 |
| Katika kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga
tarehe 18 Oktoba 2014, Simba itacheza mechi
ya kujiandaa kwa kuingia kwenye uwanja na
club kubwa ya Afrika Kusini.
Simba ambayo iliondoka nchini jana
keshokutwa (Jumamosi)
itacheza mchezo wa kirafiki na Orlando Pirates
mjini
Johannesburg, Afrika Kusini.
Katika mchezo huo, Simba SC
itawakosa wachezaji wake walio timu
ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na
Uganda, The Cranes- ambao
wanatarajiwa kujiunga na wenzao
kuanzia Jumatatu.
Hata hivyo, mshambuliaji Mganda,
Emmanuel Okwi aliyekwenda kujiunga
na The Cranes yeye hatakwenda
kabisa Afrika Kusini, kwa sababu timu
yake hiyo ya taifa itakuwa na mechi
ya kufuzu AFCON katikati ya wiki.
Wachezaji wa Simba SC walioko Stars
ni; Miraji Adam, Joram, Mgeveke,Jonas Mkude,
Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna
Chanongo ambao wote watakwenda Afrika
Kusini Jumatatu.
Simba SC imefikia katika hoteli ya
Eden Vale Petra na itakuwa inafanya
mazoezi kwenye viwanja wa Eden
Vale mjini Johannesburg. |
KAMA BADO UJAJIUNGA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI KWENYE FACEBOOK YAKO BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment