Saturday, October 11, 2014
 |
| DESEMBA
GWIJI wa Arsenal, Thierry Henry anavitoa
udenda vigogo vya Ufaransa, Paris Saint-
Germain na Monaco kwa mujibu wa taarifa
nchini humo kwamba klabu hizo zinamtaka
kumng'oa mshambuliaji huyo New York.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37,
ambaye amekuwa akiichezea New York Red
Bulls tangu mwaka 2010, atamaliza Mkataba
wake na timu hiyo ya MLS mwishoni mwa
mwaka na atakuwa tayari kurejea Ulaya
Januari.
Tetesi zimetawala kwamba Henry
anajiandaa kustaafu, lakini Mshika Bunduki
huyo wa zamani anaweza kurudi Arsenal
kwa mara ya tatu au gazeti la Le10 Sport
limesema Henry anaweza kujiunga na moja
ya vigogo vya Ligue 1.
Tetesi zinasema Henry anaweza kurejea
tena Arsenal, ama akaenda kujiunga na PSG
au Monaco Januari
Mkuu wa Idara ya kabumbu wa New York,
kocha wa zamani wa Liverpool, Gerard
Houllier, amezungumzia tetesi kwamba
Henry anaweza kucheza Ligi Kuu ya
Ufaransa.
"Ikiwa bado ana uwezo wa kucheza katika
Ligue 1? Ndiyo, hakuna tatizo," Houllier
ameliambia Le10 Sport.
"Hadi sasa hakuna uamuzi uliochukuliwa,
kwa namna moja au nyingine. Thierry bado
hajaamua kuacha soka,"amesema Houllier. |
0 comments:
Post a Comment