| Ni saa tisa kasoro mchana Msanii wa
bongofleva Baba Levo anaipiga simu
millardayo.com na kuongea kwa tabu kwenye
usikivu ulio mdogo na kusema kwamba
amepata ajali kwenye pori karibu na eneo
linaitwa Uluwila akiwa anatokea Tabora
kwenda Mpanda.
Alikua kwenye Basi liitwalo AM ambapo ghafla
wakiwa kwenye kona ilitokea Coaster ikiwa na
abiria ambayo dereva wake alikua akikwepa
barabara mbovu hivyo ikabidi ahamie kwenye
upande wa pili wa barabara ambako ndiko
lilikua linapita basi la kina Baba Levo ambalo
hakuliona sababu ni kwenye kona.
Dereva wa basi la kina Baba Levo ilibidi ahame
upande wake ili ahamie kwenye upande wa
magari yanayopanda ambao ndio upande
sahihi wa ile Coaster kupita ambapo juhudi
zake hazikufanikiwa kwani wote walikua
kwenye spidi na yule dereva wa Coaster
alihama kwenye ule upande baada ya kuona
atagongana uso kwa uso na basi la kina Baba
Levo ila bahati mbaya wakawa wote
wamejikuta upande mmoja na wakagongana
uso kwa uso.
Mwenye makosa anatajwa kuwa ni mwenye
Coaster ambapo pamoja na Baba Levo kuumia
usoni na mwilini kwa kuchanwachanwa na vioo
vya mbele vilivyopasuka kwenye basi,
ameweza kuona kuna baadhi ya watu
wamefariki ambapo kati yao ni waliopasuka
vichwa na shingo.
Dereva wa basi la kina Baba Levo hajaumia
sana wala basi halijaumia sana, Coaster ndio
imefumuka upande wa juu wote na kuharibika
sehemu nyingine pia huku kilichosababisha
Baba Levo kuumia ni kwamba alikua amekaa
pale juu ya Injini ya Basi kwenye kigodoro
kutokana na basi hilo kujaa.
Baba levo anajisikia vibaya kiasi na kwa sasa
yuko na wenzake kama 20 pamoja na Askari
mwenye silaha waliekua pamoja kwenye Basi….
wanatembea kutafuta kijiji chenye network ili
kuomba msaada manake baadhi ya abiria
wamebanwa kwenye hiyo Coaster na
hawajatolewa. |
0 comments:
Post a Comment