Saturday, October 11, 2014
 |
| Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini,
King Majuto amesema hivi kariburi alimshawishi
Wema Sepetu azungumze na mpenzi wake
Diamond Platnumz ili wafanye kazi ya pamoja.
Mzee Majuto ambaye ni mshindi wa Tuzo za
Watu 2014 ya filamu inayopenda, ameiambia
Mdadisiblog kuwa amemwachia kazi hiyo Wema ili
azungumzee na mzee (Diamond).
“Hivi karibuni nilikuwa na Wema, nimemwambia
aongee na Diamond ili tufanye filamu ya pamoja,”
amesema Majuto. “Mimi, Wema na Diamond, hata
Diamond ninaweza kuzungumza naye sema
nimeanza na Wema kwanza, akikubali mtasikia
tu.”
Kwa upande mwingine Majuto amesema ili acheze
filamu anahitaji kulipwa shilingi milioni 3.
“Umri unaenda sasa biashara za nisaidie nisaide
hakuna, kama unanitaka ili tufanye kazi
unatakiwa uandae milioni 3.” |
0 comments:
Post a Comment