda kukaahuku watu wakimponda kwa kitendo chake cha kumwaga radhi mbele ya mwanaye. Baadaye alitimkia kusikojulikana huku mtoto akielekeza njia tofauti na walipoingia kwani mama ndiye aliyekuwa ‘dairekta’.

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

IRENE AKANUSHA VIBAYA SANA KUHUSU TUHUMA ZA KUTOKA NA MSAMI .. ! PIA AZUNGUMZIA UJIO WA MOVIE MPYA ALIYOIGIZA NA MSAMI

Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amesema anajiandaa kuachia filamu yake mpya iitwayo ‘Kisoda’. Uwoya amesema alisafiri hadi Afrika Kusini ili kutafuta location tofauti zitakazoifanya filamu hiyo kuvutia. “Filamu ya Kigoda ni filamu ya aina yake katika filamu ambazo nimewahi kuzifanya,” ameiambia Bongo5. “Filamu inahusu drama and music, imeshagharimu pesa nyingi sana. Ndani utaona watu wakicheza muziki na maisha ya wasanii. Kwahiyo itakuwa tayari hivi karibuni na tutatangaza ikiwa tayar kwenda sokon.” Katika hatua nyingine, Uwoya amekanusha uvumi kuwa ana uhusiano na msanii wa Soundtrack, Msami ambaye anadai ameshiriki kwenye filamu hiyo. “Msami sijawai kuwa na mahusiano naye, alikuwa kama msanii mwenzangu. Hata ule ukaribu wake na mimi ambao ulizua tetesi za kuwa na mahusiano naye ni kutokana na hii filamu. Kwahiyo watu wajue ilikuwa ni kazi tu.” CRD BONGO5

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA 

SIMBA SC KUKIPIGA NA TIMU HII KUBWA YA SOUTH AFRICA KUJIANDAA DHIDI YA YANGA

Katika kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga tarehe 18 Oktoba 2014, Simba itacheza mechi ya kujiandaa kwa kuingia kwenye uwanja na club kubwa ya Afrika Kusini. Simba ambayo iliondoka nchini jana keshokutwa (Jumamosi) itacheza mchezo wa kirafiki na Orlando Pirates mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Katika mchezo huo, Simba SC itawakosa wachezaji wake walio timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Uganda, The Cranes- ambao wanatarajiwa kujiunga na wenzao kuanzia Jumatatu. Hata hivyo, mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyekwenda kujiunga na The Cranes yeye hatakwenda kabisa Afrika Kusini, kwa sababu timu yake hiyo ya taifa itakuwa na mechi ya kufuzu AFCON katikati ya wiki. Wachezaji wa Simba SC walioko Stars ni; Miraji Adam, Joram, Mgeveke,Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo ambao wote watakwenda Afrika Kusini Jumatatu. Simba SC imefikia katika hoteli ya Eden Vale Petra na itakuwa inafanya mazoezi kwenye viwanja wa Eden Vale mjini Johannesburg.

KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA