Saturday, October 11, 2014
 |
| Instagram ni zaidi ya uionavyo, watu wanajua
kula raha asikwambie Mtu jionee mwenyewe…
maisha mazuri hadi unashawishika kutaka kujua
zaidi wanafanya nini…ntajaribu kuwatafuta hawa
watupe siri ya mafanikio yao.
1. Vera Sidika anapenda clubs yaani mdada yeye
ni full ku party. What I like from her she has a
talent ni mchoraji balaa anaonekana msomi pia
alisema karudi shule big up @queenveebossette
naomba tuongee zaidi kuhusu vipaji vyako
naamini watu watabaki vinywa wazi..
2. Starlisha huyu naye ni mrembo wa instagram
yeye anapenda kula sehemu nzuri, kupiga picha
akiendesha magari mazuri na selfie za kumwaga.
Mungu ni mkubwa kapunguza mabifu, sikuhizi
yeye ni mshauri na mhamasishaji wa masuala
mbali mbali ya maendeleo, hii inampa heshima
safi sana @chaggabarbie naomba nijue siri ya
utulivu wako, inapendeza sana.
3. Huddah kama hayuko airport, hotelini basi
swimming pool @huddahthebosschick unapenda
kuogelea we mtoto, umekaa kibiashara tu mara
photo shoot, lebel yako ya mavazi iko hewan na
mengine atleast unaonekana unafanya kazi. Hizo
bikini ukiziweka sokoni utauza sana. Hongera
4. Masogange, picha nyingi yuko kitandani, kama
sio kitandani bafuni kama sio nje ya nyumba
then anarudi kitandani anajipiga mapicha weee
hadi analala. Hongera nawe @officialagnes
Mungu kakupendelea sana.
Kuna wengine humu nashindwa kuwaelezea
kwakweli…sitaki kujua sana maisha binafsi ya
mtu ila natamani kujifunza au tujifunze kupitia
hao “mastaa” Hakuna asiyependa kupiga
mapicha all the time kalala, anaogelea, kwenye
mahoteli makubwa na maboti anaenjoy maisha
kama mnaweza kupiga mapicha hayo jamani
tuonesheni na kazi zenu nasi tutamani kufikia
huko?? |
0 comments:
Post a Comment