Saturday, October 11, 2014
 |
| Katika hali isiyo ya kawaida,watu
wasiojulikana usiku wa kuamkia leo
wamevamia Kanisa la PAG tawi la Kagemu
kata ya Kitendaguro manispaa ya Bukoba na
kumua muumini mmoja kwa kumcharanga
mapanga hadi kufa na mwenzake
kujeruhiwa ,hawakuiba chochote ikiwemo
simu zao.
Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na imani
za kidini kwamba waliohusika na tukio hilo
ni wapinzani ya dini yao. |
 |
| Mtoa habari aliyegoma kutaja jina amesema
chanzo cha mgogoro huo na kifo cha
muumini ambaye ni mwalimu katika shule ya
sekondari KAGEMU ni baada ya marehemu
kuoa mwanamke wa dini nyingine
( inaifadhiwa ) na kumbadilisha dini huyo
mkewe na hapo waumini wa dini ya mkewe
walianza vitimbwi kwa kanisa hilo na hadi
mauaji hayo kumekuwa na vurugu za kila
mara baina ya pande mbili. |
 |
| Polisi bado wanachunguza na watatoa
taarifa baadae ,mwili wa marehemu
umeifadhiwa katika chumba cha maiti
bukoba mjini ,majeruhi amelazwa hospital
ya mkoa . |
0 comments:
Post a Comment