Kocha wa Taifa Stars,
Mart Nooij amesema kikosi
kipo tayari kwa ajili ya
mechi dhidi ya Benin.
Lakini akasisitiza,
haitakuwa mechi laini kama
ambavyo wengi wanafikiri.
"Tumejiandaa vizuri,
tunataka kucheza mpira
mzuri na kushinda, hayo
ndiyo malengo.
"Lakini Benin si timu
laini, hivyo tayari
wachezaji wanajua
wanacheza na timu ngumu
lakini inafungika,"
alisema Nooij raia wa
Uholanzi.
Stars imekuwa kambini kwa
wiki moja sasa ikijiandaa
na mechi hiyo.
Kikosi hicho kitamkosa
Mbwana Samatta ambaye
aliumia katika mechi ya
Ligi ya Mabingwa Afrika
akiitumikia TP Mazembe ya
DR Congo ambayo ilitolewa
kwenye hatua ya nusu
fainali.
Nyota wa nje watakaokuwa
kwenye kikosi hicho ni
pamoja na Thomas Ulimwengu
(TP-DR Congo), Mwinyi
Kazimoto (Al Markhiya-
Qatar) na Juma Luizio
(Zesco-Zambia).








0 comments:
Post a Comment