Saturday, October 11, 2014
null
 |
| MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameichezea
tena kwa mara ya kwanza Uruguay baada
ya miezi minne ya kutumikia adhabu ya
FIFA kwa kumng'ata begani Giorgio Chiellini
wa Italia- kufuatia kuiongoza Uruguay
kupata sare ya ugenini 1-1 na Saudi Arabia.
Mshambuliaji huyo mpya wa Barcelona
mwenye umri wa miaka 27, alipiga shut zuri
la mpira wa adhabu ambalo
liligongwa mwamba kabla ya beki Hassan
Muath Fallatah kujifunga dakika ya 47.
Hata hivyo, bao la Suarez ambaye
alipunguziwa adhabu na Mahakama ya
Usuluhishi ya FIFA (CAS) na kuruhusiwa
kucheza mechi zisizo za mashindano, bao
lake halikudumu kufuatia Naif Hazazi
aliyetokea benchi kuisawazishia Saudi
Arabia dakika ya mwisho.
Amerudi; Luis Suarez akipongezwa na
wenzake jana baada ya kusababisha bao la
kuongoza la Uruguay
Baada ya mechi, mchezaji huyo aliyehamia
Barcelona kutoka Liverpool msimu huu kwa
dau la Pauni Milioni 75, alisema: "Furaha
kuvaa jezi hii tena ambayo inanipa
mimi raha mno. Huwei kupoteza mapenzi
yako kwa jezi. Uruguay!' Suarez, ambaye
katikati ya mchezo aliomba ruhusa kwenda
chooni mara moja na akakubaliwa na refa,
kwa ujumla alicheza vizuri kwenye mchezo
huo kabla ya kumpisha mwenzake dakika ya
70. |
0 comments:
Post a Comment